Tuesday, November 24, 2009

Miwani ya jua unayoivaa ni salama kwa macho yako?


Wengi wanapendelea kuvaa miwani bila ya kupata ushauri wa daktari huku wengine wanaamua kuvaa miwani bila kuwa na tatizo lolote kwenye macho yao ili mradi wanaona miwani inawapendeza. Miwani mingi ya macho inatumika bila kuwaona wataalam wa macho hiyo ni hatari kubwa sana kwako.
Leo tunazungumzia kuhusu miwani ya jua. Wengi wanapenda kununua miwani hii mitaani na kuijaribu na kama wanaipenda wanaamua kuivaa.
Kuwe na mvua au jua watu wengi hupendelea kuficha nyuso zao kwa miwani kwa jinsi wanavyotaka.
Unaweza kuwa na miwani yenye fremu nzuri na kioo cha kutia nakshi lakini je uko kwenye vipimo vya macho?
Yaani miwani yako hiyo inakidhi kweli mazingira ya kukukuhami na jua? Vipi shauri wa miwani inayoacha nafasi ya kuhangaika kuangalia juu au chini na wakati mwingine kioo hakifai kabisa, tazama pamoja na urembo huenda ukapata mikunjo ya ngozi na hili hutalipenda.
Kama unaweza pata ushauri wa daktari kama hujaamua kuwa na miwani kwa ajili ya usalama na ulinzi wa macho yako.

Pendezesha makalio yako kwa kufanya haya


Makalio yetu ndiyo yanayotoa shepu fulani kwa mwanamke katika vivazi na ukiyaachia ovyo yanaweza kukuletea mushkeli na kama ukiyatengeneza hata yale makalio yanayosifiwa sana.
Wanawake wengi kwa sasa wanapenda kurekebisha makalio yao ili kuyapatia ukubwa unaostahili kwa jinsi wao wanavyopenda.
Tatizo hili halipo hapa nchini lakini wapo walionitupia swali na sasa inabidi nikiri kuwa lipo sana Marekani na mpasuaji wa masuala ya urembo wa Miami Dk Constantino Mendieta amethibitisha.
Mtaalam huyu amezungumzia sana utunzaji wa makalio daraja la kwanza ndiyo yanayotakwa sana. Ni kama vile umeuchukua moyo halafu ukaugeuza chini juu,haya ndio dizaini ambayo Marekani wanalilia sana.
Watu wa huko wanajimwaga katika majumba ya upasuaji kupata shepu hiyo adimu, na anayewachengua sana.
Kama unataka kuwa na shepu bomba fuata hatua zifuatazo:
1. Fanya masaji na losheni zinazoimarisha na kutengeneza ngozi nyororo katika mapaja yako,ukianzia chini ya makalio mara mbili kwa siku.
2. Ondoa miinuko midogo midogo isiyotakiwa nyuma yako kwa kuskrabu mara mbili au tatu kwa wiki ukiwa na salt scrub.
3. Pamoja na matatizo ya michuchumio,ivae ili kukupata nafasi ya kutembea kwa miondoko ya twiga inayotoa nafasi nzuri kwa makalio kuwa na mvuto.
4. Tafuta namna nzuri ya kuficha michirizi ya kunyooka kwa misuli ya mwili.
5. Mazoezi yatakufanya uwe mtu tofauti zaidi, pandisha ngazi kwa dakika kumi au zaidi na kisha chukua mazoezi ya kubana makalio yako na sehemu ya kiuno kwa kusukuma kwa ndani na kutulia hivyo kwa sekunde tano na kujiachia na unaweza kufanya hivyo unavyotaka.
Pia unaweza kuongeza uzuri wa makalio yako kwa kuhakikisha kwamba unakula vyema na unakula lishe inayostahili.

Umakini watakiwa katika chaguo la viatu


Unapoamua kuvaa aina ya viatu unakuwa na sababu za aina mbalimbali. Wengi hupendezewa na uvaaji wa viatu virefu na wengine hupendelea kuvaa viatu visivyo na kisigino flat shoes.
Wengi wetu hasa wakinadada wamekuwa wakipenda zaidi kuvaa viatu virefu licha ya kujua kuwa wakati mwingine viatu hivyo huleta madhara katika afya zao. Mara nyingi viatu virefu vimekuwa vikivaliwa na watu ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu kwa kutumia miguu na hivyo kuharibu afya za miguu yao.
Kwa upande mwingine flat shoes vimekuwa vikivaliwa sana na watu ambao wana uzito mkubwa na wale ambao hawapendi kuvaa viatu virefu.
Pia viatu hivi vimekuwa vikivaliwa kulingana na aina ya nguo uliyovaa kwani wakati mwingine nguo huendana na aina ya viatu kitu ambazo watu wengi huwa hawakizingatii mavazi mengine yanatakiwa kuvaliwa na flat shoes.
Na kitu kingine cha kuzingatia ili upendeze na aina hii ya viatu unatakiwa kuchagua vinavyoendana na rangi ya nguo uliyovaa.
Kuna aina nyingi ya viatu vya aina hii ambavyo vimekuwa vikiuzwa madukani lakini ni muhimu wakati unataka kununua kiatu cha aina hii unatakiwa kuzingatia malighafi ambayo imetengeneza kiatu.
Viatu vya ngozi huwa ni vizuri zaidi kwani huvaliwa muda mrefu bila kuharibika tofauti na viatu vya plastiki ambavyo hudumu kwa muda mfupi na kuchanika chanika.

Thursday, October 22, 2009

makosa tunayofanya katika kufanya urembo wetu


KUNA makosa mengi sana yanafanywa na watu katika juhudi za kubaki mrembo au kusaka urembo. makosa haya mara nyingi yanaleta matatizo makubwa hasa katika ngozi , macho au katika kichwa.
mara nyingi shughuli hizi za urembo wanawake hujikuta ama wanapitiliza au wanafanya kinyume na kutaka matokeo ya haraka na matokeo yake ni msheshe.
Mambo yanayoharibu katika urembo ni pamoja na kutokuangalia fiziki yaani kutofanya mazoezi. Hata kama hakuna mtu ambaye atakuona kuacha kufanya mazoezi, kutojali usafi kunatibua muonekano wako na kuondoa kujiamini.
Kitu kingine ambacho watu huwa hawakijali ni kusafisha na kurekebisha meno yao. Unapotabasamu kitu cha kwanza kuonekana kwa watu ni meno yako. basi jaribu kuyajali kidogo. yasafishe na hakikisha yanapendeza.
Kitu kingine ambacho huwa watu hawajali ni kuhakikisha kwamba mikono yao i safi na isiyokuwa na mikwaruzo. Usisahau kuitia mikono yako losheni na kuweka kucha zako safi na zinazopendeza na rekebisha kucha hizo.
Usizivuruge sana kope zako, jaribu kutafuta kitu kitakachopendezesha kope zako na kama kuna makosa usizigandamize bali weka kinachotengeneza uonekano safi.
Kuwa mwangalifu na vitu unavyotengeneza au unavyodhani vinafaa kw aurembo wako. vingine vina aleji viogope. na ukipata aleji usikimbilie kujaza kitu kingine bali angalia nini na tafuta suluhu yake kwanza.
La maana ni kuwa ni vyema kujaribu kwanza kitu katika kiganja au mkono mahali padogo kabla ya kuanza kutumia inavyostahili hasa kwa bidhaa unazotengeneza mwenyewe.

Vyakula vya kuleta ashki

Moja ya vitu ambavyo humfanya mtu kuwa na furaha na maisha mazuri ni ubashashi unaombatana na kuondoka kwa mikonjo ya moyo kwa kupata huduma ya ngono.
Nyingi ya dawa zinazoleta hamu ya ngono puia husaidia kurekebisha mfumo wa afya ya mwanamke, ndio maana nimetaka kwa hapa kidogo kuzungumzia vyakula vya kuleta ashki
Watafiti wamesema kwamba kuna aina fulani ya vyakula huleta ashki kubwa kiasi cha kuwafanya watu wawe na hamu ya kufanya ngono.
Vyakula hivyo vimedaiwa kuwa na aina fulani za kemikali ambazo hufumua mifumo ya tamaa na kufanya dai la kufanya ngono kuwa na nguvu zaidi.
Kutumia chakula kitamu kwa upungufu na kupata lishe kamili yenye uhakikakunaweza kukufanya wewe kufurahia ngono na kutamani kama masuala hayo yameanza kukimbia.
Yaani ukipata dozi inayotakiwa ya protein, carbs, na fats ni dhahiri utakuwa na nguvu zaidi kuliko hapo awali.
Lakini kabla sijakuchanganya zaidi natakakusema kwamba kuwa na nguvu ni kitu kingine na kuwa na hamu ya kufanya ngono na kuimudu ni kitu kingine.
Yaani ukiwa na uwezo wa kufanya mapenzi na kuwa na nia ya kufanya mapenzi kunatokana na wakati wmingine na aina ya chakula unachokula.
Wazungu wanasema kwamba vipo vyakula ambavyo kwa mchanganyiko wake vinbatoa kitu kinachoitwa kwa kizungu aphrodisiacs, yaani vitu ambavyo vinapandisha libido na kuachia tamaa kubwa ya ngono.
Vyakula hivi vinapunguza rehemu vinaweka sawa kiwanda cha kufanya mapenzi, vinaleta riha nzuri zaidi na kuweka homoni katika namna ambayo inastahili.
Pamoja na kukuongezea hizo hamu lakini vyakula hivyo pia vinatoa nishati ya kukutosha kufanya mapenzi.
Wapo waswali wanaokula ngisi, wapo wanaokula karanga, wapo wanaokula muhogo mbichi, wapo waanaolitengeneza vyema tui la nazi, wapo wanaojua kutumia machicha lakini ninachotaka kusema kama nilivyosema hapo juu ni namna tu ya kupiga chakula ambacho kina kemikali zenye viamsha nyege.
Pia kuna aina ya mvinyo ambayo humfanya binti awe na hamu kubwa ya kufanya mapenzi. wapo wanaozungumzia divai na wapo wanaozungumzia amarula.

Uzito mkubwa si sahihi kwa afya na urembo wako


TUMEKUWA kila siku tukizungumzia masuala ya kuweka ngozi safi na sura bomba lakini mara zote huwa tunasahau kuzungumzia uzito ambao ama hakika ni kitu kibaya kuliko kitu chochote kile.
Uzito ni sawa na uvuitaji wa sigara ambao huleta matatizo makubwa kwa watu ambao wamo katika kilinge hicho.
wataalamu wa afya na urembo wanasema wazi kuwa kuwa mnene kunapunguza sibtu namna ya kujiweka sawa katika masuala mbalimba;li ya kijamii lakini pia unakuwa na muda mfupi sana wa kuishi duniani.
Wataalamu wanasema kwamba kuwa mzito kunapiunguza maisha yako kwa miaka mitatu anasema mtafiti Gary Whitlock kutoka Clinical Trial Service Unit ya chuo kikuu cha Oxford kilichopo nchini Uingereza.
Uzito huu ni ule unaokuwa mara tatu ya uzito ambao unhatakiwa mtu awe nao kutokana na urefu wake,umri na pia afya yake.
Ndio kusema kama mtu anakuwa na uzito mathalani paundi 150, mtu huyu anapunguza umir wake w akuishi hapa duniani kwa miaka 10.
Sasa kama unapunguza umri huo watu wako wanakupenda wtafanaya nini.
Kwa maelezo mengine ni kuwa uzito wa aina hii ni sawa na uviutaji wa sigareti ambapo pamkoja na kuchakaza ngozi pia hupunguza maisha ya mtu kwa miaka kumi.
Ndio kusema katika urembo pamoja na kupiga vita sigareti uzito wa kuchusha nao lazima upigwe vita.
Kwa wanawake wengi wa kiafrika wanadhani kuwa mnene ni kuonekana bomba, pamoja na kuwa mnene ni kutamu kwani unakuwa na nyama za kushikwa lakini ni vyema watu wakatambua kwamba uzito wa kuchusha yaani mara tatu ya ulke unaostahili kuwa nao ni hatari kubwa kwa maisha yako.
Onyo hili la wataalamu limefanywa baada ya uchunguzi kwa watu 894,576 waumde kwa wake katika tafiti 57 zilizofanywa.
ingawa tafiti hizi zilifanywa kwa watu wa Kaskazini mwa Marekani na Ulaya kwa watu wenye ujazo wa 25 (BMI) hata hapa nchini watu wanastahili kuangalia juzito wao.
Kwa taarifa yako uziuto wa kuchusha hule ta tatizo la figo, ini na aina kadha za kansa na pia hyuleta matatizo ya magonjwa ya moyo na kiharusi. Unene huleta mchosho mkubwa kwa moyo na pia kuleta mizania dhaifu ya rehemu na kusababisha shida katika mwenendo wa damu.
Wanaume wenye kiuno kikubwa huongeza hatihati ya kifo wakatiw nawake wenye mzunguko mkubwa huongeza hati hati ya kifo kwa asiulimia 78.

Wednesday, October 21, 2009

mambo yanayofaa kwa miguu minene


Ni kasheshe kubwa kuirembesha miguu mikubwa, lakini ni kweli kuwa unahitaji miguu yako hiyo kuwa na nafasi kubwa ya kuonyesha uzurui ulionao.Kipendezacho ni chako.Miguu mikubwa si mwisho wa fasheni unachotakiwa kujua ama hakika ni namna ya kuiweka vyema miguu yako na uonekane bomba.
Wapo watu ambao wamekuwa na miguu mikubw akutokana na sababu mbalimbali na pamoja na kuwa na miguu hiyo wka sababu ama z alishe au kutofanya mazoezi wewe kama binti au mke unataka nguo zako zisiwe na ubazazi na badala yake zionyeshe raslimali ulizonazo yaani uzuri wako.
Kama unataka kuweka miguu yako mikubwa katika hali bora ni lazima uanze kula lishe njema na pia kufanya mazoezi.
Kitu kingine kizuri kwa wewe mwenye miguu mikubwa au tuseme minene ni kuhakikisha kqamba unavaa nguo zinazofiti lakini nguo zinazobana sana si nzuri hata kidogo na zilizopana kabisa nazo mbaya kwani itaonekana mkiguu yako ni mikubwa sana kuliko unavyofikiri.
Wakati unavaa suruali mathalani, vaa ile ambayo ni pana ambayo haipigii tambo miguu yako.
na kama ni viatu lazima uwe unavijulia kwelikweli hata siku moja usivae buti na sketi ambayo inaonyesha miguu yao waziwazi.
nataka kusema hivi kuwa na miguu minene au tuseme mikubwa si tatizo, tatizo ni wewe namna unavyofanya mambo na namna unavyojiweka katika maizngira ya kupendeza na nguo zako za kupendeza ambazo hazibani wala hazipwai.
Na pia unaweza kwa namna nzuri kabisa kuachana na sketi na pensi nyanya ambazo zinakata laini ya miguu yako kama enka nakadhalika.
tengeneza staili ambayo utaonekana wa kawaida na u mrembo katika hilo.

Monday, September 28, 2009

Jinsi ya kuondoa kikwapa

Huhitaji fedha za kigeni kuondoa kikwapa .Ni juhudi ndogo tu ya kawaida ya usafi inaweza kukusaidia.Malimao na ndimu na vitu vyenye uwezo mkubwa wa kuondoa harufu na uchafu katika kwapa.
Wengi wamekuwa wakitumia sabuni, krimu na hata pafyumu za aina mbalimbali kwa ajili ya kuondoa uchafu wa kwenye kwapa lakini bila ya mafanikio yoyote.
Matumizi ya ndimu na limao yana matokeo mazuri kwamwili wako kama utatumia kikamilifu.
Unachotakiwa na kufutafuta limao au ndimu unaikata kisha unakamua. Chukua kitambaa weka maji maji ya limao na kisha anza kusugua taratibu kwapa lako.
Hakikisha unafanya hivyo wakati ukiwa umetoka kuoga. Pia unaweza kukata limao au ndimu bila ya kukamua na kuanza kusugua katika kwapa lako. Vitu hivyo vina nguvu za kuondoa uchafu katika kwapa.
Ni muhimu kusafisha kwapa kwani kwapa linapokuwa si safi hata unapovaa nguo ya wazi unakuwa huna uhuru wa kunyanyua mkono juu pindi inapokulazimu kufanya hivyo.
Kwapa ni sehemu muhimu sana ni lazima iangaliwe kwa namna ya pekee na uhakikishe unakuwa safi muda wote ili kuondoa harufu na muonekano mbaya katika kwapa.

Umuhimu wa manukato katika urembo wako

KARIBUNI wasomaji katika blogu hii ya urembo na utanashati.Leo naona tuzungumzie jinsi manukato yanavyoweza kuwa na manufaa katika urembo wako.
Ukitaka kuwa mrembo ni wazi kuwa unatakiwa kuuweka mwili wako katika hali nzuri ya kupendeza kuanzia mavazi, mitindo ya nywele.Ndio kusema kuna vikorombwezo kibao vinavyotakiwa ili kukufanya uwe mrembo zaidi.
Manukato nayo ni muhimu katika kunogesha urembo wako.Nadhani ulishawahi kusifiwa au kusifia mtu kutokana na manukao anayotumia na wengi wetu tumekuwa tukitumia aina za manukato ambazo tunaona zinatufaa zaidi.
Ni vizuri kuchagua aina ya manukato na njia nzuri ni kupulizia kigogo kwenye mkono wako ili uweze kujua harufu yake kama umependezwa nayo au laa. Usitumie manukato ya aina fulani kwa sababu fulani anatumia.
Jaribu kutafuta aina ya manukato uliyoyachagua kwani kuwa mnukato yana harufu kali na hili huleta taabu kidogo kwa baadhi ya watu unaokuwanao karibu.
Chagua manukato ambayo yana harufu iliyotulia na pia ukali wa manukato wakati mwingine husababisha kujipulizia kiasi kikubwa cha manukato hali ambayo huwa kero kwa wengine.
Jaribu kutumia manukato kiasi fulani kwani aina nyingine hudumu muda mrefu na unapojipulizia manukato ona unafanya hivyo kwa faida yako na sio kuhakikisha kuwa kila mtu anajua umetumia manukato ya aina fulani hapo ndiyo huleta shida kidogo kutokana na kutumia kiasi kikubwa cha manukato na hivyo kuleta shida kwa wengine.
Pia unashauriwa kutotumia manukato ili kuondoa harufu ya mwili kutokana na kutooga au kutokana na sababu nyingine hapo maana ya manukato hupotea. Manukato hupendeza iwapo yatapuliziwa wakati mwili na nguo zikiwa safi. Tumia aina ya manukato uipendayo ili kuweza kukuweka mrembo zaidi.

Namna ya kuondoa vipele na mafuta usoni

Ukiwa mwanaume au mwanamke upigaji sopusopu ni jambo la busara sana ili kukuweka mtanashati na mwenyekuvutia muda wote kwa kuondoa uchafu na pia kuondoa mafuta ambayo yana kawaida ya kutanda katika sura.
Kitendo hicho huitwa scrub.Husaidia kuondoa chunusi,vipele na makovu na pia inapunguza mafuta usoni.
Uso unapokuwa na mafuta sana na kuyaondoa kunasaidia kupunguza vitu vingi pamoja na vipele na hata mabaka yaliyosababishwa na vipele au chunusi.
Unaweza kutumia scrub ya kwa njia ya mikono kwa kila baada ya siku tatu, na scrub ya mashine baada ya mwezi mmoja.
Scrub ya mkono.Tafuta aina ya scrub inayokufaa kulingana na ngozi yako.safisha uso wako mpaka uhakikishe kuwa umetakata kisha chukua scrub na kuanza kusugua usoni taratibu kwa muda wa dakika tano kisha nawa uso na unaweza kupakalosheni au poda baada ya kunawa.
Scrub ya mvuke.Chesha maji Nawa uso kwa kutumia maji safi na uhakikishe kuwaumetakata.
Futa uso kwa kutumia taulo safi.
Paka scrub usoni na pia shingoni kama utapenda. Sugua uso kwa kutoa taka.Chukua taulo jifunike na kisha inamia beseni lenye maji ya moto.Baada ya dakika tano toka na subiri kwa muda wa dakika tano nyingine kisha nawa. Paka poda au losheni.
Pia unaweza kutembelea saluni za kisasa kwa ajili ya kuufanyia facial uso wako Pia unaweza kutafuta sabuni ya ukwaju na ukawa unanawa uso asubuhi na jioni hii huondoa upele, chunusi na mabaka usoni

Thursday, September 17, 2009

namna bora ya kutunza miguu



Sasa tuzungumzie juu ya utunzaji wa miguu. Miguu ni sehemu inayoangaliwa sana hasa kwa wanawake, kwani unapoamua kuvaa nguo fupi na huku miguu yako haiko katika hali ya kuvutia sina shaka utaanza kujishuku hata kabla ya kutoka nje.

Miguu ni sehemu ambayo inatakiwa kutunzwa kwa kipekee kama ilivyo sehemu nyingine kama uso. Wengi tumekuwa tukipendezesha nyuso zetu na kusahau kbisa habari za miguu.

Haijlishi miguu yako ni miembamba au minene iwapo utaitunza vizuri sina shaka kuwa utavutia kwa nguo yoyote utakayoivaa.

Kuna njia nyingi za kutunza miguu na unaweza kutunza miguu yako hata kama huna fedha za kununulia vikorokoro vinavyotakiwa.

Unaweza kuchukua beseni na kuweka maji ya uvuguvugu yenye povu la sabuni maalum ya kuoshea miguu kisha loweka miguu na iache kwenye maji kwa muda wa robo saa hivi.

Chukua aina ya scrub uliyoichagua kwa ajili ya miguu yako paa na ikikauka anza kusugua miguu yako na hadi kwenye vidole na unyayo.

Kisha jisafishe kwa maji ya uvuguvugu.

Baadhi ya vitu unavyoweza kutumia ili ku kutengeneza miguu yako ni pamoja na foot file, Therapysa virgin vie salt scrub, Pedicure iliyotengenezwa kwa OPI Refresh Cooling ffot Gel, Innoxa cool na Calm liquid talc na Feet first reviving Foot Soak.

Bidhaa hizi unaweza kuzipata kwenye duka kubwa la vipodozi na pia utpata maelezo jisi ya kutumia

Pia unaweza kutembelea baadhi ya saluni ambazo zinatoa huduma hiyo jitahidi hata mara moja kwa mwezi kuhakikisha miguu yako inapata huduma nzuri ili iwe ya kuvutia.

Kwa wale ambao miguu yao ni makovu au madoadoa wajaribu kutumia scrub na kama hawatafanikiwa kuondoa tatizo hilo basi wanashauriwa ktumia cream na sabuni zenye mchanganyiko wa ukwaju kwani zinasaidia sana kuondoa madoa.

Pia unaweza kuchukua mkwaju ukaloweka kwenye maji ukishalainika changanya mchanganyiko huko na asali kasha paka.

Husaidia kuondoa madao na hata kwa wale wenye ngozi za mafuta na chunusi sugu mafuta yatakauka na chunusi hazitatoka tena.

Namna ya kuhami ngozi laini inayozunguka jicho


Ngozi yako inayozunguka jicho ni sehemu muhimu sana kwani ina ulaini na inahitaji uangalifu mkubwa.
Sehemu hii ya ngozi ni nyembamba mno na inaweza kupata madhara na kitu kidogo kabisa ili hali inaweza kuzeeka mapema kabisa kabla ya muda wake.
Ndio kusema lazima ufanye mambo fulani kila siku, mchana na usiku, ili kuhakikisha kwamba sehemu hii inabaki vyema kama inavyostahili.
Swala la kwanza muhimu ni kwamba ni lazima uoshe vitu vyote ulivyotumia kuremba jicho lako kwa kutumia visafishaji ambavyo si vikali.
Bidhaa nyingi zinazotengenezwa kuondoa make up katika jicho zimetengenezwa katika mazingira ya kuhakikisha kwamba ngozi inabaki hai na isiyokuwa na matatizo.
Moja ya kisafishio kizuri amnacho kina uasili ni kile cha witch hazel.Bidhaa hii inafanyakazi ya kuondoa make up huku eneo likiachwa katika hali yake.
Inatakiwa kila asubuhi unapoamka asubuhi ni vyema ukaanza na eye gel au krimu yenye unyevunyevu na unapoenda kulala wakati wa usiku.
Kwa kuwa umri unavyozidi kuongezeka ngozi huacha kujirejesha inavyotakiwa na huondoa ule ulaini wake iliokuwa nao kwanza kuhakikisha kwamba eneo hilo lina unyenyevu husaidia kuweka ngozi ile katika hali bora zaidi.
Ni vyema ukahakikisha kwamba moisturizers unayotumia ina SPF ili kuhakikisha kwamba ngozi inayozunguka jicho inahamiwa vyema dhidi ya mikunjo inayosababishwa na miale ya jua.
Njia nzuri pia ya kupunguza uvimbe wa macho ni kuweka mask kuzunguka jicho.
Pia unaweza kumasaji eneo hili ili kuondoa sumu ambayo imjijenga katika mfumo wa liymph.
Watu wengine huhifadhi eye cream kwenye friji na kutumia kumasaji eneo hilo ili kuondoa mauamivu yanayokuwepo.
Tatizo la mikunjo katika ngozi inaweza kudhibitiwa kw akutumia bidhaa za urembo zenye asidi ya glycolic ambayo pia hujulikana kama alpha hydroxy acid au AHA.
Moja ya bidhaa bora zaidi zinazosaidia kuondoa mikunjo ya uzee kuzunguka jicho ni Olay. kuna bidhaa nyingi bora ambazo zinaweza kabisa kuondoa miukunjo .
Kuna njia pia za asilia mbazo zinaweza kusaidia kuweka sawa ngozi inayozunguka jicho kama vipande vya matango.
Pia unaweza kutumia mafuta olive oil kuzunguka macho yako kila siku na utaona matokeo yake yatakavyokuwa bora.

Monday, September 14, 2009

uondoaji chunusi kwa njia za kiasili


Ukitaka kuondoa chunusi usoni na kusafisha uso usiwena madoa kwa kiasili, njia zifuatazo zaweza sana kusaidia.
Tafuta ukwaju loweka katika maji ukishalainikachanganya na asali, paka usoni.
Ni dawa nzuri sana na utaona ngozi yako inabadilikakwa kipindi kifupi.
Kama utashindwa kupata vitu hivyo tafuta sabuni pamojana krimu yenye mchanganyiko wa asali na ukwaju.
Sabuni hiyo iko katika boksi kubwa na kwa ndani inakigunia ambacho kinasaidia kusaficha uso, usinunue sabuni ya ukwaju na asali ambayo haijafungwa kwenye kitambaa kigumu chenye rangi ya kahawia itakuwa ni feki na haitakusaidia.
Kama unataka kupunguza tumbo au mwili kwa ujumla.Asubuhi kunywa chai nzito, mchana kula chakula kilichokamilika.
Ila usiku kula matunda tu ili uweze kuupa mwili nafasi ya kujitengeneza na hasa kupunguza mfuta yaliyozidi mwilini.
Uwe unakula wakati unasikia njaa tu unapokula bila yakusikia njaa unakuwa unarundika tu chakula mwilini na baadaye chakula hicho hubadilika na kuwa mafuta ambayo
hutengeneza manyama uzembe.
Ukishindwa hivyo nenda kwa daktari iliakupe masharti ya vyakula na uweze kupunguza mwili

Jamani hebu hurumieni nguo zenu, zitunzeni


Watu hutumia mamilioni kama si maelfu ya fedha zao kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wanakuwa bomba na wenye kuvutia. Lakini ni kawaida mno kuona watu hao hao wakitupa fedha hizo kwa kuzivuruga nguo zao na kuziweka pasipo heshima kiasi ya kwamba huchakaa haraka au huharibika kwa muda mfupi sana.

Wengi wetu ambao tuna haki ya kujiita watanashati tuna matatizo makubwa sana ya utunzaji wa nguo zetu na wakati mwingine tunasahau kwamba nguo hizo ni raslimali zetu ambazo zikiharibika na sisi vile vile tunaharibika.

Mathalani mtu ananunua nguo kwa paundi 4000, fedha nyingi kabisa, lakini mtu huyu ambaye alitakiwa kuheshimu nguo zake unaweza kuingia chumbani mwake ukazikuta zimetupwa tu holela kitandanim, kwenye kochi na wakati mwingine hata bsakafuni.

Wewe mtu anavua suti na kuitupa, mtu anavua sidiria na kuitupa yaani mambo yote hata hayaeleweki.

Lakini nataka kusema hivi unapokuwa unabadilisha nguo kumbuka kuzihifadhi na kuzitunza kwani hiyo ni raslimali zako mwenyewe.

Kutokana na hali hiyo nataka kukueleza kuwa nguo ziku zote zinatakiwa kuwekwa kwa urefu wake ili zirejee katika hadhi yake ya kawaida.

Ni vyema kwelikweli na nasisitiza kuweka nguo zako kwa kuzitundika ili zirejee katika ule uzuri wake wa dukani na katika matenegnezo.

Ni vyema kama kabati lako halina nafasi ya kuweka vining'inizo ukaviweka kwani ni vya maana sana hsa vile vilivyotengenezwa kwa mbao.

Na wakati mwingine tumia vishikizo ambavyo vinasimamiwa pia na vitu vngine. Ninachotaka kusema hatakama ni sketi iweke katika nafasi yake inayostahili.Vivyo hivyo kwa jaketi na suruali na hata mashati.

Pamoja na kuweka nguo yaani kuzitundika ili kupata uhalisi wake ni vyema pia kuwa na mpango katika kabati lako si tu kujifanyia mambo kama mwendawazimu.Manake kama hukuwa na mpango itakuchukua siku nzima kujua ni wapi umeweka brazia au nguo yako ya ndani.

Ni lazima siku moja uamue kufanya ratibu ya kabati ili liwe na maana kubwa kwako na kukuwezesha kufanya maamuzi ya kasi wakati wa kuchagua nguo za kuvaa ziwe za ndani au nje.

Naomba usiruhusu kwa namna yoyote ile uwekaji wa mifuko ya nailoni kwani hutunza hewa ya unyevu na hii huleta uvundo katika nguo.

Pia kufanya mambo yako yawe bomba tafadhali fanya mambo mawili. Moja hakikisha kwamba nguo za zamani unazitoa ambazo zimemalizika muda wake wa fasheni.

Na maana kubwa sana ni kuwa upangaji husaidia pia kukuwezesha kufanya mambo ambayo pengine huyapati kwa uzuri kuwa na nafasi ya kuona.

Utunzaji wa nguo hauko tu katika kuziweka vyema bali hata wakati wa kufua,Angalia kwa makini maelezo ya nguo zako, maji yanayostahili kutumika joto na pia aina ya sabuni. Na ukishamaliza basi zinyooshe kama zinavyotakiwa.

katika masuala haya ni pamoja na viatu kuangaliwa, kusafishwa na pia kutunzwa kwa mujibu wa maelekezo ikiwemo ya utiaji wa kiwi.

Wednesday, September 9, 2009

Umaridadi wa kupaka rangi kucha


Ili uwe na kucha maridadi masuala ya kuzisafi na kuziweka rangi ni muhimu ama sivyo? na kwa kawaida kucha zilizo safi ndizo hasa zinazokubali polishi yaani rangi au sivyo?

Na ama hakika kucha zilizo safi ndizo hasa zinazotengenezwa na kuwekwa sopusopu.

Ni vyema kutambua kwamba wakati wa kupaka rangi tumia mipako michache kwa kila mpako na kila mpako uachie ukauke kabla ya kuanza mpako mwingine.

Na ile ya mwisho inatakiwa kuwa bomba zaidi kwa kuwa ndio hasa itakayokuwa inatunza matabaka mengine yote.

Utengenezaji mzuri wa kucha si lazima uwe wa kwenda katika mapumziko au kuonyesha mtu ni kitu ambacho kinafaa kufanywa ili uwe mrembo kila mahali.

Kuna raha ya kujisikia katika rangi mpya katika mwaka mzima na hasa kama uchaguzi wako wa rangi za kupaka ni bomba.

Moja rangi ya pinki ama nyekundu inakupa nafasi ya kuwa funny . Unaweza kujipaka rangi mwenyewe au kuwambia mtu akupake rangi.Kuna hatua kadhaa ambazo unatakiwa kuzifanya kabla ya kupaka rangi kucha zako.

Hatua ya kwanza ni kuondoa rangi zote za awali.kwa kufanya hivyo rangi mpya itakuwa ina uwezo wa kushika katika kucha.

Pia kunasaidia rangi yako mpya isitibuliwe na rangi ya zamani kwa namna yoyote ile.

Unaweza kuondoa rangi ya zamani kwa kutumia dawa inayopatikana katika maduka ya dawa na hata yale ya vipodozi na pamba hufanya vyema kartika kuondoa rangi za kucha kwa kutumia Nail polish remover.
kazi ya pili ni kutafuta rangi inayokupendeza. unaweza kutumia rangi yoyote kwa sababu mara nyingi viatu vinazuia kuonekana kwa kucha zako la kama unahitaji rangi fulani kwa sababu miguu yako i wazi ni vyema sana.

Tazama kwamba vipaka rangi vyenyewe ni vipya kwani vilivyozeeka huleta tatizo kidogo.mara nyingi vipaka rangi vilivyokaa miaka miwili havifai tena kutumika.

Anza kupaka baada ya kubainisha kwamba unaweza kutenganisha kidole kwa kidole ili usipake kila mahali hasa kama brashi husika ni pana kidogo.

Anza katikati kwa kuanzia nyuma kupeleka mbele kisha nenda pembeni na pembeni.Na baada ya kukauka unaweza kuongeza tabaka jingine tena na tena.

Kisha paka ile ya mwisho ambayo ndiyo italinda rangi yenyewe yaani top coat . top coat husaidia sana kuweka rangi kwa muda mrefu. Top coat ni polishi isiyokuwa na rangi na kama unataka kuweka stika iweke mapema kabla ya kuweka top coat.
rangi nzuri na zilizotulia zinakufanya uwe na sababu ya kujivalia sandals zako nzuri au viatu vya wazi

Monday, September 7, 2009

Viatu visivyofaa vitakuletea ugonjwa







Wanawake wana kazi kubwa katika kuhakikisha wanaonekana wapo warembo na wana urefu unaotakiwa. Katika hali hiyo inaaminika kuwa katika wanawake wanne kati ya kumi wananunua viatu visivyowafaa wala kuwatosha.
Kura ya maoni iliyohusisha watu 2000 iliyofanywa na The Society of Chiropodists and Podiatrists imeonyesha kuwa asilimia 37 huvaa viatu vinavyowapa shida ili mradi tu wawe katika fasheni.
Asilimia 80 ya wanawake wanasema kwamba hali hiyo huwafanya wapate matatizo ya miguu kama kuota vigimbi , ukuaji wa kucha usiostahili lakini hawatafuti hata msaada wa daktari.
Lorraine Jones, kutoka Society of Chiropodists and Podiatrists, anasema kwamba hili tatizo la kutaka fasheni linaharibu afya za wanawake.
Inashauriwa kwamba mwanamke avae kiatu ambacho hakina urefu wa zaidi ya sentimeta nne na pia kina uduara kwa mbele.
Ni vyema mwanamke akaelewa kwamba kama anajisikia maumivu basi mambo si shwari hata kidogo.

Sunday, September 6, 2009

Mikato ya nywele inafaa kuzingatia kichwa











Hakuna kitu kinachofurahisha kama nywele za mwanamke. Nywele za mwanamke zinapowekwa sawa na uso wake, humfanya awe na mng'ao usiokuwa wa kawaida.
Nywele za mwanamke zinaheshimika zinathaminika na ama hakika ni hazina moja ya maana kwa mwanamke iwe zimekaangwa au zimewekwa tu kama vile mchemsho.
Nywele na staili zake hazijabadilika sana ingawa zamani nywele zilikuwa zinawekwa vitu vingi katika mizungusho ya kawaida ya kuremba na wakati mwingine kuachwa tu zikijiotea na wengine wakitumia muda mwingi kuzisuka.
Ni vyema kama mwanamke unataka kupendeza kichwani kufika kwa wataalamu wa nywele ambao watazitengeneza au kukupa ushauri kutokana na kichwa chako na si vingine.
Ni kutokana na hali hiyo lkeo tunakuletea picha mbalimbali za watu na miondoko yao kichwani kwa lengo la kukuonyesha kwamba unachosuka kichwani inafaa kifanane na kichwa chako.
Si misuko tu bali hata utengenezaji wa huria wa kutumia dawa au hata dawa za asilimi ni lazima izingatiwe ukubwa wa kichwa na namna ambavyo ungelipenda wewe uonekane.
Zamani misuko ilikuwa ya kuchekesha zaidi na matumizi ya kofia yalimaliza utata uliopo kichwani kwa wakati unapoangaliwa kwa makini.
Nataka kukuambia kwamba nywele nyingi hutengenezwa kwa kuangalia unataka kumvutia nani na kwanini.

Chumvi,sukari nyingi huzeesha ngozi


Shosti niwaambieni kuwa matumizi makubwa ya chumvi au sukari ni hatari na sumu kubwa katika ngozi zetu kwani husababisha ngozi kuwa na makunyanzi kabla ya umri.

Kawaida makunyanzi hutokea unapokaribia kuimaliza miaka ya 40.Watu ambao ngozi zao zimeathiriwa na matumizi makubwa ya sukari na chumvi wanashauriwa kupunguza matumizi yavitu hivyo kwa kula mboga za majani na matunda kwa wingi ili kuweza kuondoa sumu ambayo imejengekamwilini na pia kunywa maji mengi.

Wanasayansi wanasema kuwa, watu wanaotaka kutunza ngozi zao kutotumia sukari kwa wingi kwani sukari huchangia kuzeesha ngozi. Sukari nyingi hufanya misuli ya protini katika ngozi kujikusanya pamoja na kusababisha kutoweka kwa mnyunyuriko unaotakiwa.

Ili ngozi iwe laini ni yema ukanywa maji mengi, maji husaidia kulainisha miili yetu kwani mwili unapokuwa hauna maji ya kutosha unakuwa mkavu na ngozi haipendezi hata kama unatumia vipodozi vya aina mbalimbali na vya gharama. Ni bora kuulisha na kuunywesha mwili wako ili ngozi ijitengeneze yenyewe.

Wednesday, September 2, 2009

Namna yakujiweka fiti kwa mwanamke


Katika kujiweka fiti au tuseme kujiweka sawa kwa ajili ya kuonekana mrembo ni kazi ambayo inahitaji muda na uvumilivu vinginevyo unaweza kuwa sawa na chizi yoyote aliyejiwekea si tu maleba bali na mwili usiotamanika.

Na kwa mwanamke ambaye ana mji wake, watoto , familia na kazi inayohitaji ukakamavu mkubwa huku akitakiwa kuonekana bomba namchangamfu ni dhahiri kuwa la ziada lazima lifanyike vinginevyo mahali fulani utapwaya.unaweza kupwaya ofisini, ukaonekana huna maana , unaweza kupwaya nyumbani mtoto mkubwa akashindwa kukuangalia mara mbili na unaweza kupwaya mtaani watu wakajiuliza hee mama fulani vipi mbona usafi unamshinda?ndio kusema katika hili unahitaji mwanamke kuwa makini sana.

Inavyoonekana wanawake wengi wanapokuwa katika mtawanyiko wa mambo hujisahau kabisa na mara nyingi husahau kabisa kuwa wanahitaji kula nakufanya vitu fulani ili kujiweka fiti.Kimsingi wanawake wote wawe wanachapa kazi kama wazimu, wawe na familia, wawe na mtoto mkubwa wanatakiwa kujiweka safi na sawa muda wote pamoja na majukumu yao yaliyotawanyika.

1) suiku zote hakikisha una tunda wakati wa kifungua kinywa chako. Hiiinasaidia kuondoa sumu katika mwili wako na kusaidia kuondoa uchafuuliojiweka kwa namna inavyostahili.

2) Kunyw amaji ya kutosha , punguza chai na kahawa kufikia angalauvikombe viwiuli kwa siku na muda uliobaki kunywa vinywaji ambavyo nivya mizizi kama jasmine, chamoile tea. Vinywaji hivi katika mfumoi wajuisi ni dawa tosha kwa ngozi yako na ili ionekane ya ujana muda wotena isiwe kavu.

3) Huku umri wako ukiwa unapanda,punguza vyakula vya nafaka na kulazaidi matunda na mbogamboga ili kupunguza uzito.

4) hakikisha unatembea vya kutosha na kujinyoosha ili uwe na mwili wakuvutia, mwembamba na wenye nguvu za kutosha na wa ujana.
5) Punguza uvutaji sigara na pombe kwani ni vitu viwili vinavyozeeshangozi kwa kasi.

6) Ongeza vyakula vya samaki katika chakula chako au aina yake

7) Uwe unakula na mizizi inayokabiliana na uzee kama tulsi, amla, ashwagandha

8) Jipatie vitamu vya asili kama asali na raisins.

9) Kula vyakula vyako unavyopenda vya hovyo angalau mara moja kwa wiki

10) Kujisikia vyema ni namna bora za kukufanya uwe mwanamke bomba naanayevutia muda wote.

NB:Kujisikia vyema huku ni kujipenda mwenyewe kama hujipendi huwezi kuvutia na kama unaridhika kwa sababu ya kuridhika una tatizo kwelikweli.

Monday, August 31, 2009

NAMNA NZURI YA KUOSHA NYWELE ZAKO



KUNA kitu muhimu kuhusu uoshaji wa nywele, nywele zako ambazo unataka zikae unavyotaka kulingana na kichwa chako ili uwe na uvuto wa haiba yake katika mambo yote yanayokuzunguka.
katika mazingira ya kawaida uoshaji nywele ni kitu cha kawaida na hivyo mara nyingi hatufikirii sana suala la kuosha nywele, si la kawaida tu mwenzangu? Lakini uoshaji nywele wa uhakika wenye makini kwa kutumia shampuu kunaweza kuleta mabadiliko makubwa katika muonekano na umetaji wa nywele zako na hata makuzi yake.
Ndio kusema uoshaji wa kutumia shampuu unaweza kabisa kukupa kile ambacho huwezi kukipata katika hali ya kawaida , muondoko wa ukaaji wa nywele baada ya kuosha.
Lakini kama hutajali tulijadili hili suala la uoshaji nywele ambalo ni la kawaida tu.Naama, la kawaida lakini lenye maana kubwa kwa watu wanaojijali.
Mimi nadhani haitaumkiza kama nikisema kwa ufupi fupi kuhusu hizi shampuu za kuonshea nywele, hizi shampuu ambazo unazipata dukani, kwenye dula la urembo.
Kwanza ni lazima utambue kwamba si kila shampuu inafaa katika kusuklia nyweleza ko (uoshaji) kwani nyingine huleta mushkeri hasa kama unaumwa eczema, hali ya kuchoma choma, uwasho wa nywele, mba au aina ya grisi katika ngozi ya nywele zako wakati wa kuzitengeneza.
Nataka kukuambia kwamba bidhaa zinazotokana na uasili husaidia sana kutengeneza utamu wa nywele kama kweli unaujua na mara zote hufanyakazi bora kwa aina zote za vichwa hata kama zina matatizo niliyotaja hapo juu.
Na pia huleta aina ya burudiko.
Mara zote tunapoosha nywele zetu huwa tunaharibu lakini kama utakuwa mwangalifu kwa kutumia shampuu zenye viambata vya asili (organiki-natural botanical)utakuwa na nafasi kubwa ya kuwa na nywele tamu na wewe kuondokana na adha za uchafu wa nywele unaotia 'wazimu'.
Kama utakuwa huna shampuu ile ya dukani ambayo ina aviambata vya asili nashauri utumie yai. yai ni kifaa kizuri kabisa cha kusafishia.tenganisha kiini cha yai kutoka katika uite mweupe. konga tofauti kisha changanya na taratibu zitumie kuzichanganya katika nywele ne kusukasuka. Acha kwa dakika tatu na kisha safisha kwa maji ya uvuguvugu si ya moto kwani ukitia maji ya moto yao litajikusanya maeneo fulani fulani kichwani halafu itakuwa shida.
Njia tano za kuosha nywele zako:
1.Inama katika beseni. Hii inasaidia kutoa nafasi ya ukaaji mzuri wa kuanza kusafisha nywele bila kuumiza shingo yako na pia kusaidia kuweka damu katika mzunguko unaotakiwa.
2.Tumia kikombe kimoja cha shampuu. Ikiwa nyingi italeta matatizo kidogo na kidogo pia haitatoa kitu kinachostahili. pakaza kwa kusukasuka kila mahali kichwani mwako kwa kuanzia mbele kwenda nyuma na kisha pembeni. Kwa nywele za grisi(mafuta) changanya shampuu na maji kidogo.
3. Tumia ncha ya vidole vyako kufika mwisho wa nywele na kuzimasaji vyema kuhakikisha kwamba shampuu inaingia katika ngozi ya kichwa. Safisha kwa raha kwani inatakiwa ujisikie raha kubwa wakati wa shughuli hii ya kusafisha nywele.
4.Hakikisha kwamba umesafisha sawasawa kichwa chako kisha unaondoa shampuu kwa maji..Kitu cha maana ni kuwa usafishaji lazima ufanyike kwa uangalifu mkubwa kwani baada ya kutia shampuu na kuipeleka kila mahali kuiondoa baada ya hapo ni kitu muhimu.Iondoe kwa maji na kisha kujihakikisha kwamba imeondoka, unastahili kukitia kichwa chako maji ya baridi kwa ajili ya kutoa busti zaidi.
5.Kausha nywele zako kwa taulo safi (kwepa kusugua nywele hizo kwa taulo).Kifunike kichwa na taulo hilo ili linyonye maji taratibu na baada ya hapo unaweza kutia kitu kinachotakiwa ili kuweka nywele za safi.

Miti shamba inayofanya matiti kuwa makubwa na yaliyosimama



MATITI ya mwanamke kuwa katika shepu bomba ni shauri la wanawake wengi na si shauri la mtu mmoja tu. Aidha ni sehemu ya mwili wa mwanamke inayotoa msisimko mkubwa.
Wapo wanawake ambao wana musuli nyingi za matiti na hivyo wanakuwa na matiti makubwa na wengine wana kiasi kidogo na hivyo kuwa na matiti madogo.
Hali hiyo ina sababu zake ingawa wataalamu wanasema kwamba ukubwa wa maziwa huambatana na historia ya familia, umri,kupungua kwa uzito, ujauzito unene na kunyumbuka kwa ngozi ya kwenye matiti, kiwango cha homoni hasa estrogen na progesterone.
kwa kuwa matiti ya mwanamke ni sehemu ya utambuzi wake wa ukike na mwenyewe alivyo na pia ni alama ya uzazi na salama kwa mtoto wake.
Uzuri wa matiti ni kuwa mazima na kama kukitokea kasoro kidogo tu huwa ni kasheshe kubwa kwa upande wa mwanamke. Kutokana na hili nashauri wanawake kuwa na tabia ya kutunza matiti yao ikiwa ni pamoja na kuyakagua na kama kuna kasoro kuyafikisha kwa wahusika kuangalia tatizo.
Usafi wa mwili huambatana na kuyatunza vyema matiti yako.
Lakini wengi wanaotaka matiti makubwa ndio ho wanaopata adhabu ya kusaka matiti hayo kwa udi na uvumba.
Uzuri wa matiti
zipo njia nyingi za kuwa na matiti bomba na kwa sasa duniani matiti bomba ni yale makubwa( nadhani hii ni fasheni).Unaweza kupata matiti hayo kwa upasuaji au na kwa kupachika kitu ndani hasa silikoni na nyingine ni kutumia dawa ambapo misuli hujazia na kuyafanya matiti kuwa makubwa.
Njia ya kukuza matiti kwa salama ni kutumia dawa ambazo zimetolewa katika miti shamba, mitishamba ambayo ikichanganywa pamoja inafanyakazi mbalimbali ya kuboresha ukubwa na uimara wa matiti.
Mitishamba hii inatoka sehemu mbalimbali na Afrika Kusini wamefanikiwa kutengeneza dawa kutokana na miti hii na wanaotaka urembo wa matiti makubwa na yenye kuonekana wanapata nafasi kubwa ya kununua dawa hiyo.
Aidha baada ya kujazia matiti yako na kuwa makubwa kitu kinachofuata ni kuhakikisha kwamba matiti yako hayalegei na kuwa katika ukubwa wake bado yanasimama katika saa inayotakiwa na yenye raha yake si kutazama bali pia kuyatomasa.
Matiti hupendeza zaidi baada ya kuonekana yakiwa yametulia na yanayokubali brasia zenye maana duniani.
Aidha uzuri mwingine utatokana na kuwezesha matiti yako imara kwa kufanyia hali ya kuwezesha musuli za maziwa kufanyakazi yake.
Pamoja na kuongeza ukubwa wa matiti ni vyema kama ngozi yako inakuwa na rangi ile inayofaa huku ukihakikisha kwamba chini ya maziwa jacho halikai na wala brasia haisababishi wewe kuwa na kazi ya ziada katika usafi wa eneo hilo.
Ipo haja ya kutumia mafuta yanayostahili kukata mnururisho mkali wa mwanga unaoweza kusababisha kansa ya ngozi.
Kliniki moja ya Afrika Kusini St Herb Beauty Breast Care imetengeneza aina fulani ya mitishamba yenye mchanganyiko maridhawa kwa ajili ya matumizi ya wanawake wanaotaka urembo wa matiti makubwa na yaliyosimama bila upasuaji wala kutumbukiza kitu katika matiti hayo.
Ni lazima kuwe na mizania ya mitishamba kupata kile kitu unachotaka. Kliniki hiyo imekuja na fomula yake inayoitwa Beauty Bust Herbal Breast Enlargement Formula ambayo hushawishi kukua kwa misuli za matiti bila kushawishi uzalishaji wa maziwa na kuyaongezea uzuri matiti yako.
Pamoja na matiti hayo kuwa bora kwa matumizi hayo, matiti makubwa hulainika sana unapokuwa mzee na hili ndilo hasa nililotaka kusema, mazoezi ya mwili husaidia sana bado kuweka matiti katika shepu yake.
Kama u kijana na matiti yako yanakuwa malapa basi huenda tatizo si tu musuli zimelegea bali pia huvai brasia kukusaidia. maziwa yanaweza kuwa malapa kwa kutokuwa na kitu cha kusaidia kusimama.Hili ni wazi zaidi kwa wanawake wenye matiti makubwa au watu ambao wanafanya mazoezi bila kuwa na sapoti ya brasia.Pia matiti yanaweza kuwa malapa kutokana na kujifungua
Lakini ukitaka uhakika wa uzuri wako kwa namna ya kuwa na matiti makubwa na yalioyosimama vyema ni lazima utumie dawa hizi za matishamba ambapo mchanganyiko wake ndio umetoa fomula ya St Herb :
Fenugreek :
Kwa kawaida matunda ya mmea huu yalikuwa yanatumika na wanawake wa Kigiriki kuongeza ukubwa wa matiti yao na imehakikishwa kisayansi kuwa mtishamba huu huongeza athira ya mastogenic kwa misuli inayotengeneza maziwa.
matunda( mbegu ) ya mtuii huo yalikuwa yanatengeneza aina ya dawa ijulikanayo kama phytochemical diosgenin na estrogenic isoflavones zinazooongeza utengenezaji wa dawa ya estrogen katika mwili, dawa ambayo ni ufunguo kwa matiti yenye shepu ya mchonoko na yaliyojaa.
Mmea wa Saw Palmetto:Huu ni mmea wa kaskazini mwa Marekani na kwamba unafanana na mtende ni moja ya mmea wenye kemikali chache unaotengeneza musuli na husawazisha matatizo ya mkaziwa yenyewe.
Fennel Seed:Husaidia kuzalisha musuli nyingine mpya
L-Tyrosine:Hii ni amino acid, Tyrosine ambayo hudhibiti uzalishaji wa homoni na hivyo kupunguza unene na.
Mexican Wild Yam:Matumizi ya kila siku yanapunguza michirizi isiyotakiwa katika matiti.
Kelp:Ni zao la baharini. Ni chanzo bora cha madini ya iodine chakula chenye hiki huleta homoni zilizojipanga vyema.
Damiana:Kikawaida hutumika kwa ajili ya kuleta mizania ya homoni.Kuleta ukuzi mwema wa matiti, kupunguza dalili za matatizo yanayoambatana na siku za hedhi na kuchanganya ashiki;husaidia kupunguza uzito kuleta nguvu na kuondoa uchovu.
Dong Quai:kikawaida mmea huu wa Asia hutumika kuripea seli ikiwemo ya mammorianna, (tezi za matiti).
Mother's Wort:Mmea uliopo sehemu nyingi za Ulaya na kandoni mwa mito ambazo hutoa msukumo fulani katika kano la uzazi.
Black Cohosh :Mmea unaopatikana kaskazini mwa Marekani hutumika kama dawa ya kubadilisha homoni.
Avena Sativa:Ni kama shayiri na ina kiasi kikubwa cha saponins, flavonoids, minerals, na alkaloids kwa ajili ya mfumo wa homoni.
Humulus Lupulus:Husaidia kuimarisha matiti.
kisasili cha matiti
1. Kujiamini kwa mwanamke kumejikita zaidi katika ukubwa wa matiti yake
2. Wanawake hawana muwashawasha sana na ukubwa wamatiti yao
3. Brazia za kimichezo si za lazima.
4. matiti makubwa yanauhusiano na mambo ya ngono
5. Wanawake na matiti madogo hushindwa kunyonyesha kwa ufanisi
6. Wanawake wote hufurahia kutomaswatomaswa kwa matiti yao
7. Wanawake kwa kawaida huwa na matiti mawili yenye ukubwa unaofanana
8. Nywele kuzunguka chuchu huonyesha kwamba mwanamke huyu si wa kawaida
9. Wanawake na matiti makubwa ni wazazi sana
10.Unyonyeshaji husababisha matiti kuwa malapa

Wednesday, August 26, 2009

umuhimu wa afya ya nywele



Kuna mambo mengi ya kufanya katika kuhakikisha kuwa nywele zako zinakuwa zenye afya.
Mtaalam kutoka Chicago healers Comina DK Melody Hart anasema kuwa, afya ya nywele inategemea sana mzunguko wa damu na lishe.
Pia inaweza kutokana na homoni na tezi, ni vyema kuangalia kwa mtindo fulani wa maisha yanavyokwenda wakati unaona hakuna kasoro katika nywele zako.
Shauri kubwa ni lishe. Ni vyema kuangalia chakula tunachokula kama tunahitaji afya ya nywele zetu.
Sehemu kubwa ya vyakula tunavyokula havina vitamini, madini, wala antioxidants kwa mfano kula vyakula organic husaidia sana afya ya nywele, anasema Dk. Julia Tatum Hunter.
Dk.Hart anashawishi kula vyakula vyenye silica na sulphur kama vitunguu, vitunguu swaumu, mboga za kijani na mayai.
Sulphur inajulikana kwa msaada wake kwa nywele, ngozi na kucha.
Watu wenye upungufu wa sulphur vyakula vyenye lodin na potassium kama mwani husaidia kukua kwa nywele na unene wake.
Unatakuwa kupunguza ulaji wa vitu vitamu kama pipi, soda, sukari, chumvi na kahawa katika mwili kama mtu anataka kustawisha nywele.
Badala ya kunywa soda na kahawa mtu anastahili kunywa maji kwa wingi. Mwili unatengenezwa na asilimia 60 mpaka 80 na maji.
Kama utanyimwa maji afya ya chembe hai zitakuwa katika mgogoro mkubwa.Ukosefu wa maji hukosesha ukuaji wenye afya wa mwili . Kimsingi unashauriwa kutumia glasi sita za maji kwa siku.

Tuanzie busati letu na urembo wa asili
















Hizi ni picha za mapambo mbalimbali yanayoamgusa mwanamke. Unaweza ukaona mwenyewe yanavyochukua nafasi mbalimbali katika maungo yako kutoka kichwani hadi mguuni na pasi shaka katika sebule. Kila mara tutafanya kitu fulani kukumbushana.

Karibuni katika busati la utanashati na urembo

Nimeamua kuanzisha gazeti tando hili kuchangia kwenye ulimwengu wa elimu kuhusu miili yetu utanashati na urembo mchango tunaukaribisha