Sunday, December 29, 2013

Usijinyime kula ili kupungua uzito

YAPO maswali mengi kuhusu tatizo la ukubwa wa matumbo yetu hasa kwa sisi  wanawake.
Wengi wamekuwa wakitumia njia mbalimbali ambazo nyingine si sahihi sana katika kufanya ili mradi kuwemo na amani akilimi na kwenye mwili.
Wengi wetu tunataka matumbo yawe wastani hasa yale ambayo hayajitokezi katika nguo zetu.
Ipo njia ya haraka ya kupunguza tumbo njia hiyo ni kubadili mfumo wa ulaji.
Unaweza kwa kuanza kula mbogamboga na matunda kwa wingi na kupunguza kula vyakula vya kukaanga na kufanya mazoezi ya kutembea.
Njia salama ya kupunguza tumbo ni ile ya kupangilia vyakula, usijinyime kula kwa kudhani kwa kufanya hivyo unaweza kupunguza tumbo njia hiyo inaweza kuleta madhara makubwa . Punguza kula vyakula vyenye wanga tumia mboga mboga na matunda kwa wingi pia punguza vyakula vyenye sukari nyingi.
Vyakula kama viazi mviringo, wali, mkate hukaa tumboni zaidi ya siku tatu, Unashauriwa kuacha kula nyama nyekundu ambayo husababisha kuongeza uzito na kuongezeka kwa ukubwa wa tumbo pia.
Unaweza kuwa unakula vizuri na unafanya mazoezi lakini ukawa na tatizo hili, kuna wakati tumbo linajitokeza kuliko kawaida. Mara nyingi hali hii husababishwa na kula vyakula vya wanga kwa wingi kama hunywi maji ya kutosha, kula bila mpangilio maalum au kula mara moja kwa siku.
Kula milo mitatu kwa siku .Kunywa maji mengi  angalau lita tatu kwa siku sababu kubwa ya mtu kuwa na tumbo kubwa ni chakula anachokula.
 


 
 
 

Thursday, December 26, 2013

'Urembo si sura nzuri tu ni pamoja na kujituma'


MSHINDI wa Pili wa taji la Miss Utalii Mkoa wa Dodoma mwaka 2011, Jackline Leshange amesema urembo  ni pamoja na kujituma.
“Urembo bado naupenda na sitaacha urembo, napenda hata mavazi ninayovaa yanitambulishe kuwa ni mrembo. Urembo si sura nzuri tu lazima ujue kujituma na kujiweka nadhifu”
Jackline amesema aliingia kwenye urembo mwaka 2010 kutokana na kupenda fani hiyo na alikuwa akifuatilia warembo mbalimbali kwenye Televisheni na hata kwenye majarida mbalimbali.
Mara ya kwanza kushiriki masuala a urembo ilikuwa ni Juni 2011, alipojitosa kwenye mashindano ya Miss Dodoma ambapo hakufanikiwa kuingia kumi bora.
“Sikukataa tamaa  Oktoba mwaka 2011 nilishiriki mashindano ya Miss Utalii Dodoma ambapo niliibuka mshindi wa pili”

Anasema  kwa sasa licha ya kujishughulisha na kazi ndogondogo za kujiingizia kipato pia jioni anakwenda darasani ili kujiendeleza zaidi kielimu.


Jackline akiwa katika pozi

Jackline Leshange

Jackline Leshange akiwa amepozi


Saturday, December 21, 2013

Jinsi ya kutengeneza uso ukiwa nyumbani

Kuna namna nyingi ya kutengeneza uso iwe nyumbani au saluni. Pia ni vizuri kama kutakuwa na kuelekezana jinsi ya kutengeneza uso ukiwa nyumbani.
Ni Muhimu ukafuata hatua zifuuatazo;
1.Chukua maziwa  ya mgando na utumie kusafisha uso wako.
2.Scrub kwa kutumia mchanganyiko wa mlozi na karoti au mlozi na jani la chai.
3.Fanya toning ya maji ya uvuguvugu yaliyochanganywa na kipande cha limao  na weka kidogo katika taulo la pamba na futa uso wako mahali pote kaoro kwenye tatizo.
4.Tumia ute mweupe wa yai ambao utakuwa umemwagika katika taulo lako na kujisugua tartibu.
5.Jisafishe na maji ya vuguvugu .
6.Fanya toning tena  kama livyokuwa kwa hatua za tatu juu.
7.Ili kuondoa ukavu za ngozi , kata matango na yabandike katika ngozi.
 
 

 
 
 
 

Maajabu ya asali katika kufanikisha urembo wako

Utashangaa sana kwamba asali ndiyo hasa kitu kitamu ambacho kwa miaka mingi watu wamekuwa wakikifananisha na raha.
Hii inatokana na ukweli kwamba asali inachukua nafasi ya pekee katika dunia ya mwanadamu.
Nafasi hii ya pekee imo katika mambo mengi mpaka mwenye tiba kwa kaaida asali dawa ya kukabiliana na vitu vingi pamoja na vimelea.
Pamoja na kuwa na antiseptic pia ina moisturizer na pia ina antioxidants na inasaidia kukabiliana na uzee.
Uwepo wa kiwango kikubwa cha sukari katika asali kunaipatia uwezo wa dawa na ndiyo maana kwa miaka maelfu imesaidia watu kutibu vidonda.
Mtaalam mmoja wa ngozi mwenye makazi yake mjini New York City ambaye pia ni daktari, Amy Wechsler anasema hali ya kunyunyurika iliyonayo asali na inayonasa inafanya kuwa kinga imara katika kidonda ambacho kinahitaji kisiingiliwe n vimelea na kutoa mazingira ya kuponya, hivyo asali ni bomba kwa tiba.

 Pamoja na tiba asali ni moisturize babu kubwa kwa ajili ya sura na mwili pia.
Asali ni dawa ya asili ambayo ina uwezo wa kukusanya maji  kutoka ndani ya misuli hadi katika sehemu za juu a ngozi na hivyo kusaidia kuondoa mikunjo.

Mimi nakushauri jaribu moisturizing ya asali ambayo itaondoa ukavu wa ngozi yako na hata kuwasha na kutatarika.

Changanya vijiko vya mezani viwili vya asali na vijiko viwili vya mezani vya maziiwa.

Kisha pasha moto mchanganyiko huo, kisha paka mchanganyiko huo katika uso wako na kupumzika kwa dakika kama kumi hivi.

Kisha jioshe kwa maji ya vuguvugu.Kama unataka kitu kama kosmetiki agiza lotion ya asali ili kuweka sawa ngozi yako.

Hkikisha unanunua lotion ambayo imetengenezwa kwa asali isiyochujwa.

Aina zote za asali zinasaidia kuondoa mikunjo ya uzeeni.

Thursday, December 19, 2013

Zijue faida za karoti kwenye urembo wako

KAROTI zimekuwa zikipatikana msimu mzima wa mwaka na zimekuwa zikiuzwa kwa bei ambayo kila mtu anaimudu. Ni chakula ambacho kina utajiri mkubwa wa vitamini na madini yenye faida nyingi mwilini. Kutokana na utajiri huo karoti sasa imekuwa ikitumika zaidi kwa ajili ya kutengeneza vipodozi vya aina mbalimbali pamoja na sabuni. Ulaji wa karoti au supu yake ni muhimu zaidi katika kutengeneza ngozi kuliko hata kutumia vipodozi kama ilivyo kwa mwili ambapo mwili unaolishwa vizuri ndiyo umekuwa na ngozi nzuri zaidi. Wataalam wa afya wanasema ni bora kula karoti kwa wingi kama unataka kuwa na ngozi yenye muonekano mzuri. Aidha Beta-carotene inayopatikana ndani ya karoti inapoingia mwilini ina uwezo wa kubadilishwa na kuwa vitamin A Aidha kirutubisho cha Fiber kilicho ndani ya karoti ni muhimu kutokana na kukinga kuta za utumbo. Unapotumia karoti mara kwa mara ina uwezo wa kufanya ngozi yako kuwa nzuri na yenye kuvutia. Pia karoti ina asilimia kubwa ya Vitamin C na vitamin D, aidha ina madini Folat, Zink, Madini ya chuma na Calcium Wataalam wa afya wanasema unapokula gramu 50 hadi 75 za karoti kila mara unakuwa umejiwekea kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali . Tafiti mbalimbali zilizofanywa zinaonesha karoti zimekuwa na nguvu kubwa ya kukinga watu juu ya kansa ya koo kutokana na vitamini na madini iliyomo ndani yake. juisi ya karoti