Thursday, June 27, 2013

Upi ukweli kuhusu vyakula na harufu ya ukeni?

YAPO maswali kama chakula au matunda tunayokula huleta husababisha harufu iwe ya kupendeza au mbaya katika uke wa mwanamke. Imeelezwa kuwa matunda na mbogamboga kama nanasi husababisha majimaji yanayotoka ukeni kuwa na harufu ya kati, lakini ulaji wa nyama, samaki na bidhaa za maziwa husababisha kuwapo na harufu nzito na hili pia lipo katika matumizi ya kitunguu swaumu,viungo vya chakula na kahawa. Unywaji wa kutosha wa maji husaidia kuondoa harufu inayokera lakini kama mambo hayaeleweki basi vitu vya manukato vinatakiwa kuwekwa karibu na uke ili harufu yake iwe ya kupendeza. Lakini haya mafuta au manukato mengine hakikisha hayagusani na uke unaweza kupata shida ambayo si ya lazima. Mtaalamu wa masuala ya miili Roshini Raj, M.D., akiwa na Lisa Lombardi amesema kwamba ni kawaida kwa wanawake kutoa harufu fulani kutoka katika uke. Wataalamu hao wamesema wanaume wengi walisema kwamba harufu hiyo huwapandisha hamu ya kufanya ngono. Lakini hata hivyo wataalamu hao wameonya kwamba kama mtu atasikia harufu nzito kama ya samaki na pengine harufu znito baada ya kumaliza kufanya ngono na licha ya kusafisha uke kwa sababu basi ipo hatari kwamba una vimelea vya ugonjwa kwa kitaalamu bacterial vaginosis au BV. Ni tatizo dogo linalotibika nenda kamuone mtaalamu wako wa masuala ya wanawake kwa ushauri zaidi. Hili ni tatizo la kukosekana kwa mizania kwa vimelea vinavyoishi katika uke