Monday, September 14, 2009

Jamani hebu hurumieni nguo zenu, zitunzeni


Watu hutumia mamilioni kama si maelfu ya fedha zao kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wanakuwa bomba na wenye kuvutia. Lakini ni kawaida mno kuona watu hao hao wakitupa fedha hizo kwa kuzivuruga nguo zao na kuziweka pasipo heshima kiasi ya kwamba huchakaa haraka au huharibika kwa muda mfupi sana.

Wengi wetu ambao tuna haki ya kujiita watanashati tuna matatizo makubwa sana ya utunzaji wa nguo zetu na wakati mwingine tunasahau kwamba nguo hizo ni raslimali zetu ambazo zikiharibika na sisi vile vile tunaharibika.

Mathalani mtu ananunua nguo kwa paundi 4000, fedha nyingi kabisa, lakini mtu huyu ambaye alitakiwa kuheshimu nguo zake unaweza kuingia chumbani mwake ukazikuta zimetupwa tu holela kitandanim, kwenye kochi na wakati mwingine hata bsakafuni.

Wewe mtu anavua suti na kuitupa, mtu anavua sidiria na kuitupa yaani mambo yote hata hayaeleweki.

Lakini nataka kusema hivi unapokuwa unabadilisha nguo kumbuka kuzihifadhi na kuzitunza kwani hiyo ni raslimali zako mwenyewe.

Kutokana na hali hiyo nataka kukueleza kuwa nguo ziku zote zinatakiwa kuwekwa kwa urefu wake ili zirejee katika hadhi yake ya kawaida.

Ni vyema kwelikweli na nasisitiza kuweka nguo zako kwa kuzitundika ili zirejee katika ule uzuri wake wa dukani na katika matenegnezo.

Ni vyema kama kabati lako halina nafasi ya kuweka vining'inizo ukaviweka kwani ni vya maana sana hsa vile vilivyotengenezwa kwa mbao.

Na wakati mwingine tumia vishikizo ambavyo vinasimamiwa pia na vitu vngine. Ninachotaka kusema hatakama ni sketi iweke katika nafasi yake inayostahili.Vivyo hivyo kwa jaketi na suruali na hata mashati.

Pamoja na kuweka nguo yaani kuzitundika ili kupata uhalisi wake ni vyema pia kuwa na mpango katika kabati lako si tu kujifanyia mambo kama mwendawazimu.Manake kama hukuwa na mpango itakuchukua siku nzima kujua ni wapi umeweka brazia au nguo yako ya ndani.

Ni lazima siku moja uamue kufanya ratibu ya kabati ili liwe na maana kubwa kwako na kukuwezesha kufanya maamuzi ya kasi wakati wa kuchagua nguo za kuvaa ziwe za ndani au nje.

Naomba usiruhusu kwa namna yoyote ile uwekaji wa mifuko ya nailoni kwani hutunza hewa ya unyevu na hii huleta uvundo katika nguo.

Pia kufanya mambo yako yawe bomba tafadhali fanya mambo mawili. Moja hakikisha kwamba nguo za zamani unazitoa ambazo zimemalizika muda wake wa fasheni.

Na maana kubwa sana ni kuwa upangaji husaidia pia kukuwezesha kufanya mambo ambayo pengine huyapati kwa uzuri kuwa na nafasi ya kuona.

Utunzaji wa nguo hauko tu katika kuziweka vyema bali hata wakati wa kufua,Angalia kwa makini maelezo ya nguo zako, maji yanayostahili kutumika joto na pia aina ya sabuni. Na ukishamaliza basi zinyooshe kama zinavyotakiwa.

katika masuala haya ni pamoja na viatu kuangaliwa, kusafishwa na pia kutunzwa kwa mujibu wa maelekezo ikiwemo ya utiaji wa kiwi.

No comments:

Post a Comment