Saturday, January 23, 2010

namna ya kujaza nywele kwa njia za asili


Kunamtu amenitumia swali juu ya nini afanye ili Nywele zake ndefu ambazo ni chache, zijae.
Nataka kumwambia kwamba hilo linawezekana kwa kufanya yafuatayo.
Chukua parachichi kubwa moja, asali vijiko vitatu na kiini cha yai.
Osha nywele zako kwa shampoo na uzikaushe.
Ponda ponda parachichi mpaka lilainike kabisa. Chukua vijiko vitatu vya asali na kiini cha yai kisha changanya yote kwa pamoja.
Paka mchanganyiko huo kaa nao kwa muda wa dakika 15 kisha osha.
Fanya hivyo kwa muda wa wiki moja hadi mbili na utaweza kuona matokeo mazuri katika nywele yako.

Jinsi ya kutengeneza uso ukiwa nyumbani


1. Chukua maziwa ya mgando na utumie kusafisha uso wako.
2. Scrub kwa kutumia mchanganyiko wa mlozi na karoti au mlozi wa jani la chai.
3. fanya toning na maji vuguvugu yaliyochanganywa na kipande cha limao na weak kidogo katika taulo la pamba na futa uso wako mahali pote kasoro penye tatizo.
4. Tumia ute mweupe ambao utakuwa umemwagia katika taulo lako na kujisugua taratibu.
5. Jisafishe na maji ya vuguvugu
6. Fanya toning tena kama ilivyokuwa katika hatua ya tatu juu
7. Ili kuondoa ukavu wa ngozi, kata matango na yabandike katika ngozi.

Jinsi asali inavyokabiliana na uzee


UTASHANGAA kwamba asali ndiyo hasa kitu kitamu ambacho kwa miaka mingi watu wamekuwa wakikifananisha na raha.
Ni kweli hata unapotaka kuleta longolongo za kimapenzi utasema asali wangu wa moyo au siyo?
Hii ni kutokana na ukweli kuwa asali inachukua nafasi ya pekee katika dunia ya mwanadamu.
Nafasi hii imo hata katika mambo mengi mpaka kwenye tiba, kwa kawaida asali ni dawa ya kukabiliana na vitu vingi pamoja na vimelea.
Pamoja na kuwa na antioxidants na inasaidia kukabiliana na uzee.
Uwepo wa kiwango kikubwa cha sukari katika asali kunaipatia uwezo wa dawa na ndiyo maana kwa miaka maelfu imesaidia watu kutibu vidonda.
Mtaalam mmoja wa ngozi mwenye makazi yake mjini New York City ambaye pia ni Daktari, Amy Wechsler anasema, hali ya kunyunyuruka iliyonayo asali na inayonasa inafanya kuwa kinga imara katika kidonda ambacho kinahitaji kisiingiwe na vimelea na kutoa mazingira ya kuponya, hivyo asali ni bomba kwa tiba.
Pamoja na tiba asali ni moisturize babu kubwa kwa ajili ya sura na mwili.
Asali ni dawa ya asili ambayo ina uwezo wa kukusanya naji kutoka ndani ya misuli hadi katika sehemu za juu za ngozi na hivyo kusaidia kuondoa mikunjo.
Mimi nakushauri jaribu moisturizing ambayo itaondoa ukavu wa ngozi yako na hata kuwasha au kutatarika.
Changanya vijiko vya mezani viwili vya asali na vijiko viwili vya mezani vya maziwa. Kisha pasha moto mchanganyiko huo, paka mchanganyiko huo katika uso wako na pumzika kwa dakika kama kumi.
Jioshe na maji ya uvuguvugu si ya moto.
Kama utataka kitu kama kosmetiki agiza Bee Ceuticals Organics’ Honey Thyme Hand and body lotion ambayo imetengenezwa kutokana na asali iliyochujwa .
Aina zote za asali zinasaidia sana kuondoa mikunjo ya uzeeni..

Wednesday, January 20, 2010

Vivazi vyenye mvuto


KUNA mavazi ya aina nyingi ambapo yakivaliwa humfanya mtu apendeze au achukize Uvaaji wa nguo unatakiwa kuzingatia umri na rangi ya mwili na pia mazingira ya nguo inapovaliwa.
Sio kila nguo ni ya kuvaliwa mchana na si kila nguo ni ya kutoka nayo barabarani aina nyingine ya nguo haistahili kuvaliwa barabarani.
Mathalani wewe ni mfanyakazi unajua unatakiwa uvaeje, kujiweka mrembo na mtanashati ni muhimu pia .
Uvaaji wa nguo zilizopangiliwa rangi zinazoenda sambamba na mkoba na viatu, utengenezaji mzuri wa nywele ni muhimu.
Kuvaa nguo zenye machanganyiko wa rangi mara nyingi huonekana kuwa na muonekano mbaya hata kama nguo hizo ni za gharama kubwa. endelea kupangilia rangi y nguo iende sambamba na kiatu na mkoba.
Vaa kulingana na mahali na wakati. Kuna nguo za kazini na za kutokea. Unaponunua na kuvaa nguo ya kitoto wakati wewe ni mzee unakuwa na maana gani?
Unaweza kuwa na miaka 50 na usafiri bomba je upo tayari kuvaa kimini kikali? Sina hakika lakini ni vazi hilo ni shauri lako na huenda ukawa ni samaki katika nchi kavu kwa kuangalia tamaduni zetu.
Kizazi cha sasa kinarekebisha sana masuala ya mavazi ndio maana nataka kusema kwamba shauri la staili si lile la una miaka 50 unataka kushindana na binti yako mwenye miaka 20.
Kwa umri wako wa miaka 50 unaweza kutafuta mavazi yenye mvuto kulingana na umri wako na ukatoka bomba vile vile.
Mavazi ni muhimu yakazingatia umri

Tuesday, January 19, 2010

Kwa nini unazeeka kabla ya wakati?


Mathalani hujafikia miaka ya 30 lakini unagundua uso wako ukiwa na mikunjo mingi usoni.Ikumbukwe kuwa, miaka ya 30 ni miaka katika ngozi yako pale machafuko ya hali ya hewa, viyoyozi, jua vinapoamua kuleta madhara kwenye ngozi yako.
Mbali na kuungua n jua, kuvuta sigara na kula vibaya makunyanzi huanza kutokea unapokaribia kuimaliza miaka ya 40.
Unaweza kuzuia hali hiyo kwa kutumia vitu vyenye mchanganyiko wa antioxidants ambavyo husaidia ngozi kuwa katika hali yake ya kawaida hasa kwa ngozi iliyoharibika kutokana na jua.
Dk.Dennis Gross, wa London Dermatologist anasema kuwa, kutumia vitu vyenye mchanganyiko wa antioxidants kama green tea, lycopene,co-enzyme Q 10, vitamin C na E vitaondoa makunyanzi yanayosababishwa na jua na yale yanayosababishwa na uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe.
Anasema unaweza kutumia cream utakazoshauriwa na daktari ambapo ngozi yako itaweza kurudi katika hali yake ya kawaida.
Wanasayansi wanasema kuwa, vatu wanaotaka kutunza ngozi zao kuacha kutumia sana sukari kwani sukari inachangia kuizeesha ngozi, sukari nyingi hufanya misuli ya protini katika ngozi kujikusanya pamoja na kusababisha kutoweka kwa mnyunyuruko unaotakiwa.
Tatizo la madoa na makovu usoni linaweza kuondolea kwa kutumia cream ambazo husaidia sana kuondoa bacteria na kukausha mafuta yaliyotanda usoni na kuacha ngozi yako ikiwa salama bila tatizo la madoa au chunusi.
Ili ngozi yako iwe nzuri unashauriwa kunywa maji mengi, maji ambayo husaidia kulainisha miili yetu.
Wakati mwingine makunyanzi husababishwa na tabia ya kula vyakula vilivyoungwa kwa chumvi nyingi.
Dk.Ibrahim Kaminsa wa Iringa anasema kuwa, kama una tabia ya kula vyakula vilivyoungwa kwa chumvi nyingi uso utakuwa na makunyanzi bila kujali umri wako.
Anasema mtu aliyeathirika na tatizo la makunyanzi anatakiwa kula mbogamboga na matunda kwa wingi na kunywa maji mengi ili kuondoa sumu ambayo imejengeka mwilini.