Monday, January 6, 2014

Njia tano bomba kwa afya yako




1.            Apple moja kwa siku - hukuweka mbali na daktari.
2.           Jani la mrihani (tulsi leaf) ukitumia kwa siku hukuweka mbali na saratani
3.           Limao kwa siku -hukuweka mbali na unene
4.           Kikombe cha maziwa kwa siku -hakuna tatizo la mifupa
5.           Lita tatu za maji kwa siku- hakuna magonjwa.

Apple
Mrihani(tulsi leaf)

Limao

Glasi ya maziwa

Tende na manufaa yake kiafya




WENGI wamekuwa wakila tende hasa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani huku wengine wakisema hawajawahi kula tende kwani hawajui faida yake mwilini.
Ukweli ni kuwa tende zimekuwa zikisaidia kuimarisha mfumo wa usagaji wa chakula na pia ni tiba ya wenye matatizo kwenye njia ya hewa. Pia husaidia hata wale wenye tatizo la kuongezeka uzito mara kwa mara
Pia tende zimekuwa na utajiri wa madini mwilini na pia zina vitamin A,B na C pia hazina cholesterol kama  aina nyingine ya vyakula vyenye mafuta ambavyo vimekuwa vikileta athari mwilini. Pia kuna wale wanaopenda kula tende zikiwa mbichi na hata wale wanaokula tende ambazo tayari zimeongeza vikorombwezo vingine.
Ni muhimu kula tende ili kuongeza madini na vitamimi mwilini ili kuweka mwili sawa na kuondokana na matatizo mbalimbali ya kiafya.

Tende ikiwa imeandaliwa kitaalam tayari kwa kuliwa

Tende ikiwa shambani


Sunday, January 5, 2014

Kitunguu kina kazi zaidi ya jikoni


KWA haraka haraka kuna namna 16 ambayo unaweza kusema ni faida ya kuwa na kitunguu ndani ya nyumba na hapa nazungumzia kitunguu maji.

Wakati wa mapishi wengi wetu hatukosi kutumia kitunguu kunogesha chakula lakini nje ya jiko pia kuna matumizi ambayo mwako wake hukufanya uwe mrembo zaidi na mwenye maarifa mengi.

Kuna hata kuking’arisha chuma na kuondoa barafu katika kioo chako cha gari .

1.Hufukuza wadudu.Ukisugua kitunguu katika ngozi yako au katika nguo zako ni namna nyingine ya kukabiliana na wadudu bila sumu

2.Kulainisha koo lenye shaka. Unatengeneza chai ya kitunguu na kunywa ili kuondoa mikwaruzo katika koo. Unachemsha maji kiasi cha kikombe kikiwa na nusu ya kitunguu (vipande) na kuinywa.

3.Kuondoa gamba. chukua kipande cha kitunguu kiweke kwenye gamba kisha funga na bandeji.Acha kama saa moja hivi. Ukiondoa itakuwa rahisi kuondoa gamba hilo kwani litakuwa limelegea.

4.Kung'arisha chuma. Ponda kitunguu na changanya na maji.Ukitumia kitambaa sugua eneo linalohusika mpaka uone limeng'aa.

5.Kupoozesha ulipong'atwa na mdudu au nyuki. Sugua eneo hilo lililoumwa na kitunguu na utasikia maumivu yanapungua.

6.Kusafishia cha chuma cha kuokea.kata kitunguu na kwa kutumia umma mrefu pachika kitunguu.Ondoa kwanza mabaki magumu ka kutumia brashi na kisha washa jiko. Tumia umma wako kupitisha kitunguu katika chuma cha kuokokea mpaka uchafu wote umeondoka.

7.Hufukuza mchwa.Kama kila mara mchwa wanafika katika jiko lako kata kiasi kingi cha kitunguu na kiache wazi. Harufu yake itawakimbiza.

8. Tengeneza  dai ya DIY . pamoja na rangi yake, unaweza kutengeneza dai ya nguvu yenye rangi ya njano au nyekundu.Chukua maganda ya vitunguu na tumbukiza katika mfuko wa maziwa na funga mwishoni.Chemsha kwa dakika kama 20 kimiminika kitakachobaki ni dai ambayo inafaa kwa ajili ya kutiwa katika karatasi,nyuzi au kitambaa

9.Humeza harufu ya wali ulioungua. Ukiwa  hupendi harufu ya kuungua kwa wali waweza kuweka nusu ya kitunguu karibu na jiko  harufu ile itamezwa na kitunguu.

10.Huzuia ukungu kwenye kioo cha gari. kata kitunguu nusu na kisugue kwenye kioo wakati wa usiku.Itazuuia ukungu kujitengeneza wakati wa usiku.

11.Kutia rangi mayai ya pasaka.Zungushia mayai na ngozi za vitunguu na kisha zihifadhi katika mataulo.Weka taulo hilo katika maji yanayochemka na chemsha mayai kama kawaida. Utayatoa yakiwa tayari na rangi ya manjano iliyokoza

12.Husaidia maparachichi kutokuwa  ya kahawia.Weka vipande vya vitunguu vyekundu na maparachichi katika kontena lisiloingiza hewa.

13. Humeza rangi mpya. kata vitunguu na viweke katika bakuri lenye maji na kisha weka bakuri hilo katika chumba kilichotiwa rangi kwa usiku mzima ili harufu ya rangi imezwe.

14.Safishia visu vilivyoingia kutu. Chukua kitunguu kikubwa kisha kichome na kisu chenye kutu!

15.Huzuia wanyama usiowataka.Paka na wa jamii yake huzuiwa na kitunguu kama utakikata kitunguu hicho vipande na kumwaga kuzunguka bustani yako.

16. Hupoozesha palipoungua.Sugua kitunguu juu ya eneo lililoungua kwa lengo la kupunguza maumivu na kwa kuwa kitunguu kina aina ya kemikali inayokabili bakteria utakifanya kidonda chako kisivamie na bakteria.



Kitunguu ambacho hakijakatwa
Kitunguu kilichokatwa


Friday, January 3, 2014

Utunzaji mgongo ni muhimu



MGONGO  ni moja ya kiungo cha mwili ambacho kinahitaji uangalizi mzuri.Bila hivyo huleta tabu hasa pale mgongo unapokuwa hauko katika muonekano mzuri.
Uchafu unaoganda kwenye mgongo hupelekea muwasho wa mara kwa mara na mgongo kuwa na mabaka mabaka .
Ukweli ni kuwa jaribu kuangalia mgongo wako na kuona kama unastahili kuwa hivyo na kama haustahili basi chukua hatua kwa kuhakikisha mgongo unakuwa msafi na kutafuta tiba ya chunusi au mabakamabaka yaliyo mgongoni mwako.
Unapoufanyia tiba mgongo kwa kutumia sabuni za dawa au lotion utaufanya uwe na muonekano mzuri na hata kuwa huru kuvaa nguo yoyote.
Wengi wanashindwa kuvaa nguo za wazi kutokana na muonekano wa ngozi zao za mgongoni kuwa mbaya zenye vipele, chunusi na kupauka.Madoa kwenye mgongo yamekuwa yakikosesha wengi raha kutokana na suala la utunzaji mgongo halitiliwi maanani kama ilivyo kwenye utunzaji wa uso au miguu.
Tumia brashi laini lenye sababu ya kutosha katika kusugua mgongo wako. Kisha paka mafuta.
Kama huwezi kufikia vizuri mgongo kwa kutumia blashi basi unaweza kuomba msaada ili mradi mgongo  utakate na kuwa katika sura ya kupendeza.
Wengi wanashindwa kuvaa nguo za wazi kutokana na migongo yao kuwa na sura isiyopendeze.
Ni muhimu ukazingatia usafi wa mgongo ili uwe huru kuvaa nguo za wazi bila kuwa na mashaka kuwa kuna watu wanautazama vibaya mgongo wako na wengine wameanza kucheka.