Tuesday, November 24, 2009

Umakini watakiwa katika chaguo la viatu


Unapoamua kuvaa aina ya viatu unakuwa na sababu za aina mbalimbali. Wengi hupendezewa na uvaaji wa viatu virefu na wengine hupendelea kuvaa viatu visivyo na kisigino flat shoes.
Wengi wetu hasa wakinadada wamekuwa wakipenda zaidi kuvaa viatu virefu licha ya kujua kuwa wakati mwingine viatu hivyo huleta madhara katika afya zao. Mara nyingi viatu virefu vimekuwa vikivaliwa na watu ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu kwa kutumia miguu na hivyo kuharibu afya za miguu yao.
Kwa upande mwingine flat shoes vimekuwa vikivaliwa sana na watu ambao wana uzito mkubwa na wale ambao hawapendi kuvaa viatu virefu.
Pia viatu hivi vimekuwa vikivaliwa kulingana na aina ya nguo uliyovaa kwani wakati mwingine nguo huendana na aina ya viatu kitu ambazo watu wengi huwa hawakizingatii mavazi mengine yanatakiwa kuvaliwa na flat shoes.
Na kitu kingine cha kuzingatia ili upendeze na aina hii ya viatu unatakiwa kuchagua vinavyoendana na rangi ya nguo uliyovaa.
Kuna aina nyingi ya viatu vya aina hii ambavyo vimekuwa vikiuzwa madukani lakini ni muhimu wakati unataka kununua kiatu cha aina hii unatakiwa kuzingatia malighafi ambayo imetengeneza kiatu.
Viatu vya ngozi huwa ni vizuri zaidi kwani huvaliwa muda mrefu bila kuharibika tofauti na viatu vya plastiki ambavyo hudumu kwa muda mfupi na kuchanika chanika.

No comments:

Post a Comment