Thursday, December 16, 2010

Wewe ni mwanamke unayejiamini kwa nini usipendeze?


MWANAMKE hulka yake ni Kupendeza. kupendeza kwa mwanamke humfanya
avutie na kuonekana wa kisasa zaidi.Wanawake wengi wamekuwa
wakijisahau na kupoteza ule uzuri wa muonekano wao.
Wakati mwingine kujipamba au kujiremba ni hulka ya mtu na kuna watu
wamezaliwa wakiwa warembo bila hata kujiremba huonekana kuvutia wakati
wote.
Lakini kuna wanawake ambao licha ya kuwa wazuri wakiongeza na
kujiremba huonekana wenye mvuto zaidi.
Wanawake ambao wana uzuri wa asili hasa wale ambao wametunza ngozi zao
nyeusi za asili hupendeza sana kama watajipamba kwa vitu vya asili
kama kuvaa hereni, mikufu au bangili zilizotengenezwa kwa vitu vya
asili kama vifuu vya nazi, magome ya miti au kutengenezwa kwa kutumia
shanga.
Wakati huu wanawake wenye uwezo kifedha wamekuwa wakitumia fedha zao
kujipamba kwa mapambo ya gharama kubwa kama kuvaa mikufu na saa zenye
za dhahabu na hata madini mengine yenye thamani kubwa kama almasi.
Uvaaji wa mikufu, hereni, bangili ni mambo ambayo mwanamke anatakiwa
kuyazingatia ili kuweza kuongeza urembo wake.
Wengi wetu tumekuwa tukisahau kutumia vitu hivi katika mavazi yetu.
Vitu hivi vimekuwa vikisaidia sana kuboresha maisha yetu ya urembo
kutokana na kuwa unapovaa hereni, mkufu au bangili iliyofanana na nguo
uliyovaa hii itasaidia uonekana nadhifu zaidi kuliko unavyofikiri.
Mwanamke ambaye amekuwa akipangilia mavazi yake amekuwa akionekana
nadhifu kuliko yule ambaye amekuwa akiweka mwilini kila aina ya rangi
na kufanya muonekano wake usiwe mzuri.
Kuna mapoambo mengi siku hizi tena kwa gharama nafuu sana cha
kuzingatia ni kucheza na rangi, ukijua namna ya kupangilia rangi za
mavazi yako na mapambo yako utakuwa umefanikiwa sana katika
kufanikisha muonekano wako uwe mzuri.
Kitu kingine cha kuzingatia ni kuwa, unapoamua kupangilia rangi za
mavazi yako hakikisha kuwa mvazi hayo hayawi kwenye rangi za kung’aa
sana hasa pindi mavazi hayo ni ya kuvaliwa wakati wa mchana.
Mwisho

No comments:

Post a Comment