Thursday, December 16, 2010

Uvaaji soksi na utunzaji wake


Soksi ni vazi ambalo huvaliwa miguuni.
Miguu ni mmoja kati ya viungo ambavyo vinatoa jasho mwilini, huzalisha
zaidi jasho kila siku.
Soksi husaidia kuhakikisha kuwa unyevunyevu unahifadhiwa katika eneo
linalotakiwa na baadaye kutolewa nje kwa njia ya hewa.
Katika mazingira ya baridi soksi husaidia kupunguza uhakika wa kupata baridi.
Soksi hutengenezwa kwa pamba, sufu, nailon na aina nyingine za nyuzi.
Katika kuongeza kiasi cha ulaini, malighafi nyingine ambazo
hutengenezaa soksi hutumika.
Kuna aina mbalimbali za rangi za soksi ambazo hutengenezwa na pia
kuvaliwa kila siku.
Wengine huvaa soksi ili kuimarisha muonekano wao
Soksi za rangi ya kung’aa mara nyingi huwa ni sehemu ya vazi katika
michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutofautisha wachezaji pale
ambapo miguu pekee ndiyo inaonekana.
Mitindo ya soksi huvaliwa kulingana na matakwa ya mvaaji.
Wengine hupenda kuvaa soksi na viatu vya wazi huku wengine wakivaa na
viatu vilivyozibwa.
Soksi ndefu nyeupe huvaliwa kama sehemu ya sare za shule.
Wanamichezo wamekuwa wakitumia soksi kama sehemu ya vazi. Soksi hizi
huwa ndefu na mara nyingi huwa ni nzito.
Makundi mbalimbali yamekuwa yakivaa soksi hata wanawake ambao huvaa
soksi katika kuhakikisha wanakuwa na muonekano mzuri na mavazi
waliyovaa.
Kuna zile soksi nyepesi sana hizi mara nyingi huvaliwa na wanawake.
Soksi ni vazi ambalo huvaliwa kila siku hasa kwa wanaume ni vizuri
kama soksi zinakuwa safi muda wote ili kuondoa ile harufu mbaya ambayo
imekuwa kero kwa watu wengi.
Ni vizuri kama soksi zikafuliwa na kuanikwa juani na kukauka vizuri
kabla ya kuvaliwa. Pia wavaaji wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakuwa na
jozi nyingi za soksi ili kuweza kupunguza ugumu wa kuzitunza.
mwisho

1 comment: