Wednesday, December 15, 2010

Unatakiwa kuwa makini zaidi katika kutunza uso wako


WATU wengi wamekuwa wakichukulia suala la utunzaji wa ngozi ya uso kwa
umakini zaidi. Ngozi zina mahitaji maalum ikiwemo kuweka ngozi katika
hali ya usafi na pia kuikinga ngozi na miale ya jua na mabadiliko
mengine ya hali ya hewa.
Ngozi ya uso inahitaji umakini zaidi kwani uso ni utambulisho wa
jinsi ulivyo na imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi kwa sababu
uso umekuwa ukizalisha mafuta mengi hasa kwenye paji la uso, macho,
pua, na kidevu.
Hitaji muhimu ni kuhakikisha kuwa, ngozi yako inakuwa katika hali
nzuri na safi kuanzia asubuhi unapoamka hadi usiku unapokwenda
kulala.
Unatakiwa kuchukua dakika tano hadi 10 katika suala hili.
Utunzaji wa uso asubuhi
Wakati wa asubuhi unatakiwa kusafisha uso wako kwa maji ya vuguvugu.
Epuka kutumia sabuni ya mche (ya kufulia) kwani haikutengenezwa
maalum kwa ajili ya uso na imekuwa ikifanya ngozi ya uso kuwa
iliyokakamaa
Unatakiwa kuhakikisha kuwa, uynaosha uso wako vizuri wakati unaoga au
wakati unanawa uso kwenye sinki,
Unaweza kutumia tona kusafisha uso wako kwani husaidia kuondoa uchafu
ulioganda usoni. Baadaye unaweza kutumia moisturiza .
Utunzaji wa uso jioni
Jioni unaweza kusafisha uso wako kwa kutumia maji ya vuguvugu. Baada
ya mizunguko ya hapa na pale ngozi inakuwa imechoka na inahitaji
umakini zaidi katika suala la usafi.
Pia unapotumia tona jaribu kutumi pamba laini ili kuweza kulinda uso wako.
Unapotunza ngozi lengo ni ngozi kuwa na unyevunyevu, unatakiwa
kuhakikisha haina magamba.
Lakini pia unaweza kutoa magamba au ngozi iliyokufa ambayo hufanya
ngozi isiyokubalika.
Wakati mwingine ngozi isiyokubalka husababuisha uso kuwa na chunusi.
Angalizo
Usiende kulala bila kuondoa make -up usoni. Make-up zimekuwa
zikisababisha kuzina kwa vitundu vya kutolea hewa na hivyo kusababisha
tatizo la kuwa na ngozi isiyokubalika.
Pia unatakiwa kuacha kutumia vipodozi vyenye kemikali kwani hufanya
watu wengine kupata kansa za ngozi.Wakati mwingine sehemu za uso
hupata uvimbe .
Hizi ni moja ya changamoto zinazoweza kukutokea katika ngozi yako la
muhimu ni kuhakikisha kuwa, usafi unazingatiwa sana pamoja na kunywa
maji mengi, mboga za majani na matunda kwa wingi.

2 comments:

  1. Swali nilikuwa natumia vipodozi visivyo na kemikali mwezi mmja uliyopita nikajaribu kutumia vipodozi vyenye kemikali yan sasa uso wangu umetoa chunusi nimeshaacha vipodozi hivyo ila nimebaki na madoa uson nifanyeje ili yaishe make naona yananinyima raha

    ReplyDelete
  2. Moisturiza na tona ndo nn hivyo?

    ReplyDelete