Monday, January 6, 2014

Tende na manufaa yake kiafya




WENGI wamekuwa wakila tende hasa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani huku wengine wakisema hawajawahi kula tende kwani hawajui faida yake mwilini.
Ukweli ni kuwa tende zimekuwa zikisaidia kuimarisha mfumo wa usagaji wa chakula na pia ni tiba ya wenye matatizo kwenye njia ya hewa. Pia husaidia hata wale wenye tatizo la kuongezeka uzito mara kwa mara
Pia tende zimekuwa na utajiri wa madini mwilini na pia zina vitamin A,B na C pia hazina cholesterol kama  aina nyingine ya vyakula vyenye mafuta ambavyo vimekuwa vikileta athari mwilini. Pia kuna wale wanaopenda kula tende zikiwa mbichi na hata wale wanaokula tende ambazo tayari zimeongeza vikorombwezo vingine.
Ni muhimu kula tende ili kuongeza madini na vitamimi mwilini ili kuweka mwili sawa na kuondokana na matatizo mbalimbali ya kiafya.

Tende ikiwa imeandaliwa kitaalam tayari kwa kuliwa

Tende ikiwa shambani


No comments:

Post a Comment