Saturday, December 21, 2013

Maajabu ya asali katika kufanikisha urembo wako

Utashangaa sana kwamba asali ndiyo hasa kitu kitamu ambacho kwa miaka mingi watu wamekuwa wakikifananisha na raha.
Hii inatokana na ukweli kwamba asali inachukua nafasi ya pekee katika dunia ya mwanadamu.
Nafasi hii ya pekee imo katika mambo mengi mpaka mwenye tiba kwa kaaida asali dawa ya kukabiliana na vitu vingi pamoja na vimelea.
Pamoja na kuwa na antiseptic pia ina moisturizer na pia ina antioxidants na inasaidia kukabiliana na uzee.
Uwepo wa kiwango kikubwa cha sukari katika asali kunaipatia uwezo wa dawa na ndiyo maana kwa miaka maelfu imesaidia watu kutibu vidonda.
Mtaalam mmoja wa ngozi mwenye makazi yake mjini New York City ambaye pia ni daktari, Amy Wechsler anasema hali ya kunyunyurika iliyonayo asali na inayonasa inafanya kuwa kinga imara katika kidonda ambacho kinahitaji kisiingiliwe n vimelea na kutoa mazingira ya kuponya, hivyo asali ni bomba kwa tiba.

 Pamoja na tiba asali ni moisturize babu kubwa kwa ajili ya sura na mwili pia.
Asali ni dawa ya asili ambayo ina uwezo wa kukusanya maji  kutoka ndani ya misuli hadi katika sehemu za juu a ngozi na hivyo kusaidia kuondoa mikunjo.

Mimi nakushauri jaribu moisturizing ya asali ambayo itaondoa ukavu wa ngozi yako na hata kuwasha na kutatarika.

Changanya vijiko vya mezani viwili vya asali na vijiko viwili vya mezani vya maziiwa.

Kisha pasha moto mchanganyiko huo, kisha paka mchanganyiko huo katika uso wako na kupumzika kwa dakika kama kumi hivi.

Kisha jioshe kwa maji ya vuguvugu.Kama unataka kitu kama kosmetiki agiza lotion ya asali ili kuweka sawa ngozi yako.

Hkikisha unanunua lotion ambayo imetengenezwa kwa asali isiyochujwa.

Aina zote za asali zinasaidia kuondoa mikunjo ya uzeeni.

3 comments:

  1. Asante, nnatatzo la mabaka mgongoni naomba unisaidie juu ya hili!

    ReplyDelete
  2. Msaada tutani. yap nimeipat hiyo. nina brown sport usoni sijui nitazimaliza vipi. zinatokana na makeup na wala sijui ni makeup gani.

    ReplyDelete