Saturday, July 19, 2014

Tumia asali kufanikisha urembo wako

Nauza asali mbichi ambayo haijachanganywa na chochote ni nzuri kwa ngozi na afya yako. Bei ni Sh. 10,000 kwa kilo moja na Sh. 5,000 kwa nusu kilo.
Mawasiliano 0719818644/0762650760










Mtaalam mmoja wa ngozi mwenye makazi yake mjini New York City ambaye pia ni daktari, Amy Wechsler anasema hali ya kunyunyurika iliyonayo asali na inayonasa inafanya kuwa kinga imara katika kidonda ambacho kinahitaji kisiingiliwe n vimelea na kutoa mazingira ya kuponya, hivyo asali ni bomba kwa tiba.

 Pamoja na tiba asali ni moisturize babu kubwa kwa ajili ya sura na mwili pia.
Asali ni dawa ya asili ambayo ina uwezo wa kukusanya maji  kutoka ndani ya misuli hadi katika sehemu za juu a ngozi na hivyo kusaidia kuondoa mikunjo.

Mimi nakushauri jaribu moisturizing ya asali ambayo itaondoa ukavu wa ngozi yako na hata kuwasha na kutatarika.

Changanya vijiko vya mezani viwili vya asali na vijiko viwili vya mezani vya maziwa.
Kisha pasha moto mchanganyiko huo, kisha paka mchanganyiko huo katika uso wako na kupumzika kwa dakika kama kumi hivi.
Kisha jioshe kwa maji ya vuguvugu.Kama unataka kitu kama kosmetiki agiza lotion ya asali ili kuweka sawa ngozi yako.
Hakikisha unanunua lotion ambayo imetengenezwa kwa asali isiyochujwa.
Aina zote za asali zinasaidia kuondoa mikunjo ya uzeeni.

No comments:

Post a Comment