Hakuna raha kama kuwa na midomo (lips) zenye kuvutia tena ikiwa katika namna ambayo kila moja anaitamani kuiangalia na hata kuibusu.
Lips nzuri zina nafasi yake katika maisha ya
mwanamke kwani anakuwa mwenye kujiamini tofauti na mtu ambaye anakuwa na midomo
mikabu ambayo imekuwa ikipasuka mara kwa mara.
Kuna njia nyingi za kutunza Lips ikiwemo zile za
kiasili na hata za kisasa lakini yote hayo hutegemea na matakwa na hata uwezo wa
mhusika.
Kumekuwa na hali mbalimbali ambazo hupelekea
midomo kuwa mikavu, kukatika na hata kuchubuka na kuwa na ngozi nyekundu.
Kinachoonekana zaidi ni kuwa watu
wengi hawatilii sana maanani juu ya utunzaji wa midomo licha ya kuwa kuna
wakati midomo inakauka au kupasuka pasuka hasa wakati wa baridi.
Midomo imekuwa ikitunzwa kwa njia za
asili ikiwemo kupaka Glycerin hali inayochangia kulainisha ngozi za mdomo na
kujiepusha na mipasuko.
Njia hii ya kupaka mafuta hutumiwa
wakati wote hata pale mtu anapotaka kwenda kulala.
Pia mafuta haya husaidia kuondoa
weusi uliopo kwenye midomo.
Pamoja na hayo pia kuna mafuta
maalum ambayo hutumiwa kwa ajili ya kupaka mdomoni kwa lengo la kulainisha
midomo ambayo pia kwa kiasi kikubwa inachangia wengi kuwa na midomo inayovutia
hasa kwa wale wanaotumia.
Aidha kuna njia ya kutumia majani ya
hiliki ambapo hutumika kwa kusugua
kwenye midomo na kupelekea midomo kuwa laoini.
Jambo lingine linalosisitizwa katika
utunzaji midomo ni pamoja na kutumia maji ya limao yaliyochanganywa na asali
kwa kupakwa kwenye midomo na kukaa na mchanganyiko huo kwa muda wa saa moja
hiyo husaidia pia kuondoa hata weuzi uliopo kwenye midomo.
Pia Unywaji wa maji mengi husaidia
katika kuimarisha midomo na hata matumizi ya mlozi (almond oil) kama yakipakwa
mdomoni kabla ya kwenda kulala husaidia sana kuiweka midomo katika namna
inayopendeza.
No comments:
Post a Comment