Kioo huchangia kuimarisha
Kitu kimoja kizuri kinachorekebisha sana desturi na kitu unachotaka ni kioo. Wanawake wengi wanakwepa kujiangalia katika kioo wanaona kioo kinawapa kitu cha siri wasichotaka kujua. Kioo kinaweza kuwa rafiki yako mkubwa na kioo kinaweza kukuambia unaendeleaje kioo kinakupa kitu ambacho macho hivi hivi hayawezi kuona.
Fanya
kila kitu vizuri
Namna unavyotumia vikolozo vyako vya uzuri kwa namna
inayostahili ndivyo utakavyopata matokeo unayoyataka.Mathalani fanya kama wanavyofanya watu wa saluni unapoenda kutengeneza nywele utaona kwamba shampoo haimwagwi kichwani bali inatiwa katika mikono na kupelekwa kichwani mwako kama kusikasuka.
Fanya masaji ya nywele wakati unatengeneza nywele halafu osha vyema na nyanyua nywele zako mpaka zinakubaliana na wewe.
Onekana
Bomba
Usijali kuonekana mzuri jail kuonekana bomba,
onyesha dunia kwamba unajijali sana kwa uzuri ulionao, badala ya kuondoka mbio
kusaka uzuri wa dukani,wewe jikite katika kujitambua.
Tumia kile ulichonacho kwa namna nzuri zaidi na kuking’arisha kwe bomba au la utanyong’onyea na kuleta sura
isiyopendeza.
Mradi
wa ulimbwendeJisikie bomba, jisikie maridadi , ukijisikia mbaya ujue ndivyo dunia itakavyokuona na ukijisikia bomba ndiyo dunia itakuona bomba.
Marafiki wanaofaa
Wanachosema watu kama kwa makusudi au la ni dhahiri hukusaidia kujisikia vyema au vibaya, tafuta marafiki wanaokufanya ujisikie vizuri si wale wanaokufanya utake kujua.
Jisikilize
Jisikilize mwenyewe kwani hicho ndiyo hasa
kitakachokufanya ujisikie vyea na kuendelea na mambo yako vyema. Kujisikia
kunasuuza sana akili, tafuta muda wa kujisikiliza mwenyewe hiki ni kipindi cha
kuona mambo yalivyo.
Jipumzishe
Angalau mara mbili pumzika kwa dakika tano kuangalia make up yako, nywele pozi na nguo
hata kama umeamkaje ni vyema kujitazama kuona kama uko bomba kama ulivyotoka
nyumbani.
No comments:
Post a Comment