Friday, December 21, 2012

Namna rahisi na salama ya kupunguza tumbo

Wengi wa wasomaji wamemtumia meseji za kutaka kujua njia ya kupunguza mafuta tumboni, wanawake kwa wanaume walituma maswali kwa wingi. Njia iliyosalama ya kupunguza mafuta katika tumbo au kupunguza tumbo kubwa ni ile ya kupangilia chakula na kufanya mazoezi.
Nilipata nafasi wiki hii ya kuzungumza na daktari mmoja katika hospitali ya mkoa wa Iringa ambaye sitamtaja kwa jina na alikuwa na mengi ya kuelezea jinsi hali hiyo inavyoanza na husababishwa ni nani. Alisema kuwa,kama unataka kupunguza tumbo kwa haraka basi punguza kula vyakula vyenye wanga na badala yake tumia mbogamboga na matunda kwa wingi. Vyakula kama viazi mviringo, wali mkate hukaa tumboni kwa zaidi ya siku tatu, pia ulaji wa nyama nyekundu inasababisha kuongezeka uzito na pia huongeza ukubwa wa tumbo,vyakulahivyo vinatakiwa kutumiwa kwa kiasi kidogo sana. "Kuna wakati tumbo linajitokeza na kuwa kubwa kuliko kawaida hali hiyo inasababishwa na kula vyakula vya wanga kwa wingi, kutokunywa maji ya kutosha na pia kula bila ya mpangilio maalum" anasema. Anasema kuwa kama ntu anataka kupunguza mafuta au kuondoa kitambi anatakuwa kula milo mitatu kwa siku na si kujinyima kula kwa kudhani kuwa unaweza kupungua uzito. "Vyakula vya wanga na mafuta ufanya mtu kunenepa, acha au kupunza kula vyakula vyenye wanga ili kupunguza mafuta yaliyozidi mwilini, mafuta yanaporundikana mwilini athari moja kubwa ni kuwa na tumbo kubwa." anasema. Anasema kuwa,tumbo kuwa kubwa ni dhahiri kuwa chakula unachokula hakifanyi kazi inayotakiwa, kumekuwa na ziada mwilini na hii ziada inafanyika mafuta ambayo hujiwekesha akiba katika maeneo mbalimbali ya mwili. "Kwa kuwa Chakula hiki cha ziada huwa hakitakiwi, mwili hukibadilisha na kuweka akiba katika mfumo wa mafuta kitaalamu kama glycogem.Unaweza kukabiliana na kuzidi kwa protini zinazoyeyushwa na kuwekwa katika akiba kwa mfumo huo wa mafuta" Daktari huyo anasema kuwa, mtu mwenye tatizo hilo ni bora akapangilia mlo wake kwa siku.
"Asubuhi pata kifungua kinywa kilichokamilika, pata mlo wa mchana kama kawaida na usiku kula matunda tu kunaweza kufanya mwili wako uwe katika hali inayotakiwa. "Watu wengi wanatumia wanga mwingi wakati wa usiku muda ambao unaenda kulala na ziada ya chakula haifanyi kazi vizuri zaidi ya kujikusanya, kujibadilisha na kuhifadhiwa katika maeneo mbalimbali ya mwili hasa tumboni" anasema Daktari. Je Mazoezi husaidia kupunguza uzito wa mwili na manyama uzembe? Mazoezi ya viungo yamethibitishwa kusaidia kuchoma mafuta ya ziada katika mwili. Kutokana na hali ya ulaji unaweza kutengeneza manyama uzembe katika kifua, mapaja na maeneo fulani ya tumbo ambayo yametengenezwa kupokea maeneo ya ziada yanayotokana na mafuta yenyewe au sukari iliyobadilishwa kuwa mafuta. Nishati inayotokana na nafaka ambayop haiwezi kutumika muda huo hutengenezwa kuwa mafuta na kupelekwa eneo husika. Wanaume huwa na asilimia 8 hadi 20 ya mafuta katika mwili na ni kawaida wakati kwa wanawake ni asilinia 13 hadi 25.
Unapofanya mazoezi ya viungo unaongeza hewa ya oksijeni kwa wingi katika mapafu yako na wakati huohuo mwili nao unaunguza mafuta ili kutoa nguvu kwa mwili. Mafuta yanayounguzwa kwanza ni yale ya kawaida kabla ya kuingia katika akiba. Kuna umuhimu wa kutambua kuwa mazoezi ni kitu cha bure na kama ukifanya kwa mpangilio na vizuri hutakuwa na shida ya kutengeneza shepu yako. Dk.Martica Heaner,M.A, M.Ed. ambaye hutoa mawaidha ya keep fit ndani ya MSN anasema ni jambo la heri kama mtu atakula kidogo kabla ya kuanza mazoezi ili kutoa nishati ya kutosha ya kufanyisha mazoezi. "Lakini kama unaenda mwendo fulani mdogo tu au unatembea kwa dakika 30 huenda usiwe na haja kabisa ya kula hata hicho kidogo na hasa ikiwa uliweka kitu kiogo saa tatu zilizopita" anasema.

9 comments:

  1. Ahsante sana ntajitahidi sana hadi mwili wangu upungue
    pia kwa mtu mwenye umri wa miaka 21 anatakiwa kuwa na wastani wa kilo ngapi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndg. Pima uzito wako wa sasa gawa kwa urefu ulionao ndo utajua unapaswa kuwa na uzito upi. Hsin umri hiyo.

      Delete
    2. Asante kwa kunisaidia kujibu hilo

      Delete
    3. Jamani mimi ni mmama mwenye umri wa miaka 52 nina uzito mkubwa sana nina tumbo,mapaja makubwa,pia ni mfupi mnene sana ninahitaji msaada wako nianze na mazoezi gani?. Pia nina matatizo ya miguu baada ya kwenda hospitali nalipiga x-ray ikaonekana vifupa yangu kwenye magozi inasagana. Dactari alinishauri nipunguze uzito sasa mazoezi siwezi shauri naumwa na miguu je nitumie vyakula gani ili niweze kupunguza uzito huu.

      Delete
    4. Hivi ukinywa ukwaju inasaidia kupunguza tumbo???...

      Delete
    5. Pole sana.fanya diet ya kabeji utapunguza uzito fasta

      Delete
  2. Mama ukienda kwenye kumbi za mazoezi watakupa ain ya mazoezi itakayomaliza kabisa tatizo lako.

    ReplyDelete
  3. Kote tutazunguka kikubwa Fanya mazoezi hasa ya kukimbia asubuhi jioni,ruka kamba au jirusherushe mara60 kwa siku asubuhi30,jioni 30,lala chali kisha inua miguu juu Fanya kama unanyonga baiskeli mara30 utasikia maumivu ktk tumbo la chini,kaa kisha panua miguu kisha geuza kifua kigeuke kama unatazama nyuma unaenda na kurudi mara20 kila upande husaidia kunyoosha tumbo,kunywa maji ya vuguvugu glasi4 kila alfajiri na jioni b4 menu husaidia kuyeyusha mafuta pia punguza vyakula vya mafuta na sukari nyingi na kulakula hovyo bila ratiba hufanya tumbo kubeba zigo kubwa nakujaza mifati kibao...ukiona haya magumu basi andaa Fundi wa kukushonea nguo zako special

    ReplyDelete
  4. mimi ni mwanafunzi na shule tunakula vyakula vya wanga kwa wingi unaweza kunishauri nianyaje ilinipunguze tumbo

    ReplyDelete