Monday, September 14, 2009

uondoaji chunusi kwa njia za kiasili


Ukitaka kuondoa chunusi usoni na kusafisha uso usiwena madoa kwa kiasili, njia zifuatazo zaweza sana kusaidia.
Tafuta ukwaju loweka katika maji ukishalainikachanganya na asali, paka usoni.
Ni dawa nzuri sana na utaona ngozi yako inabadilikakwa kipindi kifupi.
Kama utashindwa kupata vitu hivyo tafuta sabuni pamojana krimu yenye mchanganyiko wa asali na ukwaju.
Sabuni hiyo iko katika boksi kubwa na kwa ndani inakigunia ambacho kinasaidia kusaficha uso, usinunue sabuni ya ukwaju na asali ambayo haijafungwa kwenye kitambaa kigumu chenye rangi ya kahawia itakuwa ni feki na haitakusaidia.
Kama unataka kupunguza tumbo au mwili kwa ujumla.Asubuhi kunywa chai nzito, mchana kula chakula kilichokamilika.
Ila usiku kula matunda tu ili uweze kuupa mwili nafasi ya kujitengeneza na hasa kupunguza mfuta yaliyozidi mwilini.
Uwe unakula wakati unasikia njaa tu unapokula bila yakusikia njaa unakuwa unarundika tu chakula mwilini na baadaye chakula hicho hubadilika na kuwa mafuta ambayo
hutengeneza manyama uzembe.
Ukishindwa hivyo nenda kwa daktari iliakupe masharti ya vyakula na uweze kupunguza mwili

3 comments:

  1. oooowwwwhhhh i love this,,,thank you

    ReplyDelete
  2. Ahsante sana mtaalamu kwa kutusaidia wenye matatizo ya chunusi. Lakini na mimi nilikuwa nataka kuijuia vizuri hiyo sabuni ya ukwaju maana nilikuwa nakuomba kama unayo utuonyeshe kwa njia ya picha ili na sisi tusije kupata feki.

    Ahsante

    ReplyDelete
  3. naomba kujua kipimo cha mchanganyiko wa asali na ukwaju.

    ReplyDelete