KUNA Msomaji ametuma swali akisema kuwa, yeye ni mwaume
mwenye umri wa miaka 30 na amekuwa akifanya shughuli zake chini ya mti ambapo
licha ya kuwa na jua kali wakati mwingine kunakuwa na upepo mkali, hali hiyo imesababisha
ngozi yake kuungua na jua na ngozi yake kukakamaa imekuwa na makunyanzi kiasi
cha kumtisha.
Kulingana na tafiti mbalimbali za kiafya, watalaam
wanasema kuungua na jua usoni kunalazimisha ngozi kuongeza uzalishaji wa
melanin hali ambayo husababisha mtu kuwa na ngozi nyeusi na kuwa kama kahawia
(brown).
Pia unaweza kupata ngozi nyeusi au kahawia kama
miale ya jua inakuwa inakupiga moja kwa moja usoni kwa asilimia 60 hadi 80.
Vitamin E inaonesha kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia
mtu asipigwe na miale ya jua usoni, vitamin
E hupatikana katika vyakula kama mafuta
ya soya, karanga, nafaka, mboga za majani, kini cha yai na nafaka ambazo
hazijakobolewa.
Vitamini E husaidia kukua kwa nywele mara mbili ya
kiwango cha ukuaji wa kawaida, pia matumizi ya lotion za kuzuia kuungua na jua
zinasaidia sana ili kujikinga na miale ya jua.
Aidha kuungua na jua huwapata watu ambao mara nyingi hufanya kazi zao wakiwa
juani aina nyingine ya ngozi ni rahisi sana kuathiriwa na jua na
zinahitaji ulinzi zaidi.
Pia ni vizuri kama kila moja atachukua tahadhari
mapema ili kujilinda na kulinda ngozi yake isipate tatizo hili.
Watu ambao ngozi zao zimeathirika na jua wanatakiwa
kuepuka kushinda juani na wanatkiwa kunywa maji mengi na kula mboga za majani
na matunda kwa wingi ili kuweza kurekebisha tatizo lililopo.
Kwa wale wenye makunyanzi kabla ya umri wanashauriwa
kula vyakula vyenye chumvi au sukari kiasi kwani matumizi makubwa ya sukari na
chumvi ni chanzo cha kuwa na makunyanzi.
Ikumbukwe kuwa kuna vuitu vingi ambavyo miili yetu
inahitaji ili kuwa na ngozi nzuri kana usingizi wa kutosha, kupumzika, kufanya
mazoezi na kula vizuri.
No comments:
Post a Comment