Muhimu kutambua mavazi ni njia kubwa na
nzuri ya kutambulisha tabia ya Mtu. Wengi wanapendwa au wanachukiwa kutokana na
mavazi wanayovaa. Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakivaa mavazi yasiyo na heshima
ama kwa kuwa mafupi au yamekuwa yakiacha sehemu kubwa ya kifua kuwa wazi.
Wasichana wa sasa wanaona kuvaa nguo zinazoacha wazi sehemu kubwa ya matiti kama fasheni.
Kuna mavazi
ya aina nyingi ambapo yakivaliwa humfanya mtu apendeze au achukize. Uvaaji wa
nguo unatakiwa kuzingatia umri na rangi ya mwili na pia mazingira ya nguo
inapovaliwa.
Sio kila
nguo ni ya kuvaliwa mchana na sio kila nguo ni ya kutoka nayo barabarani aina
nyingine za nguo hazistahili kuvaliwa barabarani unapotoka tu barabarani unaanza kupigiwa miluzi hiyo si sawa sawa.
Mathalani wewe
ni mfanyakazi unajua unatakiwa uvaaje, kujiweka mrembo na mtanashati ni kitu
muhimu. Siku hizi kuna mitimbo mbalimbali ya nguo za madukani, kushona mitindo
ya kutumia vitenge, vitambaa kwa mitindo ambayo inatunza heshima ya mvaaji.
Unatakiwa
kuvaa kulingana na mahali na wakati kwani kuna nguo za kazini na za kutokea
lakini sasa hivi si ajabu ukakutana na mtu mchana wa jua kali akiwa amevaa nguo
ya usiku au kumkuta akiwa amevaa viatu virefu huku akijua fika anatembea kwa
miguu kwa umbali mrefu.
No comments:
Post a Comment