Sunday, May 25, 2014

Athari za ngozi iliyoungua na jua




KUNA Msomaji ametuma swali akisema kuwa, yeye ni mwaume mwenye umri wa miaka 30 na amekuwa akifanya shughuli zake chini ya mti ambapo licha ya kuwa na jua kali wakati mwingine kunakuwa na upepo mkali, hali hiyo imesababisha ngozi yake kuungua na jua na ngozi yake kukakamaa imekuwa na makunyanzi kiasi cha kumtisha.
Kulingana na tafiti mbalimbali za kiafya, watalaam wanasema kuungua na jua usoni kunalazimisha ngozi kuongeza uzalishaji wa melanin hali ambayo husababisha mtu kuwa na ngozi nyeusi na kuwa kama kahawia (brown).
Pia unaweza kupata ngozi nyeusi au kahawia kama miale ya jua inakuwa inakupiga moja kwa moja usoni kwa asilimia 60 hadi 80.
Vitamin E inaonesha kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia mtu asipigwe na  miale ya jua usoni, vitamin E hupatikana  katika vyakula kama mafuta ya soya, karanga, nafaka, mboga za majani, kini cha yai na nafaka ambazo hazijakobolewa.
Vitamini E husaidia kukua kwa nywele mara mbili ya kiwango cha ukuaji wa kawaida, pia matumizi ya lotion za kuzuia kuungua na jua zinasaidia sana ili kujikinga na miale ya jua.
Aidha kuungua na jua huwapata  watu ambao mara nyingi hufanya kazi zao wakiwa juani  aina nyingine ya ngozi  ni rahisi sana kuathiriwa na jua na zinahitaji ulinzi zaidi.
Pia ni vizuri kama kila moja atachukua tahadhari mapema ili kujilinda na kulinda ngozi yake isipate tatizo hili.
Watu ambao ngozi zao zimeathirika na jua wanatakiwa kuepuka kushinda juani na wanatkiwa kunywa maji mengi na kula mboga za majani na matunda kwa wingi ili kuweza kurekebisha tatizo lililopo.
Kwa wale wenye makunyanzi kabla ya umri wanashauriwa kula vyakula vyenye chumvi au sukari kiasi kwani matumizi makubwa ya sukari na chumvi ni chanzo cha kuwa na makunyanzi.
Ikumbukwe kuwa kuna vuitu vingi ambavyo miili yetu inahitaji ili kuwa na ngozi nzuri kana usingizi wa kutosha, kupumzika, kufanya mazoezi na kula vizuri.





Saturday, May 24, 2014

Mavazi hutambulisha tabia ya mtu




Muhimu kutambua mavazi ni njia kubwa na nzuri ya kutambulisha tabia ya Mtu. Wengi wanapendwa au wanachukiwa kutokana na mavazi wanayovaa. Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakivaa mavazi yasiyo na heshima ama kwa kuwa mafupi au yamekuwa yakiacha sehemu kubwa ya kifua kuwa wazi.
Wasichana wa sasa wanaona kuvaa nguo zinazoacha wazi sehemu kubwa ya matiti kama fasheni.
Kuna mavazi ya aina nyingi ambapo yakivaliwa humfanya mtu apendeze au achukize. Uvaaji wa nguo unatakiwa kuzingatia umri na rangi ya mwili na pia mazingira ya nguo inapovaliwa.
Sio kila nguo ni ya kuvaliwa mchana na sio kila nguo ni ya kutoka nayo barabarani aina nyingine za nguo hazistahili kuvaliwa barabarani unapotoka tu barabarani unaanza kupigiwa miluzi hiyo si sawa sawa.
Mathalani wewe ni mfanyakazi unajua unatakiwa uvaaje, kujiweka mrembo na mtanashati ni kitu muhimu. Siku hizi kuna mitimbo mbalimbali ya nguo za madukani, kushona mitindo ya kutumia vitenge, vitambaa kwa mitindo ambayo inatunza heshima ya mvaaji.
Unatakiwa kuvaa kulingana na mahali na wakati kwani kuna nguo za kazini na za kutokea lakini sasa hivi si ajabu ukakutana na mtu mchana wa jua kali akiwa amevaa nguo ya usiku au kumkuta akiwa amevaa viatu virefu huku akijua fika anatembea kwa miguu kwa umbali mrefu.




Thursday, May 22, 2014

Siri ya kuuza uzuri wako kwa wenzako

KUNA watu wanataka kuvisha macho yao lakini hawana uwezo, wapo wanaotaka midomo yao kuwa minene zaidi na hana uwezo .Kwani kuna watu wanaangalia televisheni na kusema ngoja niwe kama yule au anasoma katika picha na kusema nataka kuwa hivi. Wacha mambo hayo usijilinganishe na mtu yoyote  yule, jitambue  na hakikisha kwa kujitambua kwako unajitengenezea kuwa mrembo zaidi
Kioo huchangia kuimarisha

Kitu kimoja kizuri kinachorekebisha sana desturi na kitu unachotaka ni kioo. Wanawake wengi wanakwepa kujiangalia katika kioo wanaona kioo kinawapa kitu cha siri wasichotaka kujua. Kioo kinaweza kuwa rafiki yako  mkubwa  na  kioo  kinaweza kukuambia  unaendeleaje  kioo   kinakupa  kitu ambacho macho hivi hivi hayawezi kuona.

Fanya kila kitu vizuri
Namna unavyotumia vikolozo vyako vya uzuri kwa namna inayostahili ndivyo utakavyopata matokeo unayoyataka.
Mathalani fanya kama wanavyofanya watu wa saluni unapoenda kutengeneza nywele utaona kwamba shampoo haimwagwi kichwani bali inatiwa katika mikono na kupelekwa kichwani mwako kama kusikasuka.
Fanya masaji ya nywele wakati unatengeneza nywele halafu osha vyema na nyanyua nywele zako mpaka zinakubaliana na wewe.

Onekana Bomba
Usijali kuonekana mzuri jail kuonekana bomba, onyesha dunia kwamba unajijali sana kwa uzuri ulionao, badala ya kuondoka mbio kusaka uzuri wa dukani,wewe jikite katika kujitambua.

Tumia kile ulichonacho kwa namna nzuri zaidi na kuking’arisha  kwe bomba au la utanyong’onyea na kuleta sura isiyopendeza.
Mradi wa ulimbwende
Jisikie bomba, jisikie maridadi , ukijisikia mbaya ujue ndivyo dunia itakavyokuona na ukijisikia bomba ndiyo dunia itakuona bomba.
Marafiki wanaofaa
Wanachosema watu kama kwa makusudi au la ni dhahiri hukusaidia kujisikia vyema au vibaya, tafuta marafiki wanaokufanya ujisikie vizuri si wale wanaokufanya utake kujua.

Jisikilize
Jisikilize mwenyewe kwani hicho ndiyo hasa kitakachokufanya ujisikie vyea na kuendelea na mambo yako vyema. Kujisikia kunasuuza sana akili, tafuta muda wa kujisikiliza mwenyewe hiki ni kipindi cha kuona mambo yalivyo.

Jipumzishe
Angalau mara mbili pumzika kwa dakika tano  kuangalia make up yako, nywele pozi na nguo hata kama umeamkaje ni vyema kujitazama kuona kama uko bomba kama ulivyotoka nyumbani.

 

 


Monday, May 5, 2014

Unatunzaje Lips zako?



Hakuna raha kama kuwa na midomo (lips) zenye kuvutia tena ikiwa katika namna ambayo kila moja anaitamani kuiangalia na hata kuibusu.
Lips nzuri zina nafasi yake katika maisha ya mwanamke kwani anakuwa mwenye kujiamini tofauti na mtu ambaye anakuwa na midomo mikabu ambayo imekuwa ikipasuka mara kwa mara.
Kuna njia nyingi za kutunza Lips ikiwemo zile za kiasili na hata za kisasa lakini yote hayo hutegemea na matakwa na hata uwezo wa mhusika.
Kumekuwa na hali mbalimbali ambazo hupelekea midomo kuwa mikavu, kukatika na hata kuchubuka na kuwa na ngozi nyekundu.
Kinachoonekana zaidi ni kuwa watu wengi hawatilii sana maanani juu ya utunzaji wa midomo licha ya kuwa kuna wakati midomo inakauka au kupasuka pasuka hasa wakati wa baridi.
Midomo imekuwa ikitunzwa kwa njia za asili ikiwemo kupaka Glycerin hali inayochangia kulainisha ngozi za mdomo na kujiepusha na mipasuko.
Njia hii ya kupaka mafuta hutumiwa wakati wote hata pale mtu anapotaka kwenda kulala.
Pia mafuta haya husaidia kuondoa weusi uliopo kwenye midomo.
Pamoja na hayo pia kuna mafuta maalum ambayo hutumiwa kwa ajili ya kupaka mdomoni kwa lengo la kulainisha midomo ambayo pia kwa kiasi kikubwa inachangia wengi kuwa na midomo inayovutia hasa kwa wale wanaotumia.
Aidha kuna njia ya kutumia majani ya hiliki ambapo hutumika kwa  kusugua kwenye midomo na kupelekea midomo kuwa laoini.
Jambo lingine linalosisitizwa katika utunzaji midomo ni pamoja na kutumia maji ya limao yaliyochanganywa na asali kwa kupakwa kwenye midomo na kukaa na mchanganyiko huo kwa muda wa saa moja hiyo husaidia pia kuondoa hata weuzi uliopo kwenye midomo.
Pia Unywaji wa maji mengi husaidia katika kuimarisha midomo na hata matumizi ya mlozi (almond oil) kama yakipakwa mdomoni kabla ya kwenda kulala husaidia sana kuiweka midomo katika namna inayopendeza.