MGONGO ni moja
ya kiungo cha mwili ambacho kinahitaji uangalizi mzuri.Bila hivyo huleta tabu
hasa pale mgongo unapokuwa hauko katika muonekano mzuri.
Uchafu unaoganda kwenye mgongo hupelekea muwasho wa
mara kwa mara na mgongo kuwa na mabaka mabaka .
Ukweli ni kuwa jaribu kuangalia mgongo wako na kuona
kama unastahili kuwa hivyo na kama haustahili basi chukua hatua kwa kuhakikisha
mgongo unakuwa msafi na kutafuta tiba ya chunusi au mabakamabaka yaliyo mgongoni
mwako.
Unapoufanyia tiba mgongo kwa kutumia sabuni za dawa
au lotion utaufanya uwe na muonekano mzuri na hata kuwa huru kuvaa nguo yoyote.
Wengi wanashindwa kuvaa nguo za wazi kutokana na
muonekano wa ngozi zao za mgongoni kuwa mbaya zenye vipele, chunusi na kupauka.Madoa
kwenye mgongo yamekuwa yakikosesha wengi raha kutokana na suala la utunzaji
mgongo halitiliwi maanani kama ilivyo kwenye utunzaji wa uso au miguu.
Tumia brashi laini lenye sababu ya kutosha katika
kusugua mgongo wako. Kisha paka mafuta.
Kama huwezi kufikia vizuri mgongo kwa kutumia blashi
basi unaweza kuomba msaada ili mradi mgongo
utakate na kuwa katika sura ya kupendeza.
Wengi wanashindwa kuvaa nguo za wazi kutokana na
migongo yao kuwa na sura isiyopendeze.
Ni muhimu ukazingatia usafi wa mgongo ili uwe huru
kuvaa nguo za wazi bila kuwa na mashaka kuwa kuna watu wanautazama vibaya mgongo
wako na wengine wameanza kucheka.
No comments:
Post a Comment