Wakati wa mapishi wengi wetu hatukosi kutumia kitunguu kunogesha chakula lakini nje ya jiko pia kuna matumizi ambayo mwako wake hukufanya uwe mrembo zaidi na mwenye maarifa mengi.
Kuna hata kuking’arisha chuma na kuondoa barafu katika kioo chako cha gari .
1.Hufukuza wadudu.Ukisugua kitunguu katika ngozi yako au katika nguo zako ni namna nyingine ya kukabiliana na wadudu bila sumu
2.Kulainisha koo lenye shaka. Unatengeneza chai ya kitunguu na kunywa ili kuondoa mikwaruzo katika koo. Unachemsha maji kiasi cha kikombe kikiwa na nusu ya kitunguu (vipande) na kuinywa.
3.Kuondoa gamba. chukua kipande cha kitunguu kiweke kwenye gamba kisha funga na bandeji.Acha kama saa moja hivi. Ukiondoa itakuwa rahisi kuondoa gamba hilo kwani litakuwa limelegea.
4.Kung'arisha chuma. Ponda kitunguu na changanya na maji.Ukitumia kitambaa sugua eneo linalohusika mpaka uone limeng'aa.
5.Kupoozesha ulipong'atwa na mdudu au nyuki. Sugua eneo hilo lililoumwa na kitunguu na utasikia maumivu yanapungua.
6.Kusafishia cha chuma cha kuokea.kata kitunguu na kwa kutumia umma mrefu pachika kitunguu.Ondoa kwanza mabaki magumu ka kutumia brashi na kisha washa jiko. Tumia umma wako kupitisha kitunguu katika chuma cha kuokokea mpaka uchafu wote umeondoka.
7.Hufukuza mchwa.Kama kila mara mchwa wanafika katika jiko lako kata kiasi kingi cha kitunguu na kiache wazi. Harufu yake itawakimbiza.
8. Tengeneza dai ya DIY . pamoja na rangi yake, unaweza kutengeneza dai ya nguvu yenye rangi ya njano au nyekundu.Chukua maganda ya vitunguu na tumbukiza katika mfuko wa maziwa na funga mwishoni.Chemsha kwa dakika kama 20 kimiminika kitakachobaki ni dai ambayo inafaa kwa ajili ya kutiwa katika karatasi,nyuzi au kitambaa
9.Humeza harufu ya wali ulioungua. Ukiwa hupendi harufu ya kuungua kwa wali waweza kuweka nusu ya kitunguu karibu na jiko harufu ile itamezwa na kitunguu.
10.Huzuia ukungu kwenye kioo cha gari. kata kitunguu nusu na kisugue kwenye kioo wakati wa usiku.Itazuuia ukungu kujitengeneza wakati wa usiku.
11.Kutia rangi mayai ya pasaka.Zungushia mayai na ngozi za vitunguu na kisha zihifadhi katika mataulo.Weka taulo hilo katika maji yanayochemka na chemsha mayai kama kawaida. Utayatoa yakiwa tayari na rangi ya manjano iliyokoza
12.Husaidia maparachichi kutokuwa ya kahawia.Weka vipande vya vitunguu vyekundu na maparachichi katika kontena lisiloingiza hewa.
13. Humeza rangi mpya. kata vitunguu na viweke katika bakuri lenye maji na kisha weka bakuri hilo katika chumba kilichotiwa rangi kwa usiku mzima ili harufu ya rangi imezwe.
14.Safishia visu vilivyoingia kutu. Chukua kitunguu kikubwa kisha kichome na kisu chenye kutu!
15.Huzuia wanyama usiowataka.Paka na wa jamii yake huzuiwa na kitunguu kama utakikata kitunguu hicho vipande na kumwaga kuzunguka bustani yako.
16. Hupoozesha palipoungua.Sugua kitunguu juu ya eneo lililoungua kwa lengo la kupunguza maumivu na kwa kuwa kitunguu kina aina ya kemikali inayokabili bakteria utakifanya kidonda chako kisivamie na bakteria.
Kitunguu ambacho hakijakatwa |
Kitunguu kilichokatwa |
No comments:
Post a Comment