Monday, September 7, 2009

Viatu visivyofaa vitakuletea ugonjwa







Wanawake wana kazi kubwa katika kuhakikisha wanaonekana wapo warembo na wana urefu unaotakiwa. Katika hali hiyo inaaminika kuwa katika wanawake wanne kati ya kumi wananunua viatu visivyowafaa wala kuwatosha.
Kura ya maoni iliyohusisha watu 2000 iliyofanywa na The Society of Chiropodists and Podiatrists imeonyesha kuwa asilimia 37 huvaa viatu vinavyowapa shida ili mradi tu wawe katika fasheni.
Asilimia 80 ya wanawake wanasema kwamba hali hiyo huwafanya wapate matatizo ya miguu kama kuota vigimbi , ukuaji wa kucha usiostahili lakini hawatafuti hata msaada wa daktari.
Lorraine Jones, kutoka Society of Chiropodists and Podiatrists, anasema kwamba hili tatizo la kutaka fasheni linaharibu afya za wanawake.
Inashauriwa kwamba mwanamke avae kiatu ambacho hakina urefu wa zaidi ya sentimeta nne na pia kina uduara kwa mbele.
Ni vyema mwanamke akaelewa kwamba kama anajisikia maumivu basi mambo si shwari hata kidogo.

1 comment:

  1. mnisaidie nini nifanye ili niondoe vigimbi vinanikela kweli.

    ReplyDelete