KARIBUNI wasomaji katika blogu hii ya urembo na utanashati.Leo naona tuzungumzie jinsi manukato yanavyoweza kuwa na manufaa katika urembo wako.
Ukitaka kuwa mrembo ni wazi kuwa unatakiwa kuuweka mwili wako katika hali nzuri ya kupendeza kuanzia mavazi, mitindo ya nywele.Ndio kusema kuna vikorombwezo kibao vinavyotakiwa ili kukufanya uwe mrembo zaidi.
Manukato nayo ni muhimu katika kunogesha urembo wako.Nadhani ulishawahi kusifiwa au kusifia mtu kutokana na manukao anayotumia na wengi wetu tumekuwa tukitumia aina za manukato ambazo tunaona zinatufaa zaidi.
Ni vizuri kuchagua aina ya manukato na njia nzuri ni kupulizia kigogo kwenye mkono wako ili uweze kujua harufu yake kama umependezwa nayo au laa. Usitumie manukato ya aina fulani kwa sababu fulani anatumia.
Jaribu kutafuta aina ya manukato uliyoyachagua kwani kuwa mnukato yana harufu kali na hili huleta taabu kidogo kwa baadhi ya watu unaokuwanao karibu.
Chagua manukato ambayo yana harufu iliyotulia na pia ukali wa manukato wakati mwingine husababisha kujipulizia kiasi kikubwa cha manukato hali ambayo huwa kero kwa wengine.
Jaribu kutumia manukato kiasi fulani kwani aina nyingine hudumu muda mrefu na unapojipulizia manukato ona unafanya hivyo kwa faida yako na sio kuhakikisha kuwa kila mtu anajua umetumia manukato ya aina fulani hapo ndiyo huleta shida kidogo kutokana na kutumia kiasi kikubwa cha manukato na hivyo kuleta shida kwa wengine.
Pia unashauriwa kutotumia manukato ili kuondoa harufu ya mwili kutokana na kutooga au kutokana na sababu nyingine hapo maana ya manukato hupotea. Manukato hupendeza iwapo yatapuliziwa wakati mwili na nguo zikiwa safi. Tumia aina ya manukato uipendayo ili kuweza kukuweka mrembo zaidi.
No comments:
Post a Comment