Sunday, September 6, 2009

Mikato ya nywele inafaa kuzingatia kichwa











Hakuna kitu kinachofurahisha kama nywele za mwanamke. Nywele za mwanamke zinapowekwa sawa na uso wake, humfanya awe na mng'ao usiokuwa wa kawaida.
Nywele za mwanamke zinaheshimika zinathaminika na ama hakika ni hazina moja ya maana kwa mwanamke iwe zimekaangwa au zimewekwa tu kama vile mchemsho.
Nywele na staili zake hazijabadilika sana ingawa zamani nywele zilikuwa zinawekwa vitu vingi katika mizungusho ya kawaida ya kuremba na wakati mwingine kuachwa tu zikijiotea na wengine wakitumia muda mwingi kuzisuka.
Ni vyema kama mwanamke unataka kupendeza kichwani kufika kwa wataalamu wa nywele ambao watazitengeneza au kukupa ushauri kutokana na kichwa chako na si vingine.
Ni kutokana na hali hiyo lkeo tunakuletea picha mbalimbali za watu na miondoko yao kichwani kwa lengo la kukuonyesha kwamba unachosuka kichwani inafaa kifanane na kichwa chako.
Si misuko tu bali hata utengenezaji wa huria wa kutumia dawa au hata dawa za asilimi ni lazima izingatiwe ukubwa wa kichwa na namna ambavyo ungelipenda wewe uonekane.
Zamani misuko ilikuwa ya kuchekesha zaidi na matumizi ya kofia yalimaliza utata uliopo kichwani kwa wakati unapoangaliwa kwa makini.
Nataka kukuambia kwamba nywele nyingi hutengenezwa kwa kuangalia unataka kumvutia nani na kwanini.

No comments:

Post a Comment