Monday, September 28, 2009
Jinsi ya kuondoa kikwapa
Wengi wamekuwa wakitumia sabuni, krimu na hata pafyumu za aina mbalimbali kwa ajili ya kuondoa uchafu wa kwenye kwapa lakini bila ya mafanikio yoyote.
Matumizi ya ndimu na limao yana matokeo mazuri kwamwili wako kama utatumia kikamilifu.
Unachotakiwa na kufutafuta limao au ndimu unaikata kisha unakamua. Chukua kitambaa weka maji maji ya limao na kisha anza kusugua taratibu kwapa lako.
Hakikisha unafanya hivyo wakati ukiwa umetoka kuoga. Pia unaweza kukata limao au ndimu bila ya kukamua na kuanza kusugua katika kwapa lako. Vitu hivyo vina nguvu za kuondoa uchafu katika kwapa.
Ni muhimu kusafisha kwapa kwani kwapa linapokuwa si safi hata unapovaa nguo ya wazi unakuwa huna uhuru wa kunyanyua mkono juu pindi inapokulazimu kufanya hivyo.
Kwapa ni sehemu muhimu sana ni lazima iangaliwe kwa namna ya pekee na uhakikishe unakuwa safi muda wote ili kuondoa harufu na muonekano mbaya katika kwapa.
Umuhimu wa manukato katika urembo wako
Ukitaka kuwa mrembo ni wazi kuwa unatakiwa kuuweka mwili wako katika hali nzuri ya kupendeza kuanzia mavazi, mitindo ya nywele.Ndio kusema kuna vikorombwezo kibao vinavyotakiwa ili kukufanya uwe mrembo zaidi.
Manukato nayo ni muhimu katika kunogesha urembo wako.Nadhani ulishawahi kusifiwa au kusifia mtu kutokana na manukao anayotumia na wengi wetu tumekuwa tukitumia aina za manukato ambazo tunaona zinatufaa zaidi.
Ni vizuri kuchagua aina ya manukato na njia nzuri ni kupulizia kigogo kwenye mkono wako ili uweze kujua harufu yake kama umependezwa nayo au laa. Usitumie manukato ya aina fulani kwa sababu fulani anatumia.
Jaribu kutafuta aina ya manukato uliyoyachagua kwani kuwa mnukato yana harufu kali na hili huleta taabu kidogo kwa baadhi ya watu unaokuwanao karibu.
Chagua manukato ambayo yana harufu iliyotulia na pia ukali wa manukato wakati mwingine husababisha kujipulizia kiasi kikubwa cha manukato hali ambayo huwa kero kwa wengine.
Jaribu kutumia manukato kiasi fulani kwani aina nyingine hudumu muda mrefu na unapojipulizia manukato ona unafanya hivyo kwa faida yako na sio kuhakikisha kuwa kila mtu anajua umetumia manukato ya aina fulani hapo ndiyo huleta shida kidogo kutokana na kutumia kiasi kikubwa cha manukato na hivyo kuleta shida kwa wengine.
Pia unashauriwa kutotumia manukato ili kuondoa harufu ya mwili kutokana na kutooga au kutokana na sababu nyingine hapo maana ya manukato hupotea. Manukato hupendeza iwapo yatapuliziwa wakati mwili na nguo zikiwa safi. Tumia aina ya manukato uipendayo ili kuweza kukuweka mrembo zaidi.
Namna ya kuondoa vipele na mafuta usoni
Kitendo hicho huitwa scrub.Husaidia kuondoa chunusi,vipele na makovu na pia inapunguza mafuta usoni.
Uso unapokuwa na mafuta sana na kuyaondoa kunasaidia kupunguza vitu vingi pamoja na vipele na hata mabaka yaliyosababishwa na vipele au chunusi.
Unaweza kutumia scrub ya kwa njia ya mikono kwa kila baada ya siku tatu, na scrub ya mashine baada ya mwezi mmoja.
Scrub ya mkono.Tafuta aina ya scrub inayokufaa kulingana na ngozi yako.safisha uso wako mpaka uhakikishe kuwa umetakata kisha chukua scrub na kuanza kusugua usoni taratibu kwa muda wa dakika tano kisha nawa uso na unaweza kupakalosheni au poda baada ya kunawa.
Scrub ya mvuke.Chesha maji Nawa uso kwa kutumia maji safi na uhakikishe kuwaumetakata.
Futa uso kwa kutumia taulo safi.
Paka scrub usoni na pia shingoni kama utapenda. Sugua uso kwa kutoa taka.Chukua taulo jifunike na kisha inamia beseni lenye maji ya moto.Baada ya dakika tano toka na subiri kwa muda wa dakika tano nyingine kisha nawa. Paka poda au losheni.
Pia unaweza kutembelea saluni za kisasa kwa ajili ya kuufanyia facial uso wako Pia unaweza kutafuta sabuni ya ukwaju na ukawa unanawa uso asubuhi na jioni hii huondoa upele, chunusi na mabaka usoni
Thursday, September 17, 2009
namna bora ya kutunza miguu
Sasa tuzungumzie juu ya utunzaji wa miguu. Miguu ni sehemu inayoangaliwa sana hasa kwa wanawake, kwani unapoamua kuvaa nguo fupi na huku miguu yako haiko katika hali ya kuvutia sina shaka utaanza kujishuku hata kabla ya kutoka nje.
Miguu ni sehemu ambayo inatakiwa kutunzwa kwa kipekee kama ilivyo sehemu nyingine kama uso. Wengi tumekuwa tukipendezesha nyuso zetu na kusahau kbisa habari za miguu.
Haijlishi miguu yako ni miembamba au minene iwapo utaitunza vizuri sina shaka kuwa utavutia kwa nguo yoyote utakayoivaa.
Kuna njia nyingi za kutunza miguu na unaweza kutunza miguu yako hata kama huna fedha za kununulia vikorokoro vinavyotakiwa.
Unaweza kuchukua beseni na kuweka maji ya uvuguvugu yenye povu la sabuni maalum ya kuoshea miguu kisha loweka miguu na iache kwenye maji kwa muda wa robo saa hivi.
Chukua aina ya scrub uliyoichagua kwa ajili ya miguu yako paa na ikikauka anza kusugua miguu yako na hadi kwenye vidole na unyayo.
Kisha jisafishe kwa maji ya uvuguvugu.
Baadhi ya vitu unavyoweza kutumia ili ku kutengeneza miguu yako ni pamoja na foot file, Therapysa virgin vie salt scrub, Pedicure iliyotengenezwa kwa OPI Refresh Cooling ffot Gel, Innoxa cool na Calm liquid talc na Feet first reviving Foot Soak.
Bidhaa hizi unaweza kuzipata kwenye duka kubwa la vipodozi na pia utpata maelezo jisi ya kutumia
Pia unaweza kutembelea baadhi ya saluni ambazo zinatoa huduma hiyo jitahidi hata mara moja kwa mwezi kuhakikisha miguu yako inapata huduma nzuri ili iwe ya kuvutia.
Kwa wale ambao miguu yao ni makovu au madoadoa wajaribu kutumia scrub na kama hawatafanikiwa kuondoa tatizo hilo basi wanashauriwa ktumia cream na sabuni zenye mchanganyiko wa ukwaju kwani zinasaidia sana kuondoa madoa.
Pia unaweza kuchukua mkwaju ukaloweka kwenye maji ukishalainika changanya mchanganyiko huko na asali kasha paka.
Husaidia kuondoa madao na hata kwa wale wenye ngozi za mafuta na chunusi sugu mafuta yatakauka na chunusi hazitatoka tena.
Namna ya kuhami ngozi laini inayozunguka jicho
Monday, September 14, 2009
uondoaji chunusi kwa njia za kiasili
Jamani hebu hurumieni nguo zenu, zitunzeni
Watu hutumia mamilioni kama si maelfu ya fedha zao kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wanakuwa bomba na wenye kuvutia. Lakini ni kawaida mno kuona watu hao hao wakitupa fedha hizo kwa kuzivuruga nguo zao na kuziweka pasipo heshima kiasi ya kwamba huchakaa haraka au huharibika kwa muda mfupi sana.
Wengi wetu ambao tuna haki ya kujiita watanashati tuna matatizo makubwa sana ya utunzaji wa nguo zetu na wakati mwingine tunasahau kwamba nguo hizo ni raslimali zetu ambazo zikiharibika na sisi vile vile tunaharibika.
Mathalani mtu ananunua nguo kwa paundi 4000, fedha nyingi kabisa, lakini mtu huyu ambaye alitakiwa kuheshimu nguo zake unaweza kuingia chumbani mwake ukazikuta zimetupwa tu holela kitandanim, kwenye kochi na wakati mwingine hata bsakafuni.
Wewe mtu anavua suti na kuitupa, mtu anavua sidiria na kuitupa yaani mambo yote hata hayaeleweki.
Lakini nataka kusema hivi unapokuwa unabadilisha nguo kumbuka kuzihifadhi na kuzitunza kwani hiyo ni raslimali zako mwenyewe.
Kutokana na hali hiyo nataka kukueleza kuwa nguo ziku zote zinatakiwa kuwekwa kwa urefu wake ili zirejee katika hadhi yake ya kawaida.
Ni vyema kwelikweli na nasisitiza kuweka nguo zako kwa kuzitundika ili zirejee katika ule uzuri wake wa dukani na katika matenegnezo.
Ni vyema kama kabati lako halina nafasi ya kuweka vining'inizo ukaviweka kwani ni vya maana sana hsa vile vilivyotengenezwa kwa mbao.
Na wakati mwingine tumia vishikizo ambavyo vinasimamiwa pia na vitu vngine. Ninachotaka kusema hatakama ni sketi iweke katika nafasi yake inayostahili.Vivyo hivyo kwa jaketi na suruali na hata mashati.
Pamoja na kuweka nguo yaani kuzitundika ili kupata uhalisi wake ni vyema pia kuwa na mpango katika kabati lako si tu kujifanyia mambo kama mwendawazimu.Manake kama hukuwa na mpango itakuchukua siku nzima kujua ni wapi umeweka brazia au nguo yako ya ndani.
Ni lazima siku moja uamue kufanya ratibu ya kabati ili liwe na maana kubwa kwako na kukuwezesha kufanya maamuzi ya kasi wakati wa kuchagua nguo za kuvaa ziwe za ndani au nje.
Naomba usiruhusu kwa namna yoyote ile uwekaji wa mifuko ya nailoni kwani hutunza hewa ya unyevu na hii huleta uvundo katika nguo.
Pia kufanya mambo yako yawe bomba tafadhali fanya mambo mawili. Moja hakikisha kwamba nguo za zamani unazitoa ambazo zimemalizika muda wake wa fasheni.
Na maana kubwa sana ni kuwa upangaji husaidia pia kukuwezesha kufanya mambo ambayo pengine huyapati kwa uzuri kuwa na nafasi ya kuona.
Utunzaji wa nguo hauko tu katika kuziweka vyema bali hata wakati wa kufua,Angalia kwa makini maelezo ya nguo zako, maji yanayostahili kutumika joto na pia aina ya sabuni. Na ukishamaliza basi zinyooshe kama zinavyotakiwa.
katika masuala haya ni pamoja na viatu kuangaliwa, kusafishwa na pia kutunzwa kwa mujibu wa maelekezo ikiwemo ya utiaji wa kiwi.
Wednesday, September 9, 2009
Umaridadi wa kupaka rangi kucha
Ili uwe na kucha maridadi masuala ya kuzisafi na kuziweka rangi ni muhimu ama sivyo? na kwa kawaida kucha zilizo safi ndizo hasa zinazokubali polishi yaani rangi au sivyo?
Na ama hakika kucha zilizo safi ndizo hasa zinazotengenezwa na kuwekwa sopusopu.
Ni vyema kutambua kwamba wakati wa kupaka rangi tumia mipako michache kwa kila mpako na kila mpako uachie ukauke kabla ya kuanza mpako mwingine.
Na ile ya mwisho inatakiwa kuwa bomba zaidi kwa kuwa ndio hasa itakayokuwa inatunza matabaka mengine yote.
Utengenezaji mzuri wa kucha si lazima uwe wa kwenda katika mapumziko au kuonyesha mtu ni kitu ambacho kinafaa kufanywa ili uwe mrembo kila mahali.
Kuna raha ya kujisikia katika rangi mpya katika mwaka mzima na hasa kama uchaguzi wako wa rangi za kupaka ni bomba.
Moja rangi ya pinki ama nyekundu inakupa nafasi ya kuwa funny . Unaweza kujipaka rangi mwenyewe au kuwambia mtu akupake rangi.Kuna hatua kadhaa ambazo unatakiwa kuzifanya kabla ya kupaka rangi kucha zako.
Hatua ya kwanza ni kuondoa rangi zote za awali.kwa kufanya hivyo rangi mpya itakuwa ina uwezo wa kushika katika kucha.
Pia kunasaidia rangi yako mpya isitibuliwe na rangi ya zamani kwa namna yoyote ile.
Unaweza kuondoa rangi ya zamani kwa kutumia dawa inayopatikana katika maduka ya dawa na hata yale ya vipodozi na pamba hufanya vyema kartika kuondoa rangi za kucha kwa kutumia Nail polish remover.
kazi ya pili ni kutafuta rangi inayokupendeza. unaweza kutumia rangi yoyote kwa sababu mara nyingi viatu vinazuia kuonekana kwa kucha zako la kama unahitaji rangi fulani kwa sababu miguu yako i wazi ni vyema sana.
Tazama kwamba vipaka rangi vyenyewe ni vipya kwani vilivyozeeka huleta tatizo kidogo.mara nyingi vipaka rangi vilivyokaa miaka miwili havifai tena kutumika.
Anza kupaka baada ya kubainisha kwamba unaweza kutenganisha kidole kwa kidole ili usipake kila mahali hasa kama brashi husika ni pana kidogo.
Anza katikati kwa kuanzia nyuma kupeleka mbele kisha nenda pembeni na pembeni.Na baada ya kukauka unaweza kuongeza tabaka jingine tena na tena.
Kisha paka ile ya mwisho ambayo ndiyo italinda rangi yenyewe yaani top coat . top coat husaidia sana kuweka rangi kwa muda mrefu. Top coat ni polishi isiyokuwa na rangi na kama unataka kuweka stika iweke mapema kabla ya kuweka top coat.
rangi nzuri na zilizotulia zinakufanya uwe na sababu ya kujivalia sandals zako nzuri au viatu vya wazi
Monday, September 7, 2009
Viatu visivyofaa vitakuletea ugonjwa
Kura ya maoni iliyohusisha watu 2000 iliyofanywa na The Society of Chiropodists and Podiatrists imeonyesha kuwa asilimia 37 huvaa viatu vinavyowapa shida ili mradi tu wawe katika fasheni.
Asilimia 80 ya wanawake wanasema kwamba hali hiyo huwafanya wapate matatizo ya miguu kama kuota vigimbi , ukuaji wa kucha usiostahili lakini hawatafuti hata msaada wa daktari.
Lorraine Jones, kutoka Society of Chiropodists and Podiatrists, anasema kwamba hili tatizo la kutaka fasheni linaharibu afya za wanawake.
Inashauriwa kwamba mwanamke avae kiatu ambacho hakina urefu wa zaidi ya sentimeta nne na pia kina uduara kwa mbele.
Ni vyema mwanamke akaelewa kwamba kama anajisikia maumivu basi mambo si shwari hata kidogo.
Sunday, September 6, 2009
Mikato ya nywele inafaa kuzingatia kichwa
Nywele za mwanamke zinaheshimika zinathaminika na ama hakika ni hazina moja ya maana kwa mwanamke iwe zimekaangwa au zimewekwa tu kama vile mchemsho.
Nywele na staili zake hazijabadilika sana ingawa zamani nywele zilikuwa zinawekwa vitu vingi katika mizungusho ya kawaida ya kuremba na wakati mwingine kuachwa tu zikijiotea na wengine wakitumia muda mwingi kuzisuka.
Ni vyema kama mwanamke unataka kupendeza kichwani kufika kwa wataalamu wa nywele ambao watazitengeneza au kukupa ushauri kutokana na kichwa chako na si vingine.
Ni kutokana na hali hiyo lkeo tunakuletea picha mbalimbali za watu na miondoko yao kichwani kwa lengo la kukuonyesha kwamba unachosuka kichwani inafaa kifanane na kichwa chako.
Si misuko tu bali hata utengenezaji wa huria wa kutumia dawa au hata dawa za asilimi ni lazima izingatiwe ukubwa wa kichwa na namna ambavyo ungelipenda wewe uonekane.
Zamani misuko ilikuwa ya kuchekesha zaidi na matumizi ya kofia yalimaliza utata uliopo kichwani kwa wakati unapoangaliwa kwa makini.
Nataka kukuambia kwamba nywele nyingi hutengenezwa kwa kuangalia unataka kumvutia nani na kwanini.
Chumvi,sukari nyingi huzeesha ngozi
Wednesday, September 2, 2009
Namna yakujiweka fiti kwa mwanamke
5) Punguza uvutaji sigara na pombe kwani ni vitu viwili vinavyozeeshangozi kwa kasi.