Sunday, September 28, 2014
Tumia mchanganyiko wa papai na asali kuondoa madoa usoni
Kuna maswali mengi yanayoulizwa jinsi ya kuondoa madoa usoni. Lakini jambo kubwa la kuangalia
je madoa uliyonayo
yamesababishwa na nini, Je ni kwa ajili ya kutumia madawa yenye kemikali kali kwa lengo la kupendezesha ngozi au ni
vipele tu vya kawaida.
Wengi wanapenda kutumia sabuni na cream kali ambazo baadaye zimekuwa zilileta madhara makubwa kwenye ngozi zao na
kuwafanya kuwa na mabaka meusi.
Ni muhimu pia kujifunza kutumia vipodozi vya asili ambavyo havina madhara kwenye ngozi.
Unaweza kutumia mchanganyiko wa papai na asali kwa ajili ya kuondoa madoa usoni.
Mchanganyiko huu ambayo huwa laini utauacha ngozi yako ikiwa nyororo na yenye kuvutia.
Namna ya kutumia.
Kwanza ni kusafisha uso kwa maji ya vuguvugu kwa kutumia kitambaa laini pia unaweza kusafisha hadi shingoni na hakikisha
uso umekataka kisha futa uso wako na shingo kwa taulo.
Andaa asali yako pembeni kisha kata papai na kisha liponde hadi kulainika kabuisa.
Baada ya hapo changanya rojo hiyo ya papai na asali koroga hadi kuhakikisha umepata mchanganyiko mzuri.
Anza kupata usoni taratibu hadi maeneo ya shingo unaweza kukaa na mchanganyiko huo kwa robo saa kisha safisha uso
wako.
Unaweza kutumia mchanganyiko huu mara kadhaa kwa wiki mpaka upate matokeo mazuri kwenye ngozi yako.
Lakini jambo la msingi ni kuhakikisha anaepuka kutumia cream zenye kemikali kali kwani zimekuwa na madhara kwenye
ngozi.
Saturday, August 23, 2014
Tumia limao kuondoa madoa meusi usoni
KUMEKUWA na sababu mbalimbali zinazofanya watu kutokuwa na
ngozi zisizokubalika.Mbali na hali ya hewa pia matumizi ya pombe na sigara hata
matumizi ya cream kali ambazo zimekuwa zikitumiwa na watu bila kujua madhara
yake kumechangia kwa kiasi kikubwa tatizo hilo.
Ngozi kwa kawaida inatakiwa ijitengeneze yenyewe na si
kuitengeneza kwa vipodozi kama wengi wanavyodhani. Ulaji wa matunda na mboga za
majani kwa wingi kunywa glasi nane za maji kwa siku ni njia nzuri kama unataka
kuwa na ngozi nzuri isiyo na madoa wala ukavu ambao haupendezi.
Wengi wanaacha kula mbogamboga na matunda kwa wingi hata
kutokunywa maji ya kutosha na badala yake wamekuwa akitegemea kuwa na ngozi
nzuri jambo ambalo ni gumu.Mara kadhaa tumeshuhudia watu wanaopaka cream kali
wakiwa kama wameungua usoni huku uso na mwili ukionekana kuwa makavu jambo
ambalo linaashiria kuwa kupaka cream si
suruhisho la kuwa na ngozi nzuri.
Kuna watu wamekuwa na ngozi za asili na hata unapowauliza
baadhi yao hawajawahi kupaka cream hata siku moja na bado wana ngozi nzuri
zinazovutia hao wamekuwa wakila kwa ajili ya kuhakikisha wanatengeneza ngozi
zao kutoka ndani.
Pia wengi wanaharibu ngozi zao na kuwa na madoa kutokana na
kutumia make up kwa muda mrefu na hata
anapogundua kuwa ana tatizo la madoa amekuwa akijaribu kutumia cream nyingine
kwa ajili ya kumaliza tatizo hilo jambo ambali linazidisha madhara kwenye
ngozi.
Unaweza kutibu ngozi yenye madoa usoni pia mashavuni kwa kujitibu na juisi ya limao.
Namna ya kufanya
Chukua limao lioshe
na kisha likamue na kuchuja mbegu zake. Weka juisi hiyo kwenye kikombe na kisha
tafuta kitambaa laini kichovye kwenye
juisi ya limao na dondoshea juisi ya limao kwenye sehemu zenye tatizo.
Kaa kama dakika tano
kisha usha uso kwa maji safi.Pia unaweza kuchanganya na asali mbichi na maji ya limao husaidia pia kuondoa madoa
usoni.
Limao lina sifa kubwa ya kuzuia harufu pia unaweza kulitumia
katika kuondoa harufu kali ya jasho mwilini
na husaidia kuondoa weusi kwenye kwapa, chini ya macho, mapajani pia.
Chukua kipande cha limao weka sukari kidogo, sugua.Unatakiwa kutumia
kwenye kwapa ambalo ni safi, vizuri kutumia njia hii kabla na baada ya kuoga.
Wednesday, August 20, 2014
Unatunzaje mikono yako?
Ili kuweka mikono yako kuwa na muonekano mzuri wa asili na
kuwa laini unatakiwa kuipa uangalizi wa kutosha ukiwa nyumbani. Mikono imekuwa
ikitumika na kazi nyingi za nyumbani hata ofisini na wakati mwingine tumekuwa
tukishika vitu ambavyo vinasababisha mikono kuwa migumu na hata iliyobabuka.
Watu wengi wamekuwa wakitengeneza nyuso zao na kusahau kabisa habari za kutunza mikono kitu ambacho si sawa sawa.
Unatakiwa kujifunza vitu gani vinatakiwa ili kuweza kuiweka mikono yako katika hali nzuri ikiwemo aina ya scrub na moisturizer ambayo itafanya mikono yako kuwa katika hali nzuri kila wakati.
Unaweza kutengeneza mikono yako ukiwa nyumbani au hata saluni lakini kama utafanya mara moja kwa wiki utakuwa na mikono ambayo iinaonekana vizuri.
Ili kutengeneza mikono yako unatakiwa kuwa na nail file (tupa ya kucha), brashi ya mikono, kitu cha kukatia kucha (hata webe unafaa) losheni ya mikono, taulo sabuni na maji wa vuguvugu.
Unatakiwa kuosha mikono na ukate kucha na kisha anza kuzisugua taratibu kwa kutimua tupa.
Kisha weka maji ya vuguvugu kwenye beseni na tumbukiza mikono kaa kwa muda wa dakika tano ili kuwezesha ngozi ya mikono kulainika.
Kisha anza kusugua mikono taratibu unaweza kutumia kitambaa laini ila unachotakiwa kuhakikisha unasafisha hadi sehemu za katikati ya vidole baada ya hapo suuza mikono yako na ufute kwa taulo halafu paka lotion ya mikono. Njia nzuri pia ya kutunza mikono ni kuhakikisha unakula chakula chenye kulainisha mwili na kunywa maji mengi.
Kama unakuwa hujali mwili wako na hunywi maji mengi unaweza kuwa na mikono mikavu.

Wednesday, July 30, 2014
Tengeneza mwili wako kwa kunywa maji ya Aloe Vera
Kwa ukweli kuna mshindani mpya wa maji yanayorekebisha mwili wako na kuonekana mrembo zaidi. Watu wa urembo ambao walikazania unywaji wa maji ya dafu sasa wana kitu kipya mtaani, kinywaji cha aloe vera.
Aloe vera wataalamu wanasema kwamba ikinyweka katika maji inasaidia sana kuyeyusha chakula, kuondoa sumu zilizomo mwilini na kuondoa kiungulia lakini kubwa zaidi linabortesha muonekano wako.
Wataalamu wanasema pamoja na kuleta lishe katika mwili kuondoa tatizo la maji kwa ajili ya mwili na ngozi pia ina homoni mbili za Auxin na Gibberellins ambazo huleta kinga dhidi ya viungulia na pia kuleta uponyaji.
Kauliu hiyo imetolewa na mwasisi wa Sublime Beauty, Kathy Heshelow, Gibberellins zinaaminika kuchochea ukuaji wa seli mpya kwa kuimarisha fibroblasts amnbazo hutengeneza collagen.
Maji haya husafisha tishu za ngozi ambazo huathirika sana na sukari na pombe.
Mwili unapokuwa msafi na ngozi nayo inakuwa safi na maji haya yanasaidia sana kuufanya mwili kuwa bora.
Maji ya aloe vera yanapatikana katika maduka makubwa lakini waweza tengeneza kwa namna hii:
chukua aunzi moja ya juisi changanya na aunzi nane za maji kila siku.

Saturday, July 19, 2014
Tumia asali kufanikisha urembo wako
Nauza asali mbichi ambayo haijachanganywa na chochote ni nzuri kwa ngozi na afya yako. Bei ni Sh. 10,000 kwa kilo moja na Sh. 5,000 kwa nusu kilo.
Mawasiliano 0719818644/0762650760
Mtaalam mmoja wa ngozi mwenye makazi yake mjini New York City ambaye pia ni daktari, Amy Wechsler anasema hali ya kunyunyurika iliyonayo asali na inayonasa inafanya kuwa kinga imara katika kidonda ambacho kinahitaji kisiingiliwe n vimelea na kutoa mazingira ya kuponya, hivyo asali ni bomba kwa tiba.
Pamoja na tiba asali ni moisturize babu kubwa kwa ajili ya sura na mwili pia.
Asali ni dawa ya asili ambayo ina uwezo wa kukusanya maji kutoka ndani ya misuli hadi katika sehemu za juu a ngozi na hivyo kusaidia kuondoa mikunjo.
Mimi nakushauri jaribu moisturizing ya asali ambayo itaondoa ukavu wa ngozi yako na hata kuwasha na kutatarika.
Changanya vijiko vya mezani viwili vya asali na vijiko viwili vya mezani vya maziwa.
Kisha pasha moto mchanganyiko huo, kisha paka mchanganyiko huo katika uso wako na kupumzika kwa dakika kama kumi hivi.
Kisha jioshe kwa maji ya vuguvugu.Kama unataka kitu kama kosmetiki agiza lotion ya asali ili kuweka sawa ngozi yako.
Hakikisha unanunua lotion ambayo imetengenezwa kwa asali isiyochujwa.
Aina zote za asali zinasaidia kuondoa mikunjo ya uzeeni.

Sunday, June 22, 2014
Pedal Pusher, kivazi cha wanawake wanaojiamini
Vazi la pedal pusher hutengenezwa kutokana na
vitambaa maalum vya suti, jeans au vya kawaida .
Vazi hilo huvaliwa likiwa na blausi au shati fupi na hupendeza zaidi kama likivaliwa na kikoti juu .
Unaweza kuvaa pedal pusher kazini, kwenye sehemu za starehe na huendana na urefu wake kulingana na mapenzi ya mvaaji.
Viatu vya chini au viatu virefu hufaa kubaliwa na kivazi hicho.Pedal pusher iliyoishia magotini hupendeza sana ikiwa itavaliwa na viatu vifupi na ile iliyo ndefu kupita magoti hupendeza sana kama itavaliwa na viatu virefu, ‘high heels' .

Sunday, May 25, 2014
Athari za ngozi iliyoungua na jua
KUNA Msomaji ametuma swali akisema kuwa, yeye ni mwaume
mwenye umri wa miaka 30 na amekuwa akifanya shughuli zake chini ya mti ambapo
licha ya kuwa na jua kali wakati mwingine kunakuwa na upepo mkali, hali hiyo imesababisha
ngozi yake kuungua na jua na ngozi yake kukakamaa imekuwa na makunyanzi kiasi
cha kumtisha.
Kulingana na tafiti mbalimbali za kiafya, watalaam
wanasema kuungua na jua usoni kunalazimisha ngozi kuongeza uzalishaji wa
melanin hali ambayo husababisha mtu kuwa na ngozi nyeusi na kuwa kama kahawia
(brown).
Pia unaweza kupata ngozi nyeusi au kahawia kama
miale ya jua inakuwa inakupiga moja kwa moja usoni kwa asilimia 60 hadi 80.
Vitamin E inaonesha kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia
mtu asipigwe na miale ya jua usoni, vitamin
E hupatikana katika vyakula kama mafuta
ya soya, karanga, nafaka, mboga za majani, kini cha yai na nafaka ambazo
hazijakobolewa.
Vitamini E husaidia kukua kwa nywele mara mbili ya
kiwango cha ukuaji wa kawaida, pia matumizi ya lotion za kuzuia kuungua na jua
zinasaidia sana ili kujikinga na miale ya jua.
Aidha kuungua na jua huwapata watu ambao mara nyingi hufanya kazi zao wakiwa
juani aina nyingine ya ngozi ni rahisi sana kuathiriwa na jua na
zinahitaji ulinzi zaidi.
Pia ni vizuri kama kila moja atachukua tahadhari
mapema ili kujilinda na kulinda ngozi yake isipate tatizo hili.
Watu ambao ngozi zao zimeathirika na jua wanatakiwa
kuepuka kushinda juani na wanatkiwa kunywa maji mengi na kula mboga za majani
na matunda kwa wingi ili kuweza kurekebisha tatizo lililopo.
Kwa wale wenye makunyanzi kabla ya umri wanashauriwa
kula vyakula vyenye chumvi au sukari kiasi kwani matumizi makubwa ya sukari na
chumvi ni chanzo cha kuwa na makunyanzi.
Ikumbukwe kuwa kuna vuitu vingi ambavyo miili yetu
inahitaji ili kuwa na ngozi nzuri kana usingizi wa kutosha, kupumzika, kufanya
mazoezi na kula vizuri.
Saturday, May 24, 2014
Mavazi hutambulisha tabia ya mtu
Muhimu kutambua mavazi ni njia kubwa na
nzuri ya kutambulisha tabia ya Mtu. Wengi wanapendwa au wanachukiwa kutokana na
mavazi wanayovaa. Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakivaa mavazi yasiyo na heshima
ama kwa kuwa mafupi au yamekuwa yakiacha sehemu kubwa ya kifua kuwa wazi.
Wasichana wa sasa wanaona kuvaa nguo zinazoacha wazi sehemu kubwa ya matiti kama fasheni.
Kuna mavazi
ya aina nyingi ambapo yakivaliwa humfanya mtu apendeze au achukize. Uvaaji wa
nguo unatakiwa kuzingatia umri na rangi ya mwili na pia mazingira ya nguo
inapovaliwa.
Sio kila
nguo ni ya kuvaliwa mchana na sio kila nguo ni ya kutoka nayo barabarani aina
nyingine za nguo hazistahili kuvaliwa barabarani unapotoka tu barabarani unaanza kupigiwa miluzi hiyo si sawa sawa.
Mathalani wewe
ni mfanyakazi unajua unatakiwa uvaaje, kujiweka mrembo na mtanashati ni kitu
muhimu. Siku hizi kuna mitimbo mbalimbali ya nguo za madukani, kushona mitindo
ya kutumia vitenge, vitambaa kwa mitindo ambayo inatunza heshima ya mvaaji.
Unatakiwa
kuvaa kulingana na mahali na wakati kwani kuna nguo za kazini na za kutokea
lakini sasa hivi si ajabu ukakutana na mtu mchana wa jua kali akiwa amevaa nguo
ya usiku au kumkuta akiwa amevaa viatu virefu huku akijua fika anatembea kwa
miguu kwa umbali mrefu.
Subscribe to:
Posts (Atom)