Thursday, December 19, 2013
Zijue faida za karoti kwenye urembo wako
KAROTI zimekuwa zikipatikana msimu mzima wa mwaka na zimekuwa zikiuzwa kwa bei ambayo kila mtu anaimudu.
Ni chakula ambacho kina utajiri mkubwa wa vitamini na madini yenye faida nyingi mwilini.
Kutokana na utajiri huo karoti sasa imekuwa ikitumika zaidi kwa ajili ya kutengeneza vipodozi vya aina mbalimbali pamoja na sabuni.
Ulaji wa karoti au supu yake ni muhimu zaidi katika kutengeneza ngozi kuliko hata kutumia vipodozi kama ilivyo kwa mwili ambapo mwili unaolishwa vizuri ndiyo umekuwa na ngozi nzuri zaidi.
Wataalam wa afya wanasema ni bora kula karoti kwa wingi kama unataka kuwa na ngozi yenye muonekano mzuri.
Aidha Beta-carotene inayopatikana ndani ya karoti inapoingia mwilini ina uwezo wa kubadilishwa na kuwa vitamin A Aidha kirutubisho cha Fiber kilicho ndani ya karoti ni muhimu kutokana na kukinga kuta za utumbo.
Unapotumia karoti mara kwa mara ina uwezo wa kufanya ngozi yako kuwa nzuri na yenye kuvutia.
Pia karoti ina asilimia kubwa ya Vitamin C na vitamin D, aidha ina madini Folat, Zink, Madini ya chuma na Calcium
Wataalam wa afya wanasema unapokula gramu 50 hadi 75 za karoti kila mara unakuwa umejiwekea kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali .
Tafiti mbalimbali zilizofanywa zinaonesha karoti zimekuwa na nguvu kubwa ya kukinga watu juu ya kansa ya koo kutokana na vitamini na madini iliyomo ndani yake.
juisi ya karoti
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Karoti inamaana inatafunwa ikiwa mbichi au ya kwenye vyakula?%
ReplyDelete