MSHINDI wa Pili wa taji la Miss Utalii Mkoa wa
Dodoma mwaka 2011, Jackline Leshange amesema urembo ni pamoja na kujituma.
“Urembo bado naupenda na sitaacha urembo, napenda
hata mavazi ninayovaa yanitambulishe kuwa ni mrembo. Urembo si
sura nzuri tu lazima ujue kujituma na kujiweka nadhifu”
Jackline amesema aliingia kwenye urembo mwaka 2010
kutokana na kupenda fani hiyo na alikuwa akifuatilia warembo mbalimbali kwenye
Televisheni na hata kwenye majarida mbalimbali.
Mara ya kwanza kushiriki masuala a urembo ilikuwa ni
Juni 2011, alipojitosa kwenye mashindano ya Miss Dodoma ambapo
hakufanikiwa kuingia kumi bora.
“Sikukataa tamaa Oktoba mwaka 2011 nilishiriki mashindano ya
Miss Utalii Dodoma ambapo niliibuka mshindi wa pili”
Anasema kwa sasa licha ya kujishughulisha na kazi ndogondogo za kujiingizia kipato pia jioni anakwenda darasani ili kujiendeleza zaidi kielimu.
Jackline akiwa katika pozi |
Jackline Leshange |
Jackline Leshange akiwa amepozi |
No comments:
Post a Comment