Saturday, January 15, 2011
Uvaaji wa bangili na maana zake
BANGILI ni kitu kilichotengenezwa kwa lengo la kuvaliwa mkononi kama saa.
Bangili hutengenezwa kwa kutumia ngozi, kitambaa kigumu, plastiki, chuma, na wakati mwingine huwa na nakshi za aina mbalimbali.
Fasheni za bangili hutegemea na matakwa ya mavaaji kwani kuna wale ambao wanapenda kuvaa bangili zilizotengenezwa kwa vito vya thamani kama dhahabu na almasi na wengine wakipendelea kuvaa bangili zilizotengenezwa kutokana na vitu vya asili.
Bangili licha ya kuwa ni urembo wa mkononi, wakati mwingine hutumika kama alama hasa kwa wagonjwa wanapokuwa hospitalini na hutumika kama alama ya mgonjwa.
Hapa nchini kumekuwa na wasanii wa uchongaji ambao
hutengeneza bangili kwa kutumia magome ya miti na wakati mwingine kwa kutumia vifuu vya nazi.
Inaaminika kuwa bangili ambazo hutokana na vifuu vya nazi zimekuwa zikipendeza kuvaliwa kutokana na muonekano wake kwa ujumla na pia huuzwa kwa gharama nafuu ambapo wengi wanamudu kununua kuliko bangili zilizotengenezwa kwa vito vya thamani.
Uvaaji wa bangili pia unatakiwa kuzingatia rangi ya mvaaji, kama mtu ni mweusi anashauriwa kuvaa bangili zenye mng'ao ili kuweza kuwa na muonekano mzuri.
Ni vizuri kama tutazingatia mpangilio wa rangi katika uvaaji wa bangili na itapendeza kama uvaaji huo utazingatia na rangi ya nguo au viatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment