Tuesday, January 11, 2011

Ukitaka kunukia kama Rihanna unaweza


UNATAKA kunukia kama Rihana? Inawezekana hujui ananukiaje lakini siku si nyingi utajua binti huyu anayesumbua kwa namna yake ananukia vipi na wewe kama unataka kunukia kama yeye unaweza.
Binti huyu kutoka visiwa vya Barbados anajiandaa kuingiza sokoni manukato yake katika soko.
Hatua yake hiyo inamfanya na yeye kuingia katika msululu wa watu maarufu waliotengeneza manukato yao wakiwamo Britney Spears, Paris Hilton, na Faith Hill.
Manukato hayo mapya yatajulikana kama Reb’l Fleur yanatoa namna ya taarifa na kujenga thamani ya kauli ya binti huyo kwamba bibi yake alizoea kumuita ua lililoasi yaani rebel flower.
Akielezea manukato yake hayo mapya, RiRi anasema: "Nilitaka… kitu kama hiki kwamba ‘Rihanna alikuwa hapa.’ kitu laini, kitu bomba ambacho kinaacha kumbukumbu ya mvuto wa kimapenzi.
"Lakini si kweli kuwa kila mtu anataka kunukia vyema kiasi cha kufikiri kwamba "Rihanna alikuwa hapa,"alisema.

manukato ni biashara ambayo watu maarufu wengi hujiingiza kwani inaonekana hufanya vyema na faida huwa kali.
Watu wengi hununua manukato kwa sababu ya kumpenda mtu anayefanana na manukato hayo hata kama yananukiaje.
Reb'l Fleur itaingia madukani Februari mwaka huu.

No comments:

Post a Comment