Saturday, January 15, 2011

Umuhimu wa kuvaa hereni


Hereni ni mapambo yanayovaliwa masikioni.
Kuna aina nyingi za hereni katika tamaduni mbalimbali. Heleni hutengenezwa kwa kutumia madini ya thamani kama dhahabu au diamond.
Pia hutengenezwa kwa kutumia silver na almasi.
Lakini pia kwa kutumia ubao, mfupa au kioo, vifuu vya nazi na Kutokana na tamaduni mbalimbali, hereni zimekuwa zikivaliwa zaidi na wanawake, wanaume au jinsia zote mbili.
Mara nyingi uvaaji wa heleni unatakiwa kuzingatia aina ya nguo uliyovaa, hapo unatakiwa kucheza na rangi.
Mpangilio wako wa nguo na hereni hata na viatu utakufanya uonekane maridadi muda wote.
Wanawake wa kimasai wamekuwa wakijipamba kwa mapambo
ya shanga hali ambayo inawafanya wazidi kudumisha
utamaduni wao.
Pia hereni zilizotengenezwa kwa shanga zimekuwa zikiwavutia watu wengi kuvaa kutokana na nakshi yake

Uvaaji wa bangili na maana zake


BANGILI ni kitu kilichotengenezwa kwa lengo la kuvaliwa mkononi kama saa.
Bangili hutengenezwa kwa kutumia ngozi, kitambaa kigumu, plastiki, chuma, na wakati mwingine huwa na nakshi za aina mbalimbali.
Fasheni za bangili hutegemea na matakwa ya mavaaji kwani kuna wale ambao wanapenda kuvaa bangili zilizotengenezwa kwa vito vya thamani kama dhahabu na almasi na wengine wakipendelea kuvaa bangili zilizotengenezwa kutokana na vitu vya asili.
Bangili licha ya kuwa ni urembo wa mkononi, wakati mwingine hutumika kama alama hasa kwa wagonjwa wanapokuwa hospitalini na hutumika kama alama ya mgonjwa.
Hapa nchini kumekuwa na wasanii wa uchongaji ambao
hutengeneza bangili kwa kutumia magome ya miti na wakati mwingine kwa kutumia vifuu vya nazi.
Inaaminika kuwa bangili ambazo hutokana na vifuu vya nazi zimekuwa zikipendeza kuvaliwa kutokana na muonekano wake kwa ujumla na pia huuzwa kwa gharama nafuu ambapo wengi wanamudu kununua kuliko bangili zilizotengenezwa kwa vito vya thamani.
Uvaaji wa bangili pia unatakiwa kuzingatia rangi ya mvaaji, kama mtu ni mweusi anashauriwa kuvaa bangili zenye mng'ao ili kuweza kuwa na muonekano mzuri.
Ni vizuri kama tutazingatia mpangilio wa rangi katika uvaaji wa bangili na itapendeza kama uvaaji huo utazingatia na rangi ya nguo au viatu.

Tuesday, January 11, 2011

Uondoji wa nywele katika maeneo flani

MWANAMKE na hata mwanaume anatakiwa kuwa msafi na si usafi wa kubahatisha.Sehemu ya nywele za siri zimeelezwa kuwa ni sehemu ambapo ngozi yake ni yenye kuhitaji uangalifu mkubwa wakati wa kuziondoa.
Hizi si nywele za kawaida na haziwezi kuondolewa kiholela.Sehemu zinazokaa nywele hizo ni kwapani na maeneo ya faragha.
Kutokana na unyeti wa ngozi katika maeneo hayo watu wa fasheni wamekuwa wakisisitiza kuwa waangalifu zaidi wakati wa kuyafanyia usafi.
Maeneo haya yanatakiwa yaachwe bila mikwaruzo wakati wa marekebisho ya kiusafi yanapofanyika.
Pamoja na kwamba uondoaji wa nywele hizo hauna shida sana wengi wa watu wanapata shida sana baada ya kuondoa nywele husika.
Hii inatokana ama na vifaa vinavyotumika katika uondoaji au ule ukweli wa kawaida kwamba maeneo hayo yanahitaji kuangaliwa kwa makini.
Wengi wetu hunyoa maeneo hayo kwa kutumia nyembe na hii pia huleta matatizo ya kiufundi katika ngozi husika.
Wengine hufanya kitu kinachoitwa Waxing lakini kina maumivu makubwa kwa kuwa nywele huchomolewa kutoka katika kiini chake.
Hata hivyo ukifanikiwa kuondoa unakaa muda mrefu kabla ya kupata shida nyingine.
Ukifanya mwenyewe kazi hii utachanganyikiwa,manake unaweza kuzua uwasho wa kutia aibu kutokana na ngozi yako kukataa kusalimu amri kwakazi yako mwenyewe. Nywele zinazokua ndani huwa tatizo kubwa, njia hii huleta matatizo makubwa.
Unaweza kutumia utaalamu wa kisasa wa kuondoa moja kwa moja nywele hizo, lakini unahitaji fedha na hii ndio shida yenyewe, si kila mtu ana fedha za kufanya mambo hayo.
Uondoaji huu wa kudumu wa kutumia laser huchukua muda mwingi na ama hakika ni miezi kadhaa na hii hakuna mtu anayeitaka.
Bado wapo baadhi ya wanawake ambao wanafanya juhudi za kunyoa na pia kung'oa nywele hizo katika muda mbalimbali.
Lakini pia ukienda kwa wataalamu wanaweza kukupatia vitu vya kuondoa nywele hizo kwa raha kubwa.
Zipo pia kemikali za kuondoa nywele ambapo huzihitaji shauri ni kwenda kwa saluni -zinazohusika.

Ukitaka kunukia kama Rihanna unaweza


UNATAKA kunukia kama Rihana? Inawezekana hujui ananukiaje lakini siku si nyingi utajua binti huyu anayesumbua kwa namna yake ananukia vipi na wewe kama unataka kunukia kama yeye unaweza.
Binti huyu kutoka visiwa vya Barbados anajiandaa kuingiza sokoni manukato yake katika soko.
Hatua yake hiyo inamfanya na yeye kuingia katika msululu wa watu maarufu waliotengeneza manukato yao wakiwamo Britney Spears, Paris Hilton, na Faith Hill.
Manukato hayo mapya yatajulikana kama Reb’l Fleur yanatoa namna ya taarifa na kujenga thamani ya kauli ya binti huyo kwamba bibi yake alizoea kumuita ua lililoasi yaani rebel flower.
Akielezea manukato yake hayo mapya, RiRi anasema: "Nilitaka… kitu kama hiki kwamba ‘Rihanna alikuwa hapa.’ kitu laini, kitu bomba ambacho kinaacha kumbukumbu ya mvuto wa kimapenzi.
"Lakini si kweli kuwa kila mtu anataka kunukia vyema kiasi cha kufikiri kwamba "Rihanna alikuwa hapa,"alisema.

manukato ni biashara ambayo watu maarufu wengi hujiingiza kwani inaonekana hufanya vyema na faida huwa kali.
Watu wengi hununua manukato kwa sababu ya kumpenda mtu anayefanana na manukato hayo hata kama yananukiaje.
Reb'l Fleur itaingia madukani Februari mwaka huu.