Tuesday, January 19, 2010

Kwa nini unazeeka kabla ya wakati?


Mathalani hujafikia miaka ya 30 lakini unagundua uso wako ukiwa na mikunjo mingi usoni.Ikumbukwe kuwa, miaka ya 30 ni miaka katika ngozi yako pale machafuko ya hali ya hewa, viyoyozi, jua vinapoamua kuleta madhara kwenye ngozi yako.
Mbali na kuungua n jua, kuvuta sigara na kula vibaya makunyanzi huanza kutokea unapokaribia kuimaliza miaka ya 40.
Unaweza kuzuia hali hiyo kwa kutumia vitu vyenye mchanganyiko wa antioxidants ambavyo husaidia ngozi kuwa katika hali yake ya kawaida hasa kwa ngozi iliyoharibika kutokana na jua.
Dk.Dennis Gross, wa London Dermatologist anasema kuwa, kutumia vitu vyenye mchanganyiko wa antioxidants kama green tea, lycopene,co-enzyme Q 10, vitamin C na E vitaondoa makunyanzi yanayosababishwa na jua na yale yanayosababishwa na uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe.
Anasema unaweza kutumia cream utakazoshauriwa na daktari ambapo ngozi yako itaweza kurudi katika hali yake ya kawaida.
Wanasayansi wanasema kuwa, vatu wanaotaka kutunza ngozi zao kuacha kutumia sana sukari kwani sukari inachangia kuizeesha ngozi, sukari nyingi hufanya misuli ya protini katika ngozi kujikusanya pamoja na kusababisha kutoweka kwa mnyunyuruko unaotakiwa.
Tatizo la madoa na makovu usoni linaweza kuondolea kwa kutumia cream ambazo husaidia sana kuondoa bacteria na kukausha mafuta yaliyotanda usoni na kuacha ngozi yako ikiwa salama bila tatizo la madoa au chunusi.
Ili ngozi yako iwe nzuri unashauriwa kunywa maji mengi, maji ambayo husaidia kulainisha miili yetu.
Wakati mwingine makunyanzi husababishwa na tabia ya kula vyakula vilivyoungwa kwa chumvi nyingi.
Dk.Ibrahim Kaminsa wa Iringa anasema kuwa, kama una tabia ya kula vyakula vilivyoungwa kwa chumvi nyingi uso utakuwa na makunyanzi bila kujali umri wako.
Anasema mtu aliyeathirika na tatizo la makunyanzi anatakiwa kula mbogamboga na matunda kwa wingi na kunywa maji mengi ili kuondoa sumu ambayo imejengeka mwilini.

1 comment:

  1. najitahdi sana kula ma2nda na maji lkn bdo napenda sana chumvi. nifanyeje?

    ReplyDelete