Saturday, January 23, 2010

Jinsi asali inavyokabiliana na uzee


UTASHANGAA kwamba asali ndiyo hasa kitu kitamu ambacho kwa miaka mingi watu wamekuwa wakikifananisha na raha.
Ni kweli hata unapotaka kuleta longolongo za kimapenzi utasema asali wangu wa moyo au siyo?
Hii ni kutokana na ukweli kuwa asali inachukua nafasi ya pekee katika dunia ya mwanadamu.
Nafasi hii imo hata katika mambo mengi mpaka kwenye tiba, kwa kawaida asali ni dawa ya kukabiliana na vitu vingi pamoja na vimelea.
Pamoja na kuwa na antioxidants na inasaidia kukabiliana na uzee.
Uwepo wa kiwango kikubwa cha sukari katika asali kunaipatia uwezo wa dawa na ndiyo maana kwa miaka maelfu imesaidia watu kutibu vidonda.
Mtaalam mmoja wa ngozi mwenye makazi yake mjini New York City ambaye pia ni Daktari, Amy Wechsler anasema, hali ya kunyunyuruka iliyonayo asali na inayonasa inafanya kuwa kinga imara katika kidonda ambacho kinahitaji kisiingiwe na vimelea na kutoa mazingira ya kuponya, hivyo asali ni bomba kwa tiba.
Pamoja na tiba asali ni moisturize babu kubwa kwa ajili ya sura na mwili.
Asali ni dawa ya asili ambayo ina uwezo wa kukusanya naji kutoka ndani ya misuli hadi katika sehemu za juu za ngozi na hivyo kusaidia kuondoa mikunjo.
Mimi nakushauri jaribu moisturizing ambayo itaondoa ukavu wa ngozi yako na hata kuwasha au kutatarika.
Changanya vijiko vya mezani viwili vya asali na vijiko viwili vya mezani vya maziwa. Kisha pasha moto mchanganyiko huo, paka mchanganyiko huo katika uso wako na pumzika kwa dakika kama kumi.
Jioshe na maji ya uvuguvugu si ya moto.
Kama utataka kitu kama kosmetiki agiza Bee Ceuticals Organics’ Honey Thyme Hand and body lotion ambayo imetengenezwa kutokana na asali iliyochujwa .
Aina zote za asali zinasaidia sana kuondoa mikunjo ya uzeeni..

No comments:

Post a Comment