UVAAJI wa sketi fupi mara nyingi hutegemea na matakwa ya mavaaji,
kwani mara ntingi sketi fupi huishia juu ya magoti na huwa
na urefu usiozidi sentimita 10.
Vazi hili mara nyingi huvaliwa na wanawake wa nchi za
magharibi pia utamaduni huu umeenea sana hapa nchini ambapo wanawake na
wasichana wengi wamekuwa wakivaa aina hizi za nguo na kuonekana kuwa wanakiuka
maadili ya Kitanzania.
Wataalam wa mavazi wanasema, chimbuko la sketi fupi
ni huko London Uingereza katika miaka ya 1960 ambapo wanawake walikuwa wakivaa
nguo hizo katika michezo mbalimbali na wakati huo nguo fupi zilikuwa
zikijulikana kama nguo za michezo kwani zilikuwa zikivaliwa sana na wacheza
tenisi.
Wengi
wanaovaa aina hiyo ya nguo wamekuwa na sababu tofauti huku wengine wakidai kuwa
vazi hili hufanya wajiamini zaidi huku wengine wakidai kuwa sketi fupi hufanya
wajione bomba zaidi na kuonekana wanakwenda na wakati.
Sketi fupi zipo kwenye fasheni miaka nenda rudi japo
watu wengine wamekuwa wakivaa nguo hizo zikiwa fupi sana na kuleta mtafaruku
hata pale wanapokuwa wanapita barabarani.
Muhimu kuhakikisha kuwa unapochagua nguo ya kuvaa
angalia kama inaendana na mazingira na utamaduni wa Mtanzania na je nguo yake
umevaa mahali gani na kama unaona ni kero unapofanya hivyo basi unashauriwa
kuacha kufanya hivyo.
Wengi wanavaa sketi fupi na viatu virefu huku
wakitembea umbali mrefu hali inayosababisha kupoteza maana na heshima pia.
Vaa nguo kulingana na mazingira, kama una gari ni
sawa lakini kama unajua unakwenda kutumia usafiri wa daladala huku ukiwa umevaa
sketi fupi itakayokufanya ushindwe kukaa vizuri na hata kuinama hiyo si sawa
sawa.
No comments:
Post a Comment