Saturday, August 18, 2012

Utiaji rangi nywele

KUNA fasheni mpya imeingia ya kutia rangi nywele kwa lengo la kuleta utamu fulani katika mambo ya urimbwende. Ni sehemu ya kukipa kichwa chako mvuto mpya. Pamoja na nia nzuri hiyo, akili hutibuka sana kama ulichotaka sicho ulichokipata wakati ukitia rangi. Kwenye shughuli za kutia rangi nywele, wakati mwingine unapata rangi ambayo hukuitaka kwa hiyo ni vyema kuwa mwangalifu katika hilo. Utiaji rangi nywele hautakiwi kufanywa kw akubahatisha kuna mambo unatakiwa kuzingatia.Jambo la kwanza ni vyema ukaenda kwenye saluni yenye wataalamu ingawa ni rahisi kununua vifaa vya kujikoki mwenyewe. kama unataka kujitia mwenyewe la maana ni kuwa uwe na rangi moja lakini kama unataka kuwa na vitu vya kushaini hapa na pale, basi rangi za moja kwa moja kutoka dukania mb azo unaweza kujikoki hazifai, uwezekano wa kuharibu upo. Katika kujikoki mwenyewe ni vyema ukaachana na rangi nyekundu na ukajiwekea rangi ya kahawia. Na hata ukiwa saluni ni vyema kuongea na msusi wako kumwambia unataka nini na hakikisha amekuelewa. Rangi nzuri za nywele zinazotokana na rangi tamu.na ninashauri uweke rangi za asili kama : chocolate, caramels, blonds, auburns. lakini nakutahadharisha usizipende reangi ambazo hazina asili kama Ariel red, blues, jet black, pink, au aqua. nilikuasa tu kwenda kuonana na mpambaji wako ili mambo yaende vyema.

No comments:

Post a Comment