Thursday, May 5, 2011
MZIO wa ngozi au aleji
MZIO wa ngozi au aleji ni tatizo linaloweza kukupata kutokana na mwili wako kukataa kitu fulani, hutokana na sababu ikiwemo hewa na hata chakula tunachokula.
Kimsingi ni matatizo ya mlipuko wa mfumo wa kuhami mwili kwa kutumia au kuwa katika eneo ambalo linatibua mfumo wa mwili kwa kitu ambacho pengine wengine wala hawana tatizo nacho.
Kuna vitu ambavyo huibua mzio kama vumbi katika nyumba, mavi ya panya, manyoya ya wanyama na hewa yenye aina ya spiriti.
Mzio unaweza kukufanya uwe na ukrutu, mafua, pumu na hata kuvimba kwa mwili.
Wapo watu ambao hupata tatizo la ngozi, kuwashwa na hata kujaa.
Kuna mambo mengi sana ya kujifunza, lakini inaonekana kuwa tatizo hili husababishwa na mazingira na wakati mwingine ni tatizo la kurithi.
Katika dunia ambayo inatamba sana na teknolojia, tatizo la mzio lipo kubwa na hasa kemikali zinazotumika katika vyakula na hata urembo vinapotibua kemikali zinazotengeneza aleji katika mwili.
Kuna dalili tofauti za kuelezea aleji (mzio), lakini ni kitu ambacho ama hakika kinaweza kutibua uzuri na urembo wako na hata wakati mwingine kufanya mtu usiwe na raha kwa kutokea ukurutu au kuvimba kwa mwili.
Kuna aleji mabaya kama za kuumwa na mdudu ambapo wengine hubadilika na kuvimba mwili au eneo na hata presha ya damu kupungua kabisa.
Pia kuna tatizo la kuwa na aleji na dawa na chakula.
Ninachotaka kukuambia kwa leo ni haja ya kuwa mwangalifu katika vitu vingi na mara nyingi inafaa mtu kuwa mtulivu na kuachana na kile kitu ambacho kinakuletea tabu.
Kama huna uhakika nini kinakuletea mushkeri, ni vyema kutafuta viashiria vyake kwa kumuona mtaalam wa aleji.
Sehemu kubwa ya aleji haitibiki, san asana wataalam watakupatia dawa Fulani za kukusaidia kupunguza makali, lakini kwa vyovyote vile hali hii unaweza kuimudu mwenyewe kwa kuhakikisha unaondokana na ulaji au utumiaji wa vipodozi vya ovyo ovyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hilo tatizo nami ninalo. Mwanzoni nilijua ni tatizo la ngozi kumbe siyo ila ni hali ya hewa ya baadhi ya sehemu. Mfano nikienda Iringa ndiyo balaaaa! ngozi inawasha usiku kucha, vinyweleo vinasimama na kunichoma kama upupu!
ReplyDeleteTatizo hili lipo sana iringa tuambiwa alegi tunaacha vitu wanasema ni chanzo lkn tatizo aliishi
ReplyDeleteMi nina tatizo hili la allergy linanisumbua sana sijui nitumia dawa gani ili nipone maana nimeshatumia dawa nyingi lakini tatizo liko pale pale,naomba msaada wako
ReplyDelete