Friday, May 20, 2011

Mikoba inavyochangia urembo wa mwanamke



UNAPOKUWA katika safari zako utaona jinsi wanawake wanavyobeba mikoba ya aina mbalimbali.
Wakati mwingine mingi ya mikoba huwachukiza na wengine huwa kichekesho na ingawa wengine urembo wao huambatanishwa na kujipachika tu, vitu maarufu kama vipima joto kwa lugha ya kileo.
Ukiangalia hasa mijini hakuna kabati la nguo la mwanamke ambalo litakosa mikoba, tena ya aina mbalimbali. Kwa mwanamke kuwa na mkoba moja si sawasawa, kwa wale wanaokwenda na wakati kuwa na aina nyingi ya mikoba hii hutokana na ukweli kuwa mikoba hiyo ni sehemu ya mavazi na huambatana na si tu aina ya pamba iliyopigwa bali aina ya viatu vinavyompa kampani mwanamke.
Mwanamke ni kiumbe mrembo kabisa na jinsi anavyozidi kumechisha vitu anatakiwa kuwa mrembo na mwangalifu zaidi kwani anahitaji kujiweka katika kiwango kinachostahili katika kazi zake na uonekano wake.
“Mavazi yako unayovaa yanaweza kabisa kubadili maisha yako” anasema Trinny Woodall mmoja ya watu ambao wako makini kabisa na masuala ya unadhifu wa wanawake wa wanawake katika mitoko ya aina mbalimbali aliyeko Afrika Kusini.
Inakuwaje unapokuwa na vazi tofauti na mkoba wako wa kwapani na ndiyo huo mkoba mmoja pekee unaotumia kwa kwenda pati, kwenda safari. Kwenda kazini na kadhalika?
Hakika kwa mwanamke anayejijali, anatakiwa kuwa na mikoba ya aina tofauti kwa kuzingatia haja ya shughuli zake na pia mavazi yake.
Unachotakiwa siku zote si tu kuwa na mikoba mingio, najua unaweza kuwa na mikoba, unaoupenda lakini ni dhahiri kwamba mikoba hiyo unatakiwa lakini ni dhahiri kwamba mikoba huyo inatakiwa kuwa na mwendo sawa na mavazi yako ili kukupa kitu bomba kinachoweza kuwafanya wanaume wakutazame mara mbili mbili na wanawake wenzako wakuonee gere.
Nina sababu ya kukuambia hivyo lakini wapo wanawake waliojaza mikoba kibao lakini hawaitumii lakini hapo mwanzao waliponunua walijua kwamba ni mikoba bomba kabisa yenye mvuto wa kimapenzi hasa.
Kitu cha kwanza kuzuia ni ule ufujaji wa kununua mabegi yasiyotakiwa, yaani ni kuwa makini na haja yako mwenyewe na mapenzi yako na namna wewe mwenyewe ulivyo.
Ndiyo kusema mkoba lazima uzinagatie mwili wako, upenzi wa maisha yako.
Watengeneza mikoba wengi wanaonya kabisa uchukuaji wa mikoba kwa kuiona bomba kumbe hairandani na wewe unayeibeba.
Mathalani wewe ni mrefu na mwembamba, mikoba yenye mduara ni mizuri lakini kama wewe ni mfupi uliyejazia kiasi chake mkoba unaofanana na ule wa mstatili, mrefu kiasi na mweroro ni kiboko yake.
Ningekushauri kabla hujanunua na kuvaa mikoba hiyo hebu jitazame kwanza katika kioo kwani ni lazima ukubali kwamba uko safi ndiyo uchangamke na mtaa, unapokuwa umejiangalia kwenye kioo utapata namna bora namna bora ya muonekano kama vile unavyojaribu nguo kwenye kioo.
Mikoba myembamba iliyobana hasa huonekana kuwa bomba kwao kama wewe ni mwembamba pia na kama unataka mtu kujisahau kwa namna yake katika mwili wako, lakini haitakusaidia sana kwa matiti yako ni madogo na mikono yako haijajaza inavyostahili.
Halafu tazama sana mikanda ya mikoba ina maana kubwa zaidi ni ndiyo maana ni vyema ikazingatiwa urefu wake katika mabega yako kwani kwa vyovyote vile urefu wake utakavyobeba mkoba wako ina kitu inakifanya katika mwisho wake.
Kwa hiyo kama hutaki mushkeri katika maeneo ya juu ya mapaja usitwae mkoba unaofika pale. Wengi wa wanawake hutokea bomba kama mkoba haufiki katika kiuno au juu yake kidogo, kwani kuketi hapo chini inakuwa mambo si poa katikati ya mwili kwa upande wa juu ndiyo haswaa sawa.
Ni muhimu ukitambua ya kwamba ukubwa wa mkoba wako unaambatana na wewe unaeleweka.
Lakini niseme moja tu mikoba mingi huwa bomba kama haijazwi vitu lakini mathalani kama una simu, shajara na vikorombwezo vya uzuri mkoba mwembamba haufai kwani utatuna na kuchukiza.
Mbunifu wa FUNEKA, Tasleem Bulbulia anasema kwamba mtu wa aina hii kwa kulingana na kazi zake na stahili zake za maisha mikoba mipana ni saizi yake. Ndiyo kusema kazi na stahili yako ndiyo pia itazingatia aina ya mkoba unaotakiwa kuwa nao.
Ulishatambua personaliti yako na aina yako ya maisha ni vyema ukatambua ukweli kuwa chagua kulingana na wewe na si yule kwani kivigezo haiwezekani na kwa maisha pia haiwezekani.
mwisho

Urembo wa macho utakufanya uonekane bomba zaidi


Eyeshadows ni urembo ambao hutumiwa juu na chini ya kope. Njia hii husaidia kuongeza kina na mwelekeo wa macho ya watu.
Watu wanapenda kutumia aina hii ya urembo ili kuweza kuimarisha muonekano wao.
Kama wewe ni mweusi jaribu kutumia rangi angavu ili kuimarisha muonekano wako ukitumia rangi za giza zitakufanya uonekane vibaya.
Ni muhimu kuhakikisha kuwa unakuwa makini ili kuweza kuweka macho yako katika hali bora zaidi ya kupendeza.
Wakati mwingine Eyeshadows hufanya macho kuonekana makubwa au madogo. Lakini cha muhimu kuzingatia je rangi unayopaka inaendana na macho yako au ngozi yako.
Unatakiwa kupaka rangi kwa ustadi mkubwa huku ukiweka mkolozo katika kona za macho yako.
Ni vizuri kama utatumia eyeshadow ya penseli kwani huwa rahisi kuitumia na inapatikana kwa urahisi madukani.Kuna rangi za aina nyingi ambazo hupendeza wapakaji, rangi hizo ni pamoja na pink plum, matumbawe na shaba, bluu na kijani
pamoja na fedha, dhahabu na nyingine nyingi.
Rangi hizi hutofautiana kulingana na mng'ao wake kwani kuwa zenye mng'ao mkubwa na zile zilizofifia.Njia ya kawaida ya kupaka eyeshadow ni kutoka ndani ya kona
ya jicho na nje na zaidi.Rangi kama Gray, violet, zambarau na bluu huwapendeza sana
watu wa rangi ya maji ya kunde na kusaidia kung'arisha macho yao.

Thursday, May 5, 2011

MZIO wa ngozi au aleji


MZIO wa ngozi au aleji ni tatizo linaloweza kukupata kutokana na mwili wako kukataa kitu fulani, hutokana na sababu ikiwemo hewa na hata chakula tunachokula.
Kimsingi ni matatizo ya mlipuko wa mfumo wa kuhami mwili kwa kutumia au kuwa katika eneo ambalo linatibua mfumo wa mwili kwa kitu ambacho pengine wengine wala hawana tatizo nacho.
Kuna vitu ambavyo huibua mzio kama vumbi katika nyumba, mavi ya panya, manyoya ya wanyama na hewa yenye aina ya spiriti.
Mzio unaweza kukufanya uwe na ukrutu, mafua, pumu na hata kuvimba kwa mwili.
Wapo watu ambao hupata tatizo la ngozi, kuwashwa na hata kujaa.
Kuna mambo mengi sana ya kujifunza, lakini inaonekana kuwa tatizo hili husababishwa na mazingira na wakati mwingine ni tatizo la kurithi.
Katika dunia ambayo inatamba sana na teknolojia, tatizo la mzio lipo kubwa na hasa kemikali zinazotumika katika vyakula na hata urembo vinapotibua kemikali zinazotengeneza aleji katika mwili.
Kuna dalili tofauti za kuelezea aleji (mzio), lakini ni kitu ambacho ama hakika kinaweza kutibua uzuri na urembo wako na hata wakati mwingine kufanya mtu usiwe na raha kwa kutokea ukurutu au kuvimba kwa mwili.
Kuna aleji mabaya kama za kuumwa na mdudu ambapo wengine hubadilika na kuvimba mwili au eneo na hata presha ya damu kupungua kabisa.
Pia kuna tatizo la kuwa na aleji na dawa na chakula.
Ninachotaka kukuambia kwa leo ni haja ya kuwa mwangalifu katika vitu vingi na mara nyingi inafaa mtu kuwa mtulivu na kuachana na kile kitu ambacho kinakuletea tabu.
Kama huna uhakika nini kinakuletea mushkeri, ni vyema kutafuta viashiria vyake kwa kumuona mtaalam wa aleji.
Sehemu kubwa ya aleji haitibiki, san asana wataalam watakupatia dawa Fulani za kukusaidia kupunguza makali, lakini kwa vyovyote vile hali hii unaweza kuimudu mwenyewe kwa kuhakikisha unaondokana na ulaji au utumiaji wa vipodozi vya ovyo ovyo.

Tai iendane na umbo lako


Kuna mambo mengi ya kufanya ili tuwe watu wa kuvutia kila wakati.Mpangilio wa mavazi hufanya mtu kuonekana maridadi.
Kama wewe ni mvaaji wa tai unapovaa unazingatia mambo yapi? Na je unafunga tai yako kwa namna inayokubalika?
Wengine huwa hawafahamu jinsi ya kufunga tai na hivyo kuleta mushkeri wakati wa kuvaa tai na kusababisha tai kukaa upande. Unapoamua kuvaa tai na shati ambalo halijanyooshwa ambalo linakuwa kwenye mikunjo au kuvaa tai na ndala unakuwa umeua maananzima na kulivunjia heshima vazi hili.
Tai ni vazi lawatu walio maridadi kama huwezi kuwa maridadi basi vazi hili halikufai kabisa.
Unapovaa taa unatakiwa kuzingatia aina ya umbo lako kama wewe ni mnene vaa tai inayoendana na mtu mnene na kama wewe ni mwembamba basi vaa tai inayoendana na mtu mwembamba.
Kuna wengine huvaa tai zinazofika magotini na kuwa kichekesho anapopita mtaani
Tai ni vazi ambalo huongeza heshima na hadhi ya mvaaji cha muhimu ni jinsi gani unavaa tai yako na ikiwezekana jaribu kumechisha tai na suruali kwa vile ili tai upendeze ni laima iendane na nguo unayovaa.
Ni vyema ukahakikisha kuwa unakuwa na tai zenye rangi tofauti ambazo zitaendana na nguo unazovaa.
mwisho