Tuesday, April 26, 2011
Jinsi ya kuwa bi harusi mrembo
KITU cha muhimu ni kuhakikisha unakuwa makini kwa kila unachokifanya hasa katika suala la kuweka mwili wako sawa.
Tabia ya kutaka kupunguza mwili kupita kiasi kwa kipindi kifupi inaweza kukuletea matatizo kiafya. Usijaribu kupunguza mwili katika kipindi cha miezi miwili kabla ya siku yenyewe ya harusi, kitu cha msingi ni kuanza kupanga mapema kupunguza uzito wako taratibu.
Ndiyo kusema kama unataka kuwa katika shepu unayoitaka wakati wa harusi yako basi jambo la kuzingatia ni kujiweka fiti.
Hatushtukizi harusi. Harusi zinapangwa kwa hiyo muda mwingine wa kuangalia unataka kutoka na shepu gani wakati wa harusi.
Pia usijaribu kupanga kitu kisichotekelezeka.
Wanawake wengi hutaka kujiweka katika umbile la kuwa wembamba zaidi ili kujaa katika gauni analotaka yaani kuwa kipotabo , kuwa mkweli kwako mwenyewe huwezi kuleta vurumai katika mwili wako ili tu uwe mwembamba, yaani usifikirie hata mara moja kwamba unaweza kujibadilisha unavyofikiria eti kwa kuwa unataka kuolewa.
Lakini la maana ni kuwa kama unataka kuonekana tofauti sana kiasi cha mwamba hata huyu mchumba asikutambue na marafiki wakushangae?
Kwa kawaida waolewaji huwa na muda mfupi sana na msululu wa mahitaji ili wapendeze, na kutokana na hili wengi wetu hujaribu njia za mkato nyingi zikiwa hazifai kujiweka katika mwili wa wembamba ambao tunadhani kuwa unapendeza.
Tafadhali usijaribu hata kidogo kuanza diet ambayo inatoa matokeo ya haraka huku ukiwa umetumia nguvu kidogo.
Pia achana na mpango wa kula vidonge vya kuzuia mlo au kula vidonge ambavyo vinakubana au kula aina moja ya supu kwa wiki nzima yaani ninachozungumzia ni achana na kubania mlo wako ukawa si ule wa kuleta virutubisho vyote.
Kuhusu vipodozi
Kuwa mwangalifu kuhakikisha kwamba hakuna kitu hakuna kitu kinachoharibu utaratibu wako wa kupendeza hasa ile rangi ya ngozi yako.
Usipende kutumia vitu vipya vikakututumua ukashindwa kuelewa hivi uso au mwili huu una matatizo gani? Kwani majaribuo humpeleka mtu katika balaa asilolijua.
La maana sana ni kutumia vipodozi maalum vya kulainisha na kuitonusha ngozi kwa jamu ili kuiwezesha kuwa na mafuta kiasi yanayoweza kutulia wakati wa kutengeneza vitu yaani make- up siku ya harusi, kitu ambacho mara nyingi pia husaidia ukiachia vipodozi hivyo maalum kuweka ngozi katika hali iliyotulia ni mazoezi, mara nyingi mazoezi huleta rangi maridhawa ya ngozi na kwa kuwa upo katika nchi yenye joto basi sehemu za wazi zifanywe zile mwanga wa kutosha kukamilisha rangi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment