Thursday, March 3, 2011

Pendeza kwa kuvaa nguo ndefu



WANAWAKE wamekuwa na uchaguzi wa aina gani ya nguo ambayo inatakiwa kuvaliwa katika mtoko wa usiku.
Kuna wale ambao hupendelea kuvaa nguo za kung'aa na wale ambao hupendelea nguo za kawaida lakini zenye mitindo bora zaidi.
Uchaguzi wa nguo inayotakiwa kuvaliwa unatakiwa kuzingatia mambo mengi ikiwemo kuvaa kulingana na tukio husika, kama ni pati ya kawaida au ni kwa ajili ya sherehe fulani.
Uvaaji wako unatakiwa kuzingatia rangi ya nguo na rangi ya mwili wako.
Kama wewe ni mweusi hutakiwi kuvaa nguo nyeusi kwani haitakupendeza, unashauriwa kuvaa nguo za rangi nyeupe,nyekundu, gold, bluu au njano.
Na kama wewe ni mweupe nguo ya rangi nyeusi au rangi nyingine itakupendeza kulingana na rangi ya ngozi yako.
Nguo ndefu ni nzuri zaidi kama zitavaliwa kwa kiatu kirefu na kubeba mkoba mdogo.
Cha kuzingatia ni kuhakikisha kuwa nguo hiyo haikuletei tabu wakati wa kutembea kwani nguo ikiwa ndefu sana husababisha mvaaji kuishikilia na kuonekana wakati mingine kama kituko.
Vaa nguo kulingana na umbo na hata urefu wako, nguo za wazi na ndefu hupendeza sana kama zitavaliwa na mkufu au ushanga shingoni.
Jambo la muhimu ni kuhakikisha kuwa, unakuwa na nguo maalum ya kutokea na unatunza vizuri nguo zako kwani hilo litakusaidia kuongeza umaridadi wako na kujiamini zaidi.

1 comment:

  1. hapa umenipendeza maana maguni na skrti ndefu ndio mmavazi yangu. Safi sana

    ReplyDelete