Thursday, March 3, 2011
'Singlet' kivazi kinachohitaji usafi zaidi
KUNA wanaume nawasifu kwa kuzingatia usafi wa mavazi yao na hata muonekano wao licha ya kuwa wengine wameamua kuliweka kando kidogo suala hili.
Unapokuwa mtanashati unakuwa na kila sababu ya kujiamini.
Usafi wa mwili umekuwa ukisisitizwa sana kutokana na ukweli kuwa usafi ni afya na muhimu kwa kila moja kuwa na tabia ya kuwa msafi wakati wote.
Usafi ni pamoja na kuoga na kutakata vizuri, kutorudia kuvaa nguo ambayo imevaliwa na inanuka jasho na hata kunyoosha nguo vizuri kabla ya kuvaliwa.
Singlet pamoja na kuvaliwa ndani ya shati pia zimekuwa zikivaliwa zaidi na wanamichezo ikiwemo mieleka na wale wa mbio ndefu.
Wengi wanavaa singlet ndani ya nguo nyingie iwe kwa wanaume au kwa wanawake
"Unaponunua singlet unazingatia zaidi ubora na kitambaa kilichotumika kutengeneza nguo hizo kama ni pamba au aina nyingine ya kitambaa, lakini wanaume wengi wanapendelea pamba zaidi" anasema mkazi mmoja wa Jijini Dar es salaam.
Uvaaji wa singlet unatakiwa kuzingatia zaidi usafi kutokana na ukweli kuwa nguo hiyo imekuwa ikivaliwa sana na wakati mwingine huathiriwa zaidi na jasho linalotoka mwilini.
Pia ni vizuri kuhakikisha usafi wa kwapa ili kuweza kuhakikisha kuwa,singlet yako inakuwa katika hali ya usafi muda wote na ili isiwe tabu kwako kuinua mkono kwani wengi wanaficha kwapa zao kutokana na uchafu kitu ambacho si kizuri.
Uvaaji huo unazingatia sana rangi kutokana na matakwa ya mvaaji ila wengi wanapendelea rangi nyeupe.
Nguo yoyote ya rangi nyeupe ni nzuri na inapendeza ikivaliwa kwani rangi nyeupe pia huonyesha kipimo cha usafi wako.
Kwa kina dada wanaopenda kuvaa singlet nao wanatakiwa kuhakikisha kuwa kwapa zao zinakuwa safi ili kuweza kuwa huru zaidi.
Jinsi ya kuchagua gauni bomba la harusi
GAUNI bora la harusi ni ndoto ya kila mwanamke anayetaka kuolewa. Kuwa na nguo ya maana siku ya harusi nikitu kizuri ambacho huongeza furaha na kujiamini.
Lakini kabla ya kufanya shoping kwa ajili ya gauni la harusi ni muhimu ukazingatia umbo la bi harusi,rangi yake na mahali ambapo utapata nguo hiyo.
Uchaguzi mzuri unatakiwa kuengana na gharama ya nguo hiyo ambayo hata bi harurusi akivaa ataonekana wa kisasa, anavutia, anajiamini na aliyependeza hilo litamuongezea utulivu.
Nguo nyingi za harusi zimekuwa na gharama kubwa, nunua nguo kulingana na bajeti yako ili usiweze kuharibu mipango mingine.
Kumekuwa na aina mbalimbali za nguo za harusi kulingana na matakwa ya mvaaji na uwezo aliokuwa nao.
Cha muhimu ni kuzingatia nguo hiyo inakuwa bora zaidi na kumpendezesha mvaaji.
Pendeza kwa kuvaa nguo ndefu
WANAWAKE wamekuwa na uchaguzi wa aina gani ya nguo ambayo inatakiwa kuvaliwa katika mtoko wa usiku.
Kuna wale ambao hupendelea kuvaa nguo za kung'aa na wale ambao hupendelea nguo za kawaida lakini zenye mitindo bora zaidi.
Uchaguzi wa nguo inayotakiwa kuvaliwa unatakiwa kuzingatia mambo mengi ikiwemo kuvaa kulingana na tukio husika, kama ni pati ya kawaida au ni kwa ajili ya sherehe fulani.
Uvaaji wako unatakiwa kuzingatia rangi ya nguo na rangi ya mwili wako.
Kama wewe ni mweusi hutakiwi kuvaa nguo nyeusi kwani haitakupendeza, unashauriwa kuvaa nguo za rangi nyeupe,nyekundu, gold, bluu au njano.
Na kama wewe ni mweupe nguo ya rangi nyeusi au rangi nyingine itakupendeza kulingana na rangi ya ngozi yako.
Nguo ndefu ni nzuri zaidi kama zitavaliwa kwa kiatu kirefu na kubeba mkoba mdogo.
Cha kuzingatia ni kuhakikisha kuwa nguo hiyo haikuletei tabu wakati wa kutembea kwani nguo ikiwa ndefu sana husababisha mvaaji kuishikilia na kuonekana wakati mingine kama kituko.
Vaa nguo kulingana na umbo na hata urefu wako, nguo za wazi na ndefu hupendeza sana kama zitavaliwa na mkufu au ushanga shingoni.
Jambo la muhimu ni kuhakikisha kuwa, unakuwa na nguo maalum ya kutokea na unatunza vizuri nguo zako kwani hilo litakusaidia kuongeza umaridadi wako na kujiamini zaidi.
Subscribe to:
Posts (Atom)