Monday, December 27, 2010
Jinsi ya kurembesha macho
UNAWEZA kuweka macho yako katika hali ya kupendezanakuhakikisha yanakuwa na mvuto wa kipekee.
Kama unataka kufanya macho yako yaonekane meusi pakawanja kulingana na aina ya macho yako bila kujali kama kamauna macho makubwa au madogo.
Kama una macho madogo unatakiwa kuchora mstari pembenibaada ya kupaka wanja, hii husaidia watu wenye machomadogo kuonekana kuwa wana macho makubwa.
Anzia kupaka kwenye kona za macho wakati mwingineunatakiwa kushikiria jicho wakati wa kupaka wanja.
Watu wenye macho makubwa wanashauriwa kupaka wanjawenye mistari myembamba ambayo inanakshiwa na urembo ndani yake.
Unatakiwa kuhakikisha kuwa, wanja unaotumia hauna madharakwa macho yako kwani kuna aina nyingine ya wanja mtuanapotumia macho huwasha au hutoa machozi.
Pia usipende kutumia kila aina ya wanja kwa ajili ya usalamawa macho yako, unaweza kutumia bidhaa za kampuni moja tu nasi kubadilibadili kila wakati.
Wakati wa kupaka wanja fuata mstari na rudi hivyo kwa marambili nyingine hadi kuhakikisha kuwa wanja umekolea vizuri.
Pia unaweza kutumia pamba kwa ajili ya kupaka shedo juu yamacho kwa rangi ambayo umechagua.
Hakikisha kuwa, unapokuwa unatengeneza macho yakounatakiwa ukae kwenye kioo na uwe umetulia ili kuwezakutengeneza macho yako vizuri huku ukitumia kioo ambacho kitakuonyesha vizuri.
Ni vizuri kuchagua tangi za kupaka na ni heri pia kama rangiunazochagua zinaendana na nguo au kiatu utakachovaa.Ni vizuri kupaka rangi ya kung'aa wakati wa usiku na pia rangizilizotulia wakati wa machana.
Unaweza kupaka mascara kwa kutumia brash kwa ajili ya kurembesha kope zako ili ziweze kuinuka na kuleta mvuto katika macho yako.
Thursday, December 16, 2010
Siri ya papai katika urembo wako
Tunda la kitropiki la papai lina vitamini C na E likiwa na siri
kubwa ya urembo na hutumika kutengeneza facial za aina mbalimbali.
Papai limekuwa likitumiwa kama njoia boya ya kutunza uso wako na
kumfanya mtu kuwa na ngozi ya asili.
Bidhaa ambazo zimekuwa zikitengenezwa kwa kutumia tunda la papai ni
pamoja na sabuni, lotion, tona, moisturiza, facial peels na nyingine
nyingi.
Ukitumia facial mask ya papai utakuwa na sura nzuri ya asili na kukupa
uonekanaji mzuri wa uso wako.
Facial mask hii huweza hutumika kwa watu wa umri na aina yoyote ya ngozi.
Facial mask ya papai ina nguvu ya kung’arisha uso wako.
Pia inasaidia ngozi ambayo imeshaanza kupatwa na makunyanzi kutokana
na umri kuonekana ya kuvutia kwani pia imekuwa ikiondoa chunusi na
makunyanzi pia.
Ni rahisi kutengeneza facial mask ya papai na ukitumia itakusaidia
katika kukabiliana na ngozi iliyoanza kuchoka, kung’arisha ngozi
Kuna na njia nzuri za kuhakikisha kuwa, tunakuwa na nyuso nzuri zenye
kupendeza na kuvutia ikiwemo kutumia vitu vya asili pamoja na matunda
ya aina mbalim ambayo husaidia zaidi katika kuimarisha ngozi .
Mask ya mchanganyiko wa papai yai na yai ni nzuri katika kuhakikisha
kuwa unakuwa na ngozi nzuri na nyororo.
Njia hii pia husaidia hata wale wenye nyuso za mafuta ambao wamekuwa
wakisumbuliwa na chunusi mara kwa mara kwa kufanya ngozi kuwa kavu.
Unaweza kutengeneza aina hii ya mask kwa kufanya yafuatayo:-
Chukua papai likate kasha toa mbegu na kasha lisage kwa kutumia blenda
ay kuondaponda kwenye kibakuli kwa kutumia kitukama mchi mdogo wa
kinu.
Kisha weka mchanganyiko huo kwenye chombo ulichokichagua kama kikombe au bakuli.
Vunja yai na koroga kuhakikisha kuwa mchanganyiko huo umechanganyika vizuri.
Safisha uso wako kwa kutumia cleanser au maji ya vuguvugu na uondoe
uchafu wote ulioganda usoni.
Kisha paka mask kuzunguka uso wako, na unapopaka hakikisha kuwa,
mchanganyiko huo haugusi macho yako.
Osha uso wako baada ya dakika 15 kwa kutumia maji ya vuguvugu. Jifute
kwa kutumia taulo safi
Unaweza kupaka losheni, tona au moisturiza.
Husaidia kutunza ngozi na kuondoa vipele na uchafu ulioganda usoni.
Hii ni njia rahisi ya kutengeneza uso isiyo na gharama.
Wewe ni mwanamke unayejiamini kwa nini usipendeze?
MWANAMKE hulka yake ni Kupendeza. kupendeza kwa mwanamke humfanya
avutie na kuonekana wa kisasa zaidi.Wanawake wengi wamekuwa
wakijisahau na kupoteza ule uzuri wa muonekano wao.
Wakati mwingine kujipamba au kujiremba ni hulka ya mtu na kuna watu
wamezaliwa wakiwa warembo bila hata kujiremba huonekana kuvutia wakati
wote.
Lakini kuna wanawake ambao licha ya kuwa wazuri wakiongeza na
kujiremba huonekana wenye mvuto zaidi.
Wanawake ambao wana uzuri wa asili hasa wale ambao wametunza ngozi zao
nyeusi za asili hupendeza sana kama watajipamba kwa vitu vya asili
kama kuvaa hereni, mikufu au bangili zilizotengenezwa kwa vitu vya
asili kama vifuu vya nazi, magome ya miti au kutengenezwa kwa kutumia
shanga.
Wakati huu wanawake wenye uwezo kifedha wamekuwa wakitumia fedha zao
kujipamba kwa mapambo ya gharama kubwa kama kuvaa mikufu na saa zenye
za dhahabu na hata madini mengine yenye thamani kubwa kama almasi.
Uvaaji wa mikufu, hereni, bangili ni mambo ambayo mwanamke anatakiwa
kuyazingatia ili kuweza kuongeza urembo wake.
Wengi wetu tumekuwa tukisahau kutumia vitu hivi katika mavazi yetu.
Vitu hivi vimekuwa vikisaidia sana kuboresha maisha yetu ya urembo
kutokana na kuwa unapovaa hereni, mkufu au bangili iliyofanana na nguo
uliyovaa hii itasaidia uonekana nadhifu zaidi kuliko unavyofikiri.
Mwanamke ambaye amekuwa akipangilia mavazi yake amekuwa akionekana
nadhifu kuliko yule ambaye amekuwa akiweka mwilini kila aina ya rangi
na kufanya muonekano wake usiwe mzuri.
Kuna mapoambo mengi siku hizi tena kwa gharama nafuu sana cha
kuzingatia ni kucheza na rangi, ukijua namna ya kupangilia rangi za
mavazi yako na mapambo yako utakuwa umefanikiwa sana katika
kufanikisha muonekano wako uwe mzuri.
Kitu kingine cha kuzingatia ni kuwa, unapoamua kupangilia rangi za
mavazi yako hakikisha kuwa mvazi hayo hayawi kwenye rangi za kung’aa
sana hasa pindi mavazi hayo ni ya kuvaliwa wakati wa mchana.
Mwisho
Uvaaji soksi na utunzaji wake
Soksi ni vazi ambalo huvaliwa miguuni.
Miguu ni mmoja kati ya viungo ambavyo vinatoa jasho mwilini, huzalisha
zaidi jasho kila siku.
Soksi husaidia kuhakikisha kuwa unyevunyevu unahifadhiwa katika eneo
linalotakiwa na baadaye kutolewa nje kwa njia ya hewa.
Katika mazingira ya baridi soksi husaidia kupunguza uhakika wa kupata baridi.
Soksi hutengenezwa kwa pamba, sufu, nailon na aina nyingine za nyuzi.
Katika kuongeza kiasi cha ulaini, malighafi nyingine ambazo
hutengenezaa soksi hutumika.
Kuna aina mbalimbali za rangi za soksi ambazo hutengenezwa na pia
kuvaliwa kila siku.
Wengine huvaa soksi ili kuimarisha muonekano wao
Soksi za rangi ya kung’aa mara nyingi huwa ni sehemu ya vazi katika
michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutofautisha wachezaji pale
ambapo miguu pekee ndiyo inaonekana.
Mitindo ya soksi huvaliwa kulingana na matakwa ya mvaaji.
Wengine hupenda kuvaa soksi na viatu vya wazi huku wengine wakivaa na
viatu vilivyozibwa.
Soksi ndefu nyeupe huvaliwa kama sehemu ya sare za shule.
Wanamichezo wamekuwa wakitumia soksi kama sehemu ya vazi. Soksi hizi
huwa ndefu na mara nyingi huwa ni nzito.
Makundi mbalimbali yamekuwa yakivaa soksi hata wanawake ambao huvaa
soksi katika kuhakikisha wanakuwa na muonekano mzuri na mavazi
waliyovaa.
Kuna zile soksi nyepesi sana hizi mara nyingi huvaliwa na wanawake.
Soksi ni vazi ambalo huvaliwa kila siku hasa kwa wanaume ni vizuri
kama soksi zinakuwa safi muda wote ili kuondoa ile harufu mbaya ambayo
imekuwa kero kwa watu wengi.
Ni vizuri kama soksi zikafuliwa na kuanikwa juani na kukauka vizuri
kabla ya kuvaliwa. Pia wavaaji wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakuwa na
jozi nyingi za soksi ili kuweza kupunguza ugumu wa kuzitunza.
mwisho
Umaridadi wa wanaume uko mikononi mwa wanawake
LEO nataka tukumbushane kitu kimoja nacho ni jinsi ya kumfanya mwenzi
wako aonekane maridadi wakati wote. Hapa nazungumzia wale walio katika
mahusiano ya kudumu ambao wanaishi pamoja.
“Nikiamka asubuhi jambo la kwanza ni kumuandalia mume wangu maji ya
kuoga, nahakikisha nguo zake zimepigwa pasi, viatu vimeng’arishwa,
soksi ziko safi, na akivaa lazima nimfunge tai, na nguo za kazini mimi
ndiye nachagua siku hiyo avae nguo gani” anasema Mama mmoja mkazi wa
Kimara Jijini Dar es Salaam.
Sikiliza na hii “ Mimi mume wangu huwa anaandaa nguo zake mwenyewe
anafua, apige pasi au asipige shauri yake, aoge asioge atajijua, huo
muda sina kabisa siku hizi” anasema mwanamke mmoja Mkazi wa Buguruni
Jijini Dar es Salaam.
Siku zote tumekuwa tukisisitiza urembo kwa wanawake na utanashati kwa wanaume.
Mmoja ya jukumu la mwanamke ni kuhakikisha kuwa, mwanaume wake anakuwa
maridadi na mwenye kuvutia. Jaribu kuangalia ni nguo za aina gani mume
akivaa zinampendeza na hapo unaweza kumchagulia shati na suruali
ambazo rangi zake zinaendana na hata akivaa zitamfanya apendeze.
Pia suala zima la kufua na kupiga pasi vizuri ni moja ya njia ya
kuonyesha kuwa unamjali na unamjengea namna ya kujiamini
zaidi.Utunzaji wa soksi ikiwemo ufuaji wa nguo za ndani ni jambo
linalosisitizwa sana kwani wanaume wengi wanaonekana kutojali sana
vitu hivyo ama kutokana na muda au kwa kukosa ushirikiano wa wenzi wao
katika kutunza na kufanyia usafi aina hizo za nguo.
Jamani mwanaume akiwa maridadi au mtanashati huwa anamvutia kila mtu
na zaidi sifa zinakwenda kwa mkewe ambaye anaaminika kuwa ni chanzo
cha mwanaume kuwa msafi.
Jenga mazingira ya kujali usafi wa nguo za mwenzi wako ili kuhakikisha
kuwa kila kitu kinakwenda sawa.
Pia kuna wanawake wengi ambao ni wajuzi wa kufunga tai, kama hilo bado
hulifahamu tafuta mtu ambaye atakufundisha namna bora ya kufunga tai
ili uweze kumpendezesha mume wako.
Kama unapita dukani au sehemu zinakouzwa nguo si vibaya kama unaona
kuna nguo inaweza kumfaa mwenzi wako mna ukahakikisha kuwa akivaa
anapendeza usisite kununua kwani itakuwa ni zawadi nzuri sana kwake.
Jaribu kuwa na tabia ya kumvika mwenzi wako, si kuacha kila kitu
afanye yeye kuanzia kufua, kupiga pasi na hata kung’arisha viatu.
Ni vizuri kama utaamua kuhakikisha kuwa, unamuaandaa mume wako kabla
ya kwenda kazini kisha na wewe kuendelea na shughuli zako.Hilo
litaongeza upendo na amani kwenye nyumba.
Wanawake wengi wamejisahau sana na kuacha wanaume wafanye kila kitu
wenyewe jambo ambalo husababisha wanaume wengine watoke nyumbani bila
kupiga pasi au kusahau kuchana nywele.
Jirekebishe kama una tabia za kutojali usafi wa mwenza wako,
utanashati ni muhimu kwa wanaume pia usiishie kwa wanawake kujipenda
na kujiremba kila wakati huku wakisahau waume zao
Wednesday, December 15, 2010
Onyoaji ndevu wenye raha
MOJA ya matatizo makubwa kwa wanaume ni unyoaji wa ndevu, kitu ambacho
wakati mwingine huwakera wahusika na wao kujiona kama ni wafungwa.
Pengine hili ndilo linalowasumbua watu mpaka wanajisikia vibaya
kuzaliwa wanaume, halafu hataki ndevu na ndevu zinakuja kama
zimepaliliwa vile. Lakini haya ni maamuzi tu ya kimsingi kwani naamini
unyoaji ndevu unaweza kuwa laini na wenye raha kubwa kama utafuata
haya ambayo nataka kukueleza.
Nafahamu mwanamke wako hapendi ndevu anapenda kuwa na kidevu laini
chenye raha yake kukigusa ingawa najua vile vile wapo wanawake
wanaopenda kukwanguliwa kidogo kwa namna Fulani na kidevu chenye
ndevu.
Kwa wanaume wengi asubuhi ni siku ya matatizo makubwa. Ili kuondoa
matatizo haya yafuatayo yanaweza kabisa kukusaidia kukuweka katika
aina Fulani ya raha kubwa.
1.Chagua mashine ya kunyolea na wembe ambao unadhani unaswihi ngozi
yako. Kuna aina nyingi sana za mashine za kunyolea pamoja na nyembe
zake ni muhimu kujua wembe ambao unatumia kwa kuzingatia mahitaji yako
hasa ya aina ya ndevu
2.Weka uso safi na usio uchafu. Safisha kabla ya kunyoa. Hii
inakusaidia kufungua matundu yanayoshikilia ndevu kabla ya kunyoa ili
kuweza kupata mnyoo laini na wenye uhakika.
3. Usisahau kuloweka kidevu chako vyema. Hii inasaidia wenye kupita
kiulaini zaidi na kama unatumia kiwembe cha kawaida basi ni vyema sana
kufanya kazi hiyo ukitoka kuoga.
4.Tumia maji ya moto siyo yanayounguza kama inawezekana, yanasaidia
sana kufungua vishimo vya vinyweleo. Pia unaweza kupata masaji ya
chapchap katika uso ili kusaidia kulainisha kidevu chako.
5.Chagua krimu hasa inayostahili kwako ya kunyolea kwa kutegemea ngozi
yako na chagua linalostahili unalotaka. Jipake kiasi cha kutosha
katika sehemu zinazostahili kwani husaidia kuburudisha ngozi.
6.Unaponyoa chagua zinapoelekea ndevu. Usiendelee kunyoa sehemu
iliyokwisha kunyolewa. Italeta matatizo na ua uwasha na ukomavu wa
aina Fulani wa kidevu na mbaya zaidi unaweza kujikata.
7. Baada ya kujinyoa, osha uso wako na ondoa krimu zote. Tumia
moistrurizer baada ya kunyoa.
Epeka kutumia after shave yenye pombe. Pombe inasababisha ngozi
kupoteza unyevunyevu wake kwa haraka.
Mwisho
Unatakiwa kuwa makini zaidi katika kutunza uso wako
WATU wengi wamekuwa wakichukulia suala la utunzaji wa ngozi ya uso kwa
umakini zaidi. Ngozi zina mahitaji maalum ikiwemo kuweka ngozi katika
hali ya usafi na pia kuikinga ngozi na miale ya jua na mabadiliko
mengine ya hali ya hewa.
Ngozi ya uso inahitaji umakini zaidi kwani uso ni utambulisho wa
jinsi ulivyo na imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi kwa sababu
uso umekuwa ukizalisha mafuta mengi hasa kwenye paji la uso, macho,
pua, na kidevu.
Hitaji muhimu ni kuhakikisha kuwa, ngozi yako inakuwa katika hali
nzuri na safi kuanzia asubuhi unapoamka hadi usiku unapokwenda
kulala.
Unatakiwa kuchukua dakika tano hadi 10 katika suala hili.
Utunzaji wa uso asubuhi
Wakati wa asubuhi unatakiwa kusafisha uso wako kwa maji ya vuguvugu.
Epuka kutumia sabuni ya mche (ya kufulia) kwani haikutengenezwa
maalum kwa ajili ya uso na imekuwa ikifanya ngozi ya uso kuwa
iliyokakamaa
Unatakiwa kuhakikisha kuwa, uynaosha uso wako vizuri wakati unaoga au
wakati unanawa uso kwenye sinki,
Unaweza kutumia tona kusafisha uso wako kwani husaidia kuondoa uchafu
ulioganda usoni. Baadaye unaweza kutumia moisturiza .
Utunzaji wa uso jioni
Jioni unaweza kusafisha uso wako kwa kutumia maji ya vuguvugu. Baada
ya mizunguko ya hapa na pale ngozi inakuwa imechoka na inahitaji
umakini zaidi katika suala la usafi.
Pia unapotumia tona jaribu kutumi pamba laini ili kuweza kulinda uso wako.
Unapotunza ngozi lengo ni ngozi kuwa na unyevunyevu, unatakiwa
kuhakikisha haina magamba.
Lakini pia unaweza kutoa magamba au ngozi iliyokufa ambayo hufanya
ngozi isiyokubalika.
Wakati mwingine ngozi isiyokubalka husababuisha uso kuwa na chunusi.
Angalizo
Usiende kulala bila kuondoa make -up usoni. Make-up zimekuwa
zikisababisha kuzina kwa vitundu vya kutolea hewa na hivyo kusababisha
tatizo la kuwa na ngozi isiyokubalika.
Pia unatakiwa kuacha kutumia vipodozi vyenye kemikali kwani hufanya
watu wengine kupata kansa za ngozi.Wakati mwingine sehemu za uso
hupata uvimbe .
Hizi ni moja ya changamoto zinazoweza kukutokea katika ngozi yako la
muhimu ni kuhakikisha kuwa, usafi unazingatiwa sana pamoja na kunywa
maji mengi, mboga za majani na matunda kwa wingi.
Subscribe to:
Posts (Atom)