Tuesday, August 3, 2010
Uvaaji wa mikufu na utunzaji wake
NI siku nyingine tena katika urembo na nimeona ni muhimu tukaangalia urembo katika shingo zetu.
Wanawake wengi wenye shingo fupi wana wasiwasi kama kuvaa mikufu kunaweza kufanya waonekane wenye shingo ndefu.
Wabunifu wa mitindo wanasema kuwa, kuvaa mkufu mrefu kunaweza kufanya shingo kuonekana kuwa ndefu.
Wanawake wenye shingo fupi wanashauriwa kuvaa mikufu ambayo inaendana na shingo zao.
Kama unataka muonekano mzuri wa shingo yako unashauriwa kuvaa mikufu ambayo ni inaendana na shingo yako.
Mikufu ya dhahabu imekuwa ikivaliwa sana na kuonekana kuwapendeza wengi Mikufu hii ni ya thamani kubwa ambapo mingine huwa na nakshi za kuvutia.
Lakini si kila mmoja anapenda kuvaa aina hiyo ya mikufu kutokana na kuwa ni ghali sana na wengi wamekuwa hawamudu gharama zake.
Mikufu inayotengenezwa kutokana na silver naye imekuwa ikipendwa na kuvaliwa na watu wengi wa rika zote.
Aina hii ya mikufu imekuwa ikivaliwa zaidi pia na wanaume ambao hupenda kuivaa ikiwa imetengenezwa mithiri ya minyororo midogo.
Uvaaji wa mikufu iunayotengenezwa na dhanga au vitu vya asili kama shamba, vifuu vya nazi na vitu vingine vya asili vimekuwavikivaliwa kwa wingi na wanawake kwa wanaume na kuonekana ni mfano mzuri kwa kutunza utamaduni wa Mtanzania.
Uvaaji wa mikufu hii ya asili huwapendeza zaidi wanawake hasa pale wanapovaa kwa nguo za vitenge huku sehemu kubwa a vazi hili shingoni likiwa wazi.
Mikufu hiyo ina aina ya utunzaji wake ili iweze kudumu zaidi na kuendelea kutunza thamani yake.
Tukianza na utunzaji wa mikufu ya dhahabu, hii inahitaji uangalifu wa hali ya juu ilinapokuja suala la wapi na kwa njia gani mikufu hii inaweza kutunzwa.
Mikufu ya dhahabu inapendeza sana kama ikitunzwa kwenye kasha dogo baada ya kulizungushia kitambaa laini hii husaidia vitu hivyo kutopoteza thamani yake kwa kuhifadhi mng’ao wake.
Hata katika uvaaji wake mikufu hii huitaji kuvaliwa vyema kwa uangalifu mkubwa ili isiweze kushikana na nguo na hatimaye kukatika.
Aina hizo zote za mikufu zinahitaji utunzaji mzuri ili vitu hivyo viendelee kuwa vizuri ikiwemo kuwa na sehemu maalum ya kutunzia mikufu ili kuwa rahisi kwa mvaaji kuitumia mara anapohitaji kuvaa.
Wengi wetu wamekuwa wakitundika mikufu yao ya shanga na plastiki au ile ya asili kwenye stendi maalum iliyotengenezwa kwa ajili hiyo.
Hiyo husaidia sana kwani hata mvaaji hapati shida kujua mkufu wa aina gani unafanana na aina ipi ya nguo pindi anapotaka kuivaa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment