Monday, August 31, 2009

NAMNA NZURI YA KUOSHA NYWELE ZAKO



KUNA kitu muhimu kuhusu uoshaji wa nywele, nywele zako ambazo unataka zikae unavyotaka kulingana na kichwa chako ili uwe na uvuto wa haiba yake katika mambo yote yanayokuzunguka.
katika mazingira ya kawaida uoshaji nywele ni kitu cha kawaida na hivyo mara nyingi hatufikirii sana suala la kuosha nywele, si la kawaida tu mwenzangu? Lakini uoshaji nywele wa uhakika wenye makini kwa kutumia shampuu kunaweza kuleta mabadiliko makubwa katika muonekano na umetaji wa nywele zako na hata makuzi yake.
Ndio kusema uoshaji wa kutumia shampuu unaweza kabisa kukupa kile ambacho huwezi kukipata katika hali ya kawaida , muondoko wa ukaaji wa nywele baada ya kuosha.
Lakini kama hutajali tulijadili hili suala la uoshaji nywele ambalo ni la kawaida tu.Naama, la kawaida lakini lenye maana kubwa kwa watu wanaojijali.
Mimi nadhani haitaumkiza kama nikisema kwa ufupi fupi kuhusu hizi shampuu za kuonshea nywele, hizi shampuu ambazo unazipata dukani, kwenye dula la urembo.
Kwanza ni lazima utambue kwamba si kila shampuu inafaa katika kusuklia nyweleza ko (uoshaji) kwani nyingine huleta mushkeri hasa kama unaumwa eczema, hali ya kuchoma choma, uwasho wa nywele, mba au aina ya grisi katika ngozi ya nywele zako wakati wa kuzitengeneza.
Nataka kukuambia kwamba bidhaa zinazotokana na uasili husaidia sana kutengeneza utamu wa nywele kama kweli unaujua na mara zote hufanyakazi bora kwa aina zote za vichwa hata kama zina matatizo niliyotaja hapo juu.
Na pia huleta aina ya burudiko.
Mara zote tunapoosha nywele zetu huwa tunaharibu lakini kama utakuwa mwangalifu kwa kutumia shampuu zenye viambata vya asili (organiki-natural botanical)utakuwa na nafasi kubwa ya kuwa na nywele tamu na wewe kuondokana na adha za uchafu wa nywele unaotia 'wazimu'.
Kama utakuwa huna shampuu ile ya dukani ambayo ina aviambata vya asili nashauri utumie yai. yai ni kifaa kizuri kabisa cha kusafishia.tenganisha kiini cha yai kutoka katika uite mweupe. konga tofauti kisha changanya na taratibu zitumie kuzichanganya katika nywele ne kusukasuka. Acha kwa dakika tatu na kisha safisha kwa maji ya uvuguvugu si ya moto kwani ukitia maji ya moto yao litajikusanya maeneo fulani fulani kichwani halafu itakuwa shida.
Njia tano za kuosha nywele zako:
1.Inama katika beseni. Hii inasaidia kutoa nafasi ya ukaaji mzuri wa kuanza kusafisha nywele bila kuumiza shingo yako na pia kusaidia kuweka damu katika mzunguko unaotakiwa.
2.Tumia kikombe kimoja cha shampuu. Ikiwa nyingi italeta matatizo kidogo na kidogo pia haitatoa kitu kinachostahili. pakaza kwa kusukasuka kila mahali kichwani mwako kwa kuanzia mbele kwenda nyuma na kisha pembeni. Kwa nywele za grisi(mafuta) changanya shampuu na maji kidogo.
3. Tumia ncha ya vidole vyako kufika mwisho wa nywele na kuzimasaji vyema kuhakikisha kwamba shampuu inaingia katika ngozi ya kichwa. Safisha kwa raha kwani inatakiwa ujisikie raha kubwa wakati wa shughuli hii ya kusafisha nywele.
4.Hakikisha kwamba umesafisha sawasawa kichwa chako kisha unaondoa shampuu kwa maji..Kitu cha maana ni kuwa usafishaji lazima ufanyike kwa uangalifu mkubwa kwani baada ya kutia shampuu na kuipeleka kila mahali kuiondoa baada ya hapo ni kitu muhimu.Iondoe kwa maji na kisha kujihakikisha kwamba imeondoka, unastahili kukitia kichwa chako maji ya baridi kwa ajili ya kutoa busti zaidi.
5.Kausha nywele zako kwa taulo safi (kwepa kusugua nywele hizo kwa taulo).Kifunike kichwa na taulo hilo ili linyonye maji taratibu na baada ya hapo unaweza kutia kitu kinachotakiwa ili kuweka nywele za safi.

No comments:

Post a Comment