Tuesday, March 28, 2017

Tuko katika maonesho njoo Tuunge mkono




WAJASIRIAMALI nchini wametakiwa kutumia vifungashio vyenye ujazo sahihi ili kufikia soko la kimataifa.
Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam leo na Kaimu Meneja Sehemu ya Elimu, Habari na Mawasiliano kutoka Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA), Irene John wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Wajasiriamali yaliyoandaliwa na Chama cha Akiba na Mikopo (Saccos) cha Wajasiriamali Wanawake Tanzania (TASWE).
John alisema wajasiriamali wengi nchini wamekuwa wakishindwa kuyafikia masoko ya kimataifa kutokana na vifungashio vyao kukosa vipimo sahihi.
Huwezi kufikia soko la kimataifa kama utatumia vipimo sahihi kama kitu ni cha kilo moja weka kwenye ujazo wa kilo moja kwa kufanya hivi utaweza kujitangaza na kuifanya biashara yako kuwa kwenye kiwango sahihi, alisema John na kuongeza kuwa matumizi ya ujazo usio sahihi sio tu yanawanyima kujulikana katika soko la kimataifa, bali yanaweza kuwaumiza wajasiriamali au walaji.
Kuna ambao wanatumia chupa za maji kufungasha bidhaa zao, lakini hawajui kama maji ni mepesi na ujazo wake wake hauwezi kulingana na asali hivyo unaweza kujinyima wewe kama mjasiriamali au ukamnyima mlaji, aliongeza.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TASWE, Anna Matinde alisema maonesho hayo yameshirikisha wajasiriamali 192 kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Comoro, Uganda, Rwanda, Kenya na wenyeji Tanzania.
Matinde alisema maonesho hayo ni muhimu kwa kuwa yanasaidia nchi zilizoshiriki kubadilishana uzoefu katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali.
Aidha, alisema ili kuhakikisha elimu ya ujasirimali inafika katika nchi za Afrika Taswe inajenga chuo cha mafunzo Comoro ili kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa bidhaa za Tanzania.
Naye Ofisa Ukuzaji wa Biashara kutoka Mamlaka ya Uendelezaji Biashara Tanzania (Tantrade), Judith Matage alitoa mwito kwa wajasiriamali hao kuyatumia maonesho hayo kujitangaza na sio kuuza bidhaa pekee.
Hii ni fursa lazima muitumie sio muuze tu sambazeni mawasiliano kwa wajasiriamali kutoka nchi nyingine kwa kufanya hivi kutawaongezea kujitangaza katika nchi mbalimbali, alisema Matage.

Saturday, February 13, 2016

Mwanaume kuwa na ngozi nzuri huleta furaha, kujiamini

HAIJALISHI unafanya kazi kwenye mazingira gani lakini cha muhimu ni kuzingatia unatunza vizuri ngozi yako ya uso ili kuboresha muonekano wake. Mwanaume kuwa na ngozi nzuri huleta, furaha na kujiamini pia . Muonekano mzuri usoni ni miongoni mwa mambo ambayo wanaume wanatakiwa kuyazingatia na hili linawezekana kama utaijali ngozi yako na utanashati kwa jumla. Kuna wanaume ambao hawana hata muda wa kujiangalia kwenye kioo labda kwa kudhani kuwa mambo hayo yanatakiwa kufanywa na wanawake jambo ambalo si sawa sawa. Kuna mambo mengi ambayo mwanaume anatakiwa kufanya ili aweze kuonekana na muonekano mzuri. Miongoni mwa mambo hayo ni kuhakikisha unasafisha uso na kutakata, hapa unaweza kutumia taulo laini kwa kupaka kidogo sabuni na kisha safisha uso taratibu na baadaye unasuuza uso na kuufuta. Pia unaweza kutumia cleanser ambayo ni maaluma kwa ajili ya kusafisha uso. Si jambo la ajabu unapopita kwenye saluni na kukuta wanaume wakisafishwa uso au kufanya scrubing ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikisaidia kuondoa madoa usoni, mafuta na kufanya ngozi ipendeze. Unaposafisha uso unaruhusu vitundu vya kutolea hewa kubaki wazi na hivyo kufanya ngozi kuwa na afya nzuri na hata muonekano wake kuwa bora zaidi. Jitahidi kusaifisha uso na kufanyia scub uso wako japo angalau mara mbili kwa wiki jambo hili kwa kiasi kikubwa husaidia kuondoa seli zilizokufa kwenye ngozi. Pia hufanya kuwa laini na ya kuvutia. Unaweza kupaka loshen au cream za kiume ambazo zipo madukani kwa ajili ya kuboresha zaidi ngozi yako.

Thursday, August 27, 2015

Unene husababisha muda mfupi wa kuishi



Uzito ni sawa na uvutaji wa sigara ambao huleta matatizo makubwa kwa watu ambao wamo katika kilinge hicho.

Wataalam wa afya na urembo wanasema wazi kuwa mnene kunapunguza sit u namna ya kujiweka sawa katika masuala mbalimbali ya kijamii lakini pia unakuwa na muda mfupi sana wa kuishi duniani.
Wataalam wanasema kwamba kuwa mzito kunapunguza maisha yakokwa miaka mitatu anasema mtafiti Gary Whitlock kutoka Clinical Trial Service Unit ya Chuo Kikuu cha Oxford  kilichopo
Uzito huo ni ule unaokuwa mara tatu ya uzito ambao mtu anatakiwa awe nao kutokana na urefu wake, umri na afya yake.
Ndio kusema kama mtu anakuwa na uzito mathalani paundi 150 mtu huyo anapunguza umri wake wa kuishi duniani kwa miaka 10.
Pia uzito wa kuchusha umekuwa ukileta tatizo la figo, ini na aina kadhaa za kansa na pia huleta matatizo ya magonjwa ya moyo na kiharusi.
Unene huleta mchosho mkubwa kwa moyo na huleta mizania dhaifu ya rehemu na kusababisha shida katika mwenendo wa damu.
Wakati wanaume wenye kiuno kikubwa huongeza hatihati ya kifo wakati wanawake wenye mzunguko mkubwa huongeza hatihati ya kifo kwa asilimia 78

Uvaaji sketi fupi uzingatie utamaduni wetu


UVAAJI wa sketi fupi mara nyingi hutegemea na matakwa ya mavaaji,


 kwani mara ntingi sketi fupi huishia juu ya magoti na huwa na urefu usiozidi sentimita 10.
Vazi hili mara nyingi huvaliwa na wanawake wa nchi za magharibi pia utamaduni huu umeenea sana hapa nchini ambapo wanawake na wasichana wengi wamekuwa wakivaa aina hizi za nguo na kuonekana kuwa wanakiuka maadili ya Kitanzania.
Wataalam wa mavazi wanasema, chimbuko la sketi fupi ni huko London Uingereza katika miaka ya 1960 ambapo wanawake walikuwa wakivaa nguo hizo katika michezo mbalimbali na wakati huo nguo fupi zilikuwa zikijulikana kama nguo za michezo kwani zilikuwa zikivaliwa sana na wacheza tenisi.
 Wengi wanaovaa aina hiyo ya nguo wamekuwa na sababu tofauti huku wengine wakidai kuwa vazi hili hufanya wajiamini zaidi huku wengine wakidai kuwa sketi fupi hufanya wajione bomba zaidi na kuonekana wanakwenda na wakati.
Sketi fupi zipo kwenye fasheni miaka nenda rudi japo watu wengine wamekuwa wakivaa nguo hizo zikiwa fupi sana na kuleta mtafaruku hata pale wanapokuwa wanapita barabarani.
Muhimu kuhakikisha kuwa unapochagua nguo ya kuvaa angalia kama inaendana na mazingira na utamaduni wa Mtanzania na je nguo yake umevaa mahali gani na kama unaona ni kero unapofanya hivyo basi unashauriwa kuacha kufanya hivyo.
Wengi wanavaa sketi fupi na viatu virefu huku wakitembea umbali mrefu hali inayosababisha kupoteza maana na heshima pia.
Vaa nguo kulingana na mazingira, kama una gari ni sawa lakini kama unajua unakwenda kutumia usafiri wa daladala huku ukiwa umevaa sketi fupi itakayokufanya ushindwe kukaa vizuri na hata kuinama hiyo si sawa sawa.


Thursday, February 12, 2015

Rangi ya tai huzungumza



Wachambuzi wa mambo ya saikolojia wanasema kwamba kwa kuchukua tai na kulivaa ile rangi ndiyo itakayoweza kupeleka ujumbe wa wewe unataka nini au unataka watu wakutambue  kwa namna gani.
Wakati Joshua Blue, Makamu mkuu wa shule ya Kennedy mjini Hong Kong, anapoendesha baraza la wanafunzi anavaa tai lenye rangi ya light violet ili kumpa mamlaka.
Tai la rangi ya bluish-purple  anasema ni “colourful yet muted”, anaamini kwamba rangi ya bluu inawafanya wanafunzi wasiboreke wakatiw anasikiliza, anajizuia kutumia brighter purples na pinks wakati akiwa mbele ya wanafunzi.
“Huhitaji kuwa na rangi nyingi zinazong’aa kwani watoto watajivuruga,” anasema Blue mwenye umri wa miaka 35.
Hakika inaweza kuwa kama kichekesho lakini wataalamu wanasema kwamba uchaguzi wa rangi ya tai inasaidia sana kupeleka ujumbe unaotakiwa kwa wahusika. Na hii haijalishi ni mteja, mdau wafanyakazi au watoto.
 “Rangi hutoa aina Fulani ya ishara,” anasema David Zyla, Mwandishi mwenye makao makuu yake New York anayeandika Color Your Style.
“Suti ile ile inaweza kubadilishwa kimtindo yaani salamu zake kwa kubadili rangi ya tai, na kila mvao ukawa na ishara na salamu tofauti.”
Baada ya kusoma maelezo yote hayo, nikuulize je sasa unaweza kufikiria unataka kuvaa tai gani katika mkutano wako ujao.Labda nikusaidie kwa namna hii.:
Rangi inayotawala, rangi nyekundu
Si bahati mbaya au kitendo cha kubahatisha kwa wanasiasa wengi kuvaa tai lenye rangi nyekundi ndani ya suti zilizo dark  na mashati mepesi.
“Tai nyekundu inaonesha mamlaka,” anasema Mark Woodman, mchambuzi wa mambo ambaye amejifunza masuala ya huko Laurel, Maryland, Marekani. “Kuna kitu Fulani kipo ndani ya rangi nyekundu ambacho mara zote kinajitokeza kumuimarisha mtu na kumpa mvuto wa pekee.”


Ofisa Mtendaji wa JPMorgan, Jamie Dimon huvaa tai nyekundu anapozungumza na  wananchi
Hata hivyo wataalamu wanasema kwamba kuna rangi nyekundu na rangi nyekundu.Nyekundu iliyokoza kwa miondoko ambayo wazungu wanasema ni burgundy, husaidia kuleta imani na matumaini wakati ile nyekundu nyepesi na pink inakuwa zaidi onesho la ubunifu na namna ulivyo kistaili.Katika miaka michache iliyopita rangi ya pink inaweza kuonesha mshikamano na wamama anasema Woodman.
Wakati unaendesha mradi au unataka kupeleka ujumbe Fulani kwa kruu yako fikiria kuvaa tai la rangi nyekundu iliyokoza ambayo inashaini.Tai la rangi nyekundi unaweza kuwa njia bora ya kuonesha mamlaka.
Royal purples
Ross Znavor, Mtendaji katika moja ya taasisi za kifedha mjini New York yeye huvaa tai la rangi ya purple na si nyekundu katika mikutano ya kibiashara,Rangi hii huonesha kujiamini na humsaidia watu kuendelea kumkumbuka.
Anasema kuvaa tai hilo kunampatia mtu mwingine kukubali kwamba wewe unaweza kushirikiana naye na kujenga uhusiano wa kudumu.
Lindsay anasema purple, kiasili ni rangi ya utiifu na utajiri na kwa sasa inaaanza kukubalika maeneo ya kazi.
 


Arnold Schwarzenegger huonesha kujiamini kwa kuvaa tai rangi ya purple.
“Wanaume wanaovaa mashati ya lighter purple na tai za darker purple, hutaka kutambulika haraka katika kundi bila kuleta ushawishi mwingine wa kipuuzi unaovuruga”.
Rangi nyeusi
Inawezekana  huvai kila siku au kila mahali lakini ukivaa tai nyeusi katika mikutano ya watendaji, kwenye dhifa unakupa wewe hali ya muondoko mweroro wenye utanashati mkubwa , anasema Zyla.

Muigizaji sinema Leonardo DiCaprio  huvaa tai nyeusi katika mikutano au maeneo ambayo ni ya kikazi zaidi.
Lakini ni kweli kuwa rangi nyeusi inakufanya kuwa na ujeuri wa aina Fulani na  wengine wanasema kusema kwamba  inakuwa overdressed katika mazingira mengi. “Rangi hii inafaa kutotumika kama wewe unataka kuendelea kupanda ngazi, wapandisha ngazi wanaweza kufikiria kwamba wewe ni jeuri wa aina Fulani hivi,” anasema Zyla.
Ni vyema sana kama mtu atakuwa amejipatia grey shades, anaongeza Woodman. Tai la rangi ya grey linaweza kukupa mwonekano wenye mvuto mweroro usio na jeuri na usiojinata anasema Woodman.
“Grey  iko poa, iliyotulia na ya kisasa zaidi,” anasema.Ili kuifanya iwe imetulia zaidi piga tai hili na shati ambalo ni lighter, pastel-coluored.  Tafadhali angalia lighter grey shades na  malizia na shaini ili kukupa muonekano ambao ni polished.
Rangi ya kijani
Rangi ya kijani ina maana nyingi kuanzia kuzaliwa upya hadi rangi ya fedha kwa mataifa Fulani.Lakini cha ajabu ni rangi yenye ‘kelele’ nyingi katika maeneo ya kazi.
Wakati mwingine kijani inakuwa too much.


“Je unataka kukumbukwa akwa ajili ya tai au kama wewe binafsi?,”  anauliza Woodman .Anasema kuchagua rangi ya kijani inayostahili ni kazi kubwa.Kijani inayowaka inavuruga kutokana na mwako wake na pia inakuwa na taabu sana kupata suti inayoambatana nayo au hata shati. Hata hivyo tai la light green likiwa na subtle print linaweza kuwa jema katika shati ambalo rangi yake ni neutral.
Tai ya rangi ya njano, ni tai la kiasili kwa nchi nyingi hata waingereza   wanaliheshimu kwa sababu linakupa uhakika, kukuweka mng’avu na mwenye siha hasa ya kufaa.
Ni rangi inayoonesha jua, hivyo watu wengi wanaweza kuwa na kishawishi cha kuzungumza nawe kwa sababu ya ukweli kuwa ni rangi yenye mvuto wa kipekee. Kwa wengi kuvaa tai la rangi ya njano kunaonesha kwamba maisha yeye anayaangalia katika dunia chanya zaidi, anasema Eve Roth Lindsay, mshauri wa masuala ya muonekano wa Hong Kong.
 Lakini kiukweli kuwa unapaswa kuwa mwangalifu usije ukafanya kosa la uasili na utamaduni wa eneo lenu inapokuja suala la rangi.
Mathalani rangi ya njano nchini india ina maananisha kwamba wewe ni mfanyabiashara wakati rangi nyeupe nchini China inamaana upo katika kipindi cha maombolezo.
Rangi ya bluu
 Unahofu ya kupeleka ujumbe ambao uhuhitaji kwa kutumia tai uliyovaa yaani rangi yake?basi ni vyema ukafikiria kutumia tai ya rangi ya bluu.
Rangi hii hutumika katika matukio yote.
Rangi ya bluu ni rangi bomba kwa kuwa inawakumbusha watu anga na bahari, vitu vyenye kutuliza maisha ya binadamu anasema Lindsay.
“Rangi ya bluu hakika ni salama zaidi kuivaa,” anasema. 


Bluu inaonekana dhahiri ni rangi ya nguvu ya kimataifa
Tai ya Patterned blue hutoa hali ya kutulia na kitaalamu zaidi na inaweza kutumiwa katika mikutano ya kimataifa ya kibiashara na mazingira bila kupeleka ujumbe  usiotakiwa.
 Tai ya  subtle blue inaweza kuwa na mvuto na kujionesha undani wakati cobalt au royal blue hukufanya ujiachie ndani ya kundi kwa namna Fulani. “Bluu iliyokoza ni rangi ya marubani watukuka. Bluu bahari ni rangi inayoaminika, inayokupa imani na kiburi cha uwezo,”  anasema Lindsay .
Kuwa rafiki na asili
“Kabati lako likiwa na rangi rafiki za asili kama tan, kahawia, earthy colours, salmon na njano hufaa sana kwa watu wanaojishughulisha na wengine kama wafanyabiashara (mauzo), walimu na watu wa huduma mbalimbali,” anasema Lindsay.
Hakikisha kwamba tai la rangi ya  kahawia haiku pekee kwani inaweza kuonesha ugoigoi katika wajihi. Hata hivyo  tai la beige linaweza kukuonesha kwamba huna matatizo, yuko huru.
Epuka kuvaa tai la rangi ya udongo na shati linalofanana nalo. Na kama unataka kujishebedua na kuonekana kweli katika eneo la kazi rangi hizi za asili achana nazo kabisa.