Wachambuzi wa mambo ya saikolojia
wanasema kwamba kwa kuchukua tai na kulivaa ile rangi ndiyo itakayoweza
kupeleka ujumbe wa wewe unataka nini au unataka watu wakutambue kwa namna gani.
Wakati Joshua Blue, Makamu mkuu wa
shule ya Kennedy mjini Hong Kong, anapoendesha baraza la wanafunzi anavaa tai
lenye rangi ya light violet ili kumpa mamlaka.
Tai la rangi ya bluish-purple anasema ni “colourful yet muted”, anaamini
kwamba rangi ya bluu inawafanya wanafunzi wasiboreke wakatiw anasikiliza,
anajizuia kutumia brighter purples na pinks wakati akiwa mbele ya wanafunzi.
“Huhitaji kuwa na rangi nyingi
zinazong’aa kwani watoto watajivuruga,” anasema Blue mwenye umri wa miaka 35.
Hakika inaweza kuwa kama kichekesho
lakini wataalamu wanasema kwamba uchaguzi wa rangi ya tai inasaidia sana
kupeleka ujumbe unaotakiwa kwa wahusika. Na hii haijalishi ni mteja, mdau
wafanyakazi au watoto.
“Rangi hutoa aina Fulani ya ishara,” anasema David
Zyla, Mwandishi mwenye makao makuu yake New York anayeandika Color Your Style.
“Suti ile ile inaweza kubadilishwa
kimtindo yaani salamu zake kwa kubadili rangi ya tai, na kila mvao ukawa na
ishara na salamu tofauti.”
Baada ya kusoma maelezo yote hayo,
nikuulize je sasa unaweza kufikiria unataka kuvaa tai gani katika mkutano wako
ujao.Labda nikusaidie kwa namna hii.:
Rangi inayotawala, rangi nyekundu
Si bahati mbaya au kitendo cha
kubahatisha kwa wanasiasa wengi kuvaa tai lenye rangi nyekundi ndani ya suti
zilizo dark na mashati mepesi.
“Tai nyekundu inaonesha mamlaka,” anasema
Mark Woodman, mchambuzi wa mambo ambaye amejifunza masuala ya huko Laurel,
Maryland, Marekani. “Kuna kitu Fulani kipo ndani ya rangi nyekundu ambacho mara
zote kinajitokeza kumuimarisha mtu na kumpa mvuto wa pekee.”
Ofisa Mtendaji wa JPMorgan, Jamie
Dimon huvaa tai nyekundu anapozungumza na
wananchi
Hata hivyo wataalamu wanasema kwamba
kuna rangi nyekundu na rangi nyekundu.Nyekundu iliyokoza kwa miondoko ambayo
wazungu wanasema ni burgundy, husaidia kuleta imani na matumaini wakati ile nyekundu
nyepesi na pink inakuwa zaidi onesho la ubunifu na namna ulivyo kistaili.Katika
miaka michache iliyopita rangi ya pink inaweza kuonesha mshikamano na wamama
anasema Woodman.
Wakati unaendesha mradi au unataka
kupeleka ujumbe Fulani kwa kruu yako fikiria kuvaa tai la rangi nyekundu
iliyokoza ambayo inashaini.Tai la rangi nyekundi unaweza kuwa njia bora ya
kuonesha mamlaka.
Royal purples
Ross Znavor, Mtendaji katika moja ya
taasisi za kifedha mjini New York yeye huvaa tai la rangi ya purple na si nyekundu
katika mikutano ya kibiashara,Rangi hii huonesha kujiamini na humsaidia watu
kuendelea kumkumbuka.
Anasema kuvaa tai hilo kunampatia
mtu mwingine kukubali kwamba wewe unaweza kushirikiana naye na kujenga uhusiano
wa kudumu.
Lindsay anasema purple, kiasili ni
rangi ya utiifu na utajiri na kwa sasa inaaanza kukubalika maeneo ya kazi.
Arnold Schwarzenegger huonesha
kujiamini kwa kuvaa tai rangi ya purple.
“Wanaume wanaovaa mashati ya lighter
purple na tai za darker purple, hutaka kutambulika haraka katika kundi bila
kuleta ushawishi mwingine wa kipuuzi unaovuruga”.
Rangi nyeusi
Inawezekana huvai kila siku au kila mahali lakini ukivaa
tai nyeusi katika mikutano ya watendaji, kwenye dhifa unakupa wewe hali ya
muondoko mweroro wenye utanashati mkubwa , anasema Zyla.
Muigizaji sinema Leonardo DiCaprio huvaa tai nyeusi katika mikutano au maeneo
ambayo ni ya kikazi zaidi.
Lakini ni kweli kuwa rangi nyeusi inakufanya
kuwa na ujeuri wa aina Fulani na wengine
wanasema kusema kwamba inakuwa overdressed
katika mazingira mengi. “Rangi hii inafaa kutotumika kama wewe unataka
kuendelea kupanda ngazi, wapandisha ngazi wanaweza kufikiria kwamba wewe ni
jeuri wa aina Fulani hivi,” anasema Zyla.
Ni vyema sana kama mtu atakuwa
amejipatia grey shades, anaongeza Woodman. Tai la rangi ya grey linaweza kukupa
mwonekano wenye mvuto mweroro usio na jeuri na usiojinata anasema Woodman.
“Grey iko poa, iliyotulia na ya kisasa zaidi,” anasema.Ili
kuifanya iwe imetulia zaidi piga tai hili na shati ambalo ni lighter,
pastel-coluored. Tafadhali angalia lighter grey shades na malizia na shaini ili kukupa muonekano ambao
ni polished.
Rangi ya kijani
Rangi ya kijani ina maana nyingi
kuanzia kuzaliwa upya hadi rangi ya fedha kwa mataifa Fulani.Lakini cha ajabu
ni rangi yenye ‘kelele’ nyingi katika maeneo ya kazi.
Wakati mwingine kijani inakuwa too
much.
“Je unataka kukumbukwa akwa ajili ya
tai au kama wewe binafsi?,” anauliza Woodman
.Anasema kuchagua rangi ya kijani inayostahili ni kazi kubwa.Kijani inayowaka
inavuruga kutokana na mwako wake na pia inakuwa na taabu sana kupata suti
inayoambatana nayo au hata shati. Hata hivyo tai la light green likiwa na
subtle print linaweza kuwa jema katika shati ambalo rangi yake ni neutral.
Tai ya rangi ya njano, ni tai la
kiasili kwa nchi nyingi hata waingereza wanaliheshimu kwa sababu linakupa uhakika,
kukuweka mng’avu na mwenye siha hasa ya kufaa.
Ni rangi inayoonesha jua, hivyo watu
wengi wanaweza kuwa na kishawishi cha kuzungumza nawe kwa sababu ya ukweli kuwa
ni rangi yenye mvuto wa kipekee. Kwa wengi kuvaa tai la rangi ya njano
kunaonesha kwamba maisha yeye anayaangalia katika dunia chanya zaidi, anasema Eve
Roth Lindsay, mshauri wa masuala ya muonekano wa Hong Kong.
Lakini kiukweli kuwa unapaswa kuwa mwangalifu
usije ukafanya kosa la uasili na utamaduni wa eneo lenu inapokuja suala la
rangi.
Mathalani rangi ya njano nchini
india ina maananisha kwamba wewe ni mfanyabiashara wakati rangi nyeupe nchini
China inamaana upo katika kipindi cha maombolezo.
Rangi ya bluu
Unahofu ya kupeleka ujumbe ambao
uhuhitaji kwa kutumia tai uliyovaa yaani rangi yake?basi ni vyema ukafikiria
kutumia tai ya rangi ya bluu.
Rangi hii hutumika katika matukio
yote.
Rangi ya bluu ni rangi bomba kwa
kuwa inawakumbusha watu anga na bahari, vitu vyenye kutuliza maisha ya binadamu
anasema Lindsay.
“Rangi ya bluu hakika ni salama
zaidi kuivaa,” anasema.
Bluu inaonekana dhahiri ni rangi ya
nguvu ya kimataifa
Tai ya Patterned blue hutoa hali ya
kutulia na kitaalamu zaidi na inaweza kutumiwa katika mikutano ya kimataifa ya
kibiashara na mazingira bila kupeleka ujumbe
usiotakiwa.
Tai ya subtle blue inaweza kuwa na mvuto na
kujionesha undani wakati cobalt au royal blue hukufanya ujiachie ndani ya kundi
kwa namna Fulani. “Bluu iliyokoza ni rangi ya marubani watukuka. Bluu bahari ni
rangi inayoaminika, inayokupa imani na kiburi cha uwezo,” anasema Lindsay .
Kuwa rafiki na asili
“Kabati lako likiwa na rangi rafiki
za asili kama tan, kahawia, earthy colours, salmon na njano hufaa sana kwa watu
wanaojishughulisha na wengine kama wafanyabiashara (mauzo), walimu na watu wa
huduma mbalimbali,” anasema Lindsay.
Hakikisha kwamba tai la rangi ya kahawia haiku pekee kwani inaweza kuonesha
ugoigoi katika wajihi. Hata hivyo tai la
beige linaweza kukuonesha kwamba huna matatizo, yuko huru.
Epuka kuvaa tai la rangi ya udongo
na shati linalofanana nalo. Na kama unataka kujishebedua na kuonekana kweli
katika eneo la kazi rangi hizi za asili achana nazo kabisa.