Sunday, September 28, 2014
Tumia mchanganyiko wa papai na asali kuondoa madoa usoni
Kuna maswali mengi yanayoulizwa jinsi ya kuondoa madoa usoni. Lakini jambo kubwa la kuangalia
je madoa uliyonayo
yamesababishwa na nini, Je ni kwa ajili ya kutumia madawa yenye kemikali kali kwa lengo la kupendezesha ngozi au ni
vipele tu vya kawaida.
Wengi wanapenda kutumia sabuni na cream kali ambazo baadaye zimekuwa zilileta madhara makubwa kwenye ngozi zao na
kuwafanya kuwa na mabaka meusi.
Ni muhimu pia kujifunza kutumia vipodozi vya asili ambavyo havina madhara kwenye ngozi.
Unaweza kutumia mchanganyiko wa papai na asali kwa ajili ya kuondoa madoa usoni.
Mchanganyiko huu ambayo huwa laini utauacha ngozi yako ikiwa nyororo na yenye kuvutia.
Namna ya kutumia.
Kwanza ni kusafisha uso kwa maji ya vuguvugu kwa kutumia kitambaa laini pia unaweza kusafisha hadi shingoni na hakikisha
uso umekataka kisha futa uso wako na shingo kwa taulo.
Andaa asali yako pembeni kisha kata papai na kisha liponde hadi kulainika kabuisa.
Baada ya hapo changanya rojo hiyo ya papai na asali koroga hadi kuhakikisha umepata mchanganyiko mzuri.
Anza kupata usoni taratibu hadi maeneo ya shingo unaweza kukaa na mchanganyiko huo kwa robo saa kisha safisha uso
wako.
Unaweza kutumia mchanganyiko huu mara kadhaa kwa wiki mpaka upate matokeo mazuri kwenye ngozi yako.
Lakini jambo la msingi ni kuhakikisha anaepuka kutumia cream zenye kemikali kali kwani zimekuwa na madhara kwenye
ngozi.
Subscribe to:
Posts (Atom)