KUMEKUWA na sababu mbalimbali zinazofanya watu kutokuwa na
ngozi zisizokubalika.Mbali na hali ya hewa pia matumizi ya pombe na sigara hata
matumizi ya cream kali ambazo zimekuwa zikitumiwa na watu bila kujua madhara
yake kumechangia kwa kiasi kikubwa tatizo hilo.
Ngozi kwa kawaida inatakiwa ijitengeneze yenyewe na si
kuitengeneza kwa vipodozi kama wengi wanavyodhani. Ulaji wa matunda na mboga za
majani kwa wingi kunywa glasi nane za maji kwa siku ni njia nzuri kama unataka
kuwa na ngozi nzuri isiyo na madoa wala ukavu ambao haupendezi.
Wengi wanaacha kula mbogamboga na matunda kwa wingi hata
kutokunywa maji ya kutosha na badala yake wamekuwa akitegemea kuwa na ngozi
nzuri jambo ambalo ni gumu.Mara kadhaa tumeshuhudia watu wanaopaka cream kali
wakiwa kama wameungua usoni huku uso na mwili ukionekana kuwa makavu jambo
ambalo linaashiria kuwa kupaka cream si
suruhisho la kuwa na ngozi nzuri.
Kuna watu wamekuwa na ngozi za asili na hata unapowauliza
baadhi yao hawajawahi kupaka cream hata siku moja na bado wana ngozi nzuri
zinazovutia hao wamekuwa wakila kwa ajili ya kuhakikisha wanatengeneza ngozi
zao kutoka ndani.
Pia wengi wanaharibu ngozi zao na kuwa na madoa kutokana na
kutumia make up kwa muda mrefu na hata
anapogundua kuwa ana tatizo la madoa amekuwa akijaribu kutumia cream nyingine
kwa ajili ya kumaliza tatizo hilo jambo ambali linazidisha madhara kwenye
ngozi.
Unaweza kutibu ngozi yenye madoa usoni pia mashavuni kwa kujitibu na juisi ya limao.
Namna ya kufanya
Chukua limao lioshe
na kisha likamue na kuchuja mbegu zake. Weka juisi hiyo kwenye kikombe na kisha
tafuta kitambaa laini kichovye kwenye
juisi ya limao na dondoshea juisi ya limao kwenye sehemu zenye tatizo.
Kaa kama dakika tano
kisha usha uso kwa maji safi.Pia unaweza kuchanganya na asali mbichi na maji ya limao husaidia pia kuondoa madoa
usoni.
Limao lina sifa kubwa ya kuzuia harufu pia unaweza kulitumia
katika kuondoa harufu kali ya jasho mwilini
na husaidia kuondoa weusi kwenye kwapa, chini ya macho, mapajani pia.
Chukua kipande cha limao weka sukari kidogo, sugua.Unatakiwa kutumia
kwenye kwapa ambalo ni safi, vizuri kutumia njia hii kabla na baada ya kuoga.