Saturday, February 22, 2014

Matango kitu muhimu katika mwili wako


WATAALAMU wamesema kwamba matango ni chakula muhimu sana katika mwili wako kutokana na kufanhyakazi mbalimbali za kuuweka sawa pamoja na kuupa maji.
Ni vyema kuhakikisha kwamba kila siku unakula tango kwa afya yako.
Hakika kama upo bize sana kiasi cha kusahau kuinywa maji ya kutosha, kula tango ambalo asilimia 90 ni maji. tango litakuongezea maji unayohitaji.
Tango pia linakabiliana na joto nje na ndani ya mwili. ndio kusema kwa kula tango mwili unapunguza mashambulio ya kiungulia. Pia kama utajipaka tango utapata nafuu sana dhidi ya miale ya jua.
Kazi nyingine ya tango ni kupunguza sumu katika mwili, maji yote yaliyomo ndani ya tango linafanya liwe kama fagio la kuondoa sumu mbalimbali mwilini na ulaji wa kila mara wa tangu unasaidia kuondoa mawe katika figo (kidney stones).
Aidha tango linasaidia kukupatia vitamin.Tango lina vitamin nyingi zinazohitajika katika mwili kwa siku. Kuna vitamin A,B,C ambazo hupiga busti katika mfumo wako wa kinga kukupa uangavu na nishati unayoihitaji.
unaweza kufanya jusi ya tango kuwa na nguvu zaidi kw akuichanganya na karoti na spinachi.Usimenye tango lioshe na kulila na unaposaga kupata juisi vivyo hivyo kwani ngozi yake inavitamini C kiasi cha asilimia 123 ya inayohitajika kila siku katika mwili.

Upasuaji wa kibonyo shavuni waleta janga



Mwanamke mmoja mwenye makazi yake campbel, Uingereza amejikuta anaingia katika wakati mgumu baada ya kufanya upasuaji wa urembo kwa lengo la kutengeneza kibonyo shavuni.

Mwanamke huyo Cherelle Campbell, ambaye ni mwanasheria mtarajiwa, alikuwa mwanamke wa kwanza kufanyiwa upasuaji wa urembo kutengeneza kibonyo.

Upasuaji huo wa urembo unahusisha kutengenezwa kw amatundu kadhaa shavyuni kutengeneza muonekano wa kibonyo mtu anapotabasamu au kuongea.

Shughuli hiyo yenye gharama  ya dola za Marekani 2,500 imeletea shida binti huyo ambaye anasema kwamba sasa anajiona kama kituko, kwani matundu yameingia ndani zaidi.

Wednesday, February 5, 2014

Sabuni za kurudisha ubikira kumbe ni hatari


 
 KUWA mrembo ni pamoja na kujikubali jinsi ulivyo na jinsi utakavyojiweka soap soapHata mtu akikupenda akupende  jinsi ulivyo. Pamoja na hayo kumekuwa na mambo mbalimbali yanayofanywa na baadhi ya wanawake au wasichana kwa lengo la kufanikisha azma mbalimbali.
Miongoni mwa mambo hayo ni matumizi ya madawa mbalimbali ikiwemo yake ya kuongeza hips, makalio, kubadilisha rangi ya ngozi na hata kufanyia operesheni sura ili kuwa na muonekano ambao wanauona bora zaidi.
Pia kumekuwa na aina mbalimbali za sabuni kutoka ndani na nje ya nchi ambazo zimekuwa zikiuzwa ambazo zinadaiwa hurejesha ubikira zimesambaa sana madukani huku wateja wakubwa wakiwa ni wasichna na wanawake.
Hata hivyo walaatalam mbalimbali wanasema kuwa sabuni hhizo ambazo hutummika kwa kunawia sehemu za siti husaidia kurudisha bikira kwa mwanamke na hata kuwa na mnato.
Lakini wanaootumia sabuni hizo wameonywa kuwa  sabuni hizo zina kemikali zenye madhara makubwa kwa mtumiaji kwani zina uwezo mkubwa wa kusababisha kansa ya shingo ya kizazi.
Kwa mujibu wa Mkaguzi wa Dawa na Mfamasia wa Manispaa ya Dodoma Daria Mwanuka anasema hivi sasa kumekuwa na sabuni mbalimbali ambapo wanaoziuza wanadai zimekuwa zikisababisha bikira iliyopotea kurudi kitu ambacho si kweli.
Mtaalam huyo Anasema  Sabuni hizo zinapunguza tu majimaji  yaliyo sehemu za siri za mwanamke jambo ambalo husababisha wakati wa kufanya mapenzi mwanaume kupata ugumu kwenye muingiliano  kwa vile mwili unakuwa umekataliwa kutoa maji na hivyo kuleta michubuko kitu ambacho ni hatari hasa wenye maambukizi ya magonjwa.

Pia michubuko inapotokea ni rahisi mwanamke kuambukizwa magonjwa ya zinaa hata virusi vya Ukimwi. Sabuni hizo zinatengeneza hali fulani ukeni  lakini haiwezi kurejesha hali ya maumbile iliyopotea.
Mfamasia huyo anasema wanaotumia sabuni hizo wako katika hatari kubwa ya kuambukuzwa magonjwa na hata kupata saratanni ya shingo a usazi kwani kemikali zinazotumika katika kutengeneza sabuni hizo zina athari kubwa kiafya.
Anataka wanawake kutatambua thamani yao na kuachana na matumizi ya sabuni hizo ambazo hazina manufaa yoyote na badala yake zimekuwa na madhara makubwa kwao.

Mkaguzi wa dawa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kanda ya Dodoma, Fredrick  Luyangi  anasema mrudiano wa athari hasa kwa matumizi ya sabuni huleta athari kubwa mwilini na wakati mwingine kutengeneza kansa taratibu bila mhusika kufahamu.Sabuni hizo husababisha kansa ya kizazi na kubainisha sabuni hizo licha kupigwa marufuku zimekuwa zikiuzwa kwenye maduka ya vipodozi.
“Mara nyingi kwenye operesheni zinazofanyika zimekuwa zikiondolewa sokoni lakini hata hivyo zimekuwa zikiingizwa kwa wingi hali inayofanya zoezi la kudhibiti kuwa gumu” anasema.

Anawataka wanawake kuacha matumizi ya sabuni hizo ambazo zina madhara makubwa sana kwao kwani zikikosa wanunuzi zitaondoka sokoni.
Jamani wanawake wenzangu tubadilike Kuna wengine wameshazaa zaidi ya mara mbili lakini bado wanahangaika kurudisha maumbile yao yawe madogo na kuhangaika na kila aina ya sabuni inawezekana kweli katika hilo?

Miongoni mwa maneno yaliyokwenye sabuni za kunawia ukeni.