Monday, March 5, 2012

Jiweke hai kwa kula yai sehemu nyeupe


KUNA mambo mengi yanaweza kufanywa na yai, lakini moja ambalo pengine hulijui sawasawa ni kuwa yai, laweza kukusaidia kuwa macho kwa kipindi kirefu.
Taarifa hii ambayo ipo katika mitandao nakuletea kwako ili uweze nawe kuona faida ya kujisikia freshi kwa lengo la kuachana na usingizi singizi unaokuandamana ukiwa kazini.
Wanasema wataalamu wa lishe kwamba wewe kula yai moja tu mambo yako yatakuwa safi, usingizi hautakuandamana kwa kuwa sehemu hiyo nyeupe inafanya kitu fulani kusaidia uunguzaji wa nishati.
Wanasema kuwa ile sehemu nyeupe ya yai ndiyo hasa inayofaa kukufanya kuondokana na usingizi na pia kuwa timamu.
Maneno haya yametokana na utafiti uliofanywa na Chuo kikuu cha Cambridge ambao wamebaini kwamba protini ya yai ina nguvu zaidi kuliko carbohydrates zinazopatikana katika chokoleti, biskuti na peremende ambazo ndio huaminika kwa kuleta nishati
ya nguvu haraka zaidi.
Kwa maneno mengine watafiti wamebaini kwamba unaweza kuchagua ni ubongo gani wa sehemu gani ufanye kazi muda gani kwa kuangalia chakula unachokula.
Watafiti hao wanashauri kama kuna chaguo kati ya jam kwenye tosti pamoja na utamu wake mtu akikuwekea na sehemu nyeupe ya yai kwa tosti, kimbilia yai kwa tosti.
Pia wataalamu hao wamesema kwamba rehemu inayopatikana katika sehemu nyeupe ya yai ina msukumo mdogo sana wa kukupatia magonjwa ya moyo.

Samahani kwa kimya kirefu

Wasomaji wapendwa nimekuwa kimya kwa muda kidogo. Nilikuwa katika malezi. Lakini nadhani sasa naweza kuwatumikia tena katika libeneke letu hili la urembo tukiangalia afya zetu, uzuri wetu na siha njema karibuni sana.